Mradi mpya wa benki kuwasogezea wafugaji Tanzania ya Viwanda

15Mar 2019
Renatha Msungu
Dodoma
Nipashe
Mradi mpya wa benki kuwasogezea wafugaji Tanzania ya Viwanda

MOJA ya sheria, sera pia miongozo inayosimamia kampuni na mashirika ya ndani na nje ya nchi, ni kuwajibika kwa jamii, kuhudumia mambo mbalimbali ambayo jamii jirani inaweza kunufaika na shughuli za asasi husika.

Shughuli za ufugaji katika mandhari tofauti, ambazo zinatumia njia za asili. PICHA : MTandao

Aidha, shughuli za kitaasisi ambazo zinafanyika na hasa za kibiashara, zinatakiwa kugusa malengo ya kitaifa kuichumi. Hapo ikajulikana mojawapo, ni mkongwe kilimo, ambayo ni ‘uti wa mgongo’ wa taifa.

Benki ya NMB katika kujipanga kwake kuwainua kiuchumi wakulima na wafugaji, imeendana mpango bajeti yake katika miaka mitano ijayo, kwa ajili ya kuwahakikisha wanainuka kiuchumi.

Inaelezwa katika mpango huo, kuna sura inayohusu kuanzishwa viwanda vidogo vya uzalishaji maziwa pamoja na wakulima kujiinua katika soko la nje na ndani ya nchi.

Meneja Mwandamizi wa Idara ya Kilimo ya Benki ya NMB, Carol Nyangaro, anasema benki yake imetenga Sh. bilion 500 za kuwainua kiuchumi na tayari wakulima wameshaanza kukopa ili kujiendeleza na kilimo kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Nyanagaro, ni mpango ulioanza kufanyiwa kazi mwaka 2015 na unakamilika mwakani, huku akijigamba kuona mabadiliko katika kilimo hicho kinachofadhiliwa na mpango wa benki kupitia mkopo tajwa.

Mtazamo huo unakamata sura mbili za kilimo na ufugaji, ambazo ni sekta mbili zenye uhusiano wa karibu sana na zinaangukia katika kundi moja la tafsiri na hata uwajibikaji.

Kutokana na hilo, wakopeshaji hao wanawataka wakulima na wafugaji kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo ya fedha zilizotolewa ili kuhakikisha wanafanikisha wanachokikusudia mbele ya jamii.

Mbali na ufugaji, pia benki hiyo inawajibika na ukopeshaji katika maeneo mengi ya umma.

Nyangaro anaiabia Nipashe kuwa, hivi sasa wafugaji na wakulima kupitia mikopo hiyo wameanza kuonesha mabadiliko makubwa katika biashara zao ikiwemo uzalishaji mzuri wa maziwa, mtazamo wa mbali akiamini yatafikia kusafirishwa nje ya nchi.

Mkoa wa Dodoma ni sehemu mojawaopo ya maeneo mengi nchini na hasa mkoa ya Kanda ya Kati, ambako ufugaji uko juu na kwa maana hiyo hata uzalishaji maziwa uko katika kiwango kikubwa kiasi cha kukosa soko.

Pia, katika rekodi, Tanzania pia ni miongoni mwa nchi zilizo na ufugaji wa wanyama kama ng’ombe na mbuzi, katika ngazi ya juu zaidi barani Afrika.

Nyangaro anasema, kuwa katika mpango wa muda mrefu wa aina hiyo ya mkopo, ni kwamba wanalenga kutoa msukuko wa kimtaji na kiuwekezaji, utakaofikisha nchi kuwa na mtaji wa kutosha, ili kuhakikisha wafugaji na wakulima wanaingia katika soko la kimataifa.

"Kwa kweli tumejipanga sana labda wafugaji na wakulima washindwe kuja kuzikopa fedha hizo ili kujiendeleza," anasema Nyangaro.

Anasema NMB itahakikisha wanasonga mbele katika kutekeleza mpango mkakati wao, wanaoamini utaisaidia sana jamii katika sekta hiyo.

Waziri Mpina

Anasema, wameamua kuitisha mkutano wa wadau wa wafugaji na wakulima, kupitia wizara husika chini ya Waziri wa Mifugi na Uvuvi, Luhaga Mpina, ili kuhakikisha changamoto zote zinazowakabili, zinatatuliwa, bila ya kujali ukubwa wa tatizo.

Nyangario anafafanua kuwa, tayari wameshaweka mkakati wa kuwafikia wakulima na baadaye wafugaji, ili waweze kupata fedha hizo kwa ajili ya kujiendeleza katika kazi zao za kila siku.

Anasema, wameandaa mipango ya kipekee inayofuatilia kilimo na kuongeza idara hiyo inafanya vizuri na tayari asilimia 40 ya fedha zilizotengwa tayari zimepelekwa kwa wakulima kwa ajili ya kuendeleza kilimo.

Waziri Mpina mwenye dhamana ya Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina anakiri kuwa ni jambo zuri lililofanywa na benki ya NMB na mfano wa kuigwa, kwa sababu wameamua kuiendeleza sekta hiyo.

Waziri Mpina anaekeza imani yake, endapo itatekeklezwa ilivyolengwa pia na taasisi nyinginezo basi, sekta hiyo itakuwa juu na kusaidia uzalishai wa maziwa kufikia kiwango cha juu kama ilivyo kwa nchi jirani ya Kenya, ambayo iko juu katika uzalishaji wa bidhaa za mifugo.

"Tunaishukuru NMB tunaomba mpango mkakati wao uendelee hivi hivi,"anasema Mpina na kufafanua kuwa, zaidi kwamba endapo uzalishaji wa maziwa utaongeza tofauti na ilivyo sasa, basi soko litakuwa kubwa na kuzifikia nchi za jirani katika uzalishaji wa maziwa ya ng,ombe.

Anasema, hivi sasa Watanzania wanazalisha lita billion 2.4 kwa mwaka, wakati Kenya wako katika kiwango cha lita bilion 5.7, jambo ambalo ni fedheha ukilingaisha na kiwango cha mifugo iliyopo nchini.

Waziri anasema, Tanzania ina malisho mazuri, lakini imeachwa nyuma na majirani kama Kenya, huku akirejea imani yake kwa mpango wa NMB, kwamba wafugaji watauchangamkia ili kuweza kuinua uzalishaji kiwango cha maziwa na kuingia katika soko la ushindani.

Mfugaji

Mfugaji Peter Mlewa, anasema wana kila sababu ya kushukuru mradi huo, kutokana na kuwakumbuka sekta hiyo ambayo imekuwa ikisahaulika kila wakati.

Mlewa anasema, kwa sasa wataitumia vema nafasi waliopata kutoka benki hiyo kuhakikisha wanafikia malengo yao ya uzalishaji maziwa mengi ambayo yatasambazwa hadi nchi za jirani.

Habari Kubwa