Mtoto mwenye miguu mitatu apata matibabu ya aina yake

04May 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mtoto mwenye miguu mitatu apata matibabu ya aina yake

MTOTO aliyezaliwa nchini hapa akiwa na miguu mitatu, mmoja ukiwa umejiunga kwenye nyonga, matibabu yake yamefanyika kwa mafanikio yanayoweka rekodi mpya.

Hatua za kitabibu zilizofanyika nchini Australia, zimechukuliwa kwa kuuondoa mguu wa tatu, baada ya kupelekwa huko kwa msaada wa taasisi moja isiyo ya kiserikali ya Bangladesh.

Choity Khatun, ambaye mguu wake wa tatu unaelezwa na wataalamu kwamba ni sehemu ya pacha aliyejiunga hapo kwa namna yake.

Anasema hali hiyo ndiyo imesababisha kupatikane mguu huo kwenye nyonga, ikiwa sehemu ya pacha aliyejiunga kwa namna isiyo ya kawaida.

Daktari Chris Kimber, Mkuu wa Upasuaji huo uliofanyika katika Hospitali ya Victoria, naye anakiri kwamba ni aina ya upasuaji adimu waliowahi kukutana nao.

"Ni operesheni inayofanikishwa na mtu anayepaswa kutumia muda mwingi katika kufanya uchambuzi wa hali halisi na kisha kupanga namna ambavyo utatekelezwa” anaeleza daktari huyo.

Msingi wa mafanikio hayo, ni kwamba utekekezaji wake ulipitia awamu nyingi ya kujifunza na kutafiti, ukianzia na mjadala wa kina baina ya madaktari wa Bangladesh na wenzao wa Australia.

Daktari anaeleza namna upasuaji ulivyofanyika ni kwamba, sehemu ya nyonga iliondolewa na kisha ukafanyiwa maboresho ya kitabibu.
"Bado (mtoto) ameachiwa shehemu kubwa iliyopo pale na kati ya nyonga na miguu yake ya kawaida," anasema Dk. Kimber.

Anasema mtoto huyo wa kike alikuwa na viungo vingi vya siri viwili, vikiwemo vya haja kubwa na viungo vingine vingi vilivyokuwepo mara mbili na baadhi vikiwa katika mahali isiyo sahihi kwa mujibu wa maumbile ya mwanadamu.

Inaelezwa kuwa, baada ya ufuatiliaji huo wa kina, timu ya wataalamu iliingia kazini kutatua kwa mafanikio, Novemba mwaka jana.

Walianza kwa kuondoa mguu mmoja, kisha wakaufanyia maboresho uliobaki kuuweka vizuri na binti huyo mchanga asasa anautumia kama ilivyo kwa binadamu wenziwe katika maisha ya kawaida.

Dk. Kimber anasema mtoto huyo asiye na uono mzuri, hivi sasa anaweza kutembea na kukimbia kwa kiasi fulani, huku akiwa na maendeleo mazuri ya kuongezeka uzito wa mwili, jambo ambalo ni la kawaida katika maisha ya mwanadamu.

Mtaalam Dk. Kimber, anasema kuhusu maendeleo ya maisha ya mtoto baadaye, ni kwamba timu ya madaktari hao wamepanga kumfanyia upasuaji mwingine katika umri wake wa baadaye, atakapokuwa anaelekea kwenye ujana.

Kwa sasa inaelezwa yuko vizuri kiafya, akiwa na mama yake na wanatarajiwa kurudi nyumbani Bangladesh karibuni, bila zaidi la kityabibu.

Mama yake akizungumza wiki iliyopita, anaeleza kufurahia mafanikio hayo na kilicho mbele yake ni kwamba anatazamia safari ya kurejea nyumbani kusimamia mafanikio na maendeleo yake kiafya.

"Kila kitu hivi sasa kiko vizuri sasa. Anaweza kucheza kama walivyo, watoto wadogo. Tuko kama wengine," anasema.

Habari Kubwa