Mzizi wa janga la vita ya ardhi Kilosa

02Jun 2016
Christina Mwakangale
Dar es Salaam
Nipashe
Mzizi wa janga la vita ya ardhi Kilosa
  • ‘Chanzo cha migogoro ongezeko la watu, viongozi’

MIGOGORO ya ardhi inayoendelea katika maeneo tofauti nchini, imekuwa ikiwaathiri wakazi wake, hususan wafugaji na wakulima.

Mfugaji wa Mvomero, akiwaeleza wanahabari hali halisi ya mapgano katio yao na wakulima.

Kadri muda unavyoendelea, kuna mahitaji makubwa ya ardhi nchini na yanaongezeka, huku uwekezaji ukivutiwa zaidi na wageni, pia wakazi wake.

Changamoto kubwa inayokabili sekta hiyo ya ardhi ni uvamizi wa maeneo makubwa ya ardhi ambayo hayajapimwa na kupewa matumizi rasmi, kama vile ujenzi, kilimo na ufugaji.

Ni hali inayowafanya watu wengi kuvamia na kutwaaa maeneo hayo. Kwa mujibu wa takwimu rasmi kitaifa, maeneo yaliyopimwa rasmi nchini ni asilimia 10 pekee, eneo lisilopimwa ni hekta 615,000 likiwa halijapimwa.

Mazingira hayo huzaa msuguano baina ya wakulima na wafugaji, hali inayoishia katika vifo vya watu na mifugo kufa. Hayo ndio mazingira yanayotawala huko Kilosa.

Hivi karibuni taasisi ya Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), ilizindua Mradi wa Uwajibikaji katika Uwekazaji katika Ardhi (RIPL), uliowalenga wanajamii, watumiaji ardhi na wamiliki wadogo kuwa na taarifa, pamoja na kunufaika na ardhi.

Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa wafugaji, wakulima, asasi za kiraia, taasisi za serikali na wadau wengine wa ardhi.

MFUGAJI AFUNGUKA
Mfugaji Adamu Ole Mwarabu kutoka kijiji cha Parakwiyo wilayayaKilosa, mkoaniMorogoro, anaelezea namna wafugaji wanavyokumbana na changamoto ya kukosekana maeneo ya malisho.

Adamu anasema ana mifugo 50 ambayo anaitaja kuwa michache, kulingana na kiwango walicho nacho wafugaji wengi.
Mwarabu anayejitambulisha kuwa mfugaji wa kisasa, anasema sababu kuu inayowaathiri ni uhaba wa ardhi na kuachana mazingira ya kiwa na mifugo mingi isiyo na tija, kwani idadi ndogo ndiyo inayomuwezesha kuihudumia vizuri.

Anasema kwamba, amaeshuhudia migogoro mingi inayotokana na baadhi ya viongozi wa vijiji na serikali kupora ardhi ya wananchi.

Mwarabu anafafanua kwamba katika kijiji cha Mabwegere wilayani Kilosa, baada ya kuzuka mgogoro mwaka 2012 na shauri hilo lilipelekwa mahakamani.

Anasimulia kisa hicho kwamba, iliamuliwa kisheria eneo hilo kuwa la wafugaji, lakini utekelezaji wake unasuasua hadi sasa, ikiwa ni miaka 14 imepita.

Pia anataja kisa kingine cha mgogoro ni katika kijiji cha Kambala wilaya ya Mvomero, nako kuna mgogoro baina ya wafugaji na wakulima.

Katika hatua hizo za awalai wakati huo, ilipendekezwa kwa pamoja na na mamlaka za mkoa na wizara inayohusika na ardhi, utenganisha maeneo ya wanaosuguana.

UFUMBUZI USIOTEKELEZEKA
Mwarabu anasema hadi kufikia mwaka 2013, kulitokea mauaji ya wafugaji na wakulima watano wilayani Mvomero kutokana na migogoro ya ardhi.

“Mapendekezo yaliyotolewa hivi karibuni, walisema shimo lichimbwe, ili kutenganisha eneo la wafugaji na wakulima,” anasimulia Mwarabu.

Anaongeza:”Lakini ilionekana maeneo ya kimila ya jamii ya Kimaasai yalichukuliwa na kuwekwa upande wa wakulima.”
Mwarabu anadai uamuzi huo unarudisha nyuma jitihada za kuwaunganisha Watanzania, kwani kutenga jamii hizo kwa kuchimba shimo kunakuza migogoro na kuelekeza lawama kwa serikal, kwamba “Inashindwa kutatua migogoro.”
Ushauri wake kwa serikalini, ni kwamba iwalinde wananchi wake kwa kusimamia na kuimarisha ulinzi, kama inavyoelekezwa na Katiba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997.

Anasema kuna umuhimu wa kubaini wanaohodhi ardhi kubwa bila ya kuiendeleza, huku wafugaji na wakulima wengi wakikosa ardhi kwa kutoiendeleza migogoro.

Mwarabu anasema kitendo cha kumegwa ardhi za wafugaji na kuibadili kuwa hifadhi na mbuga za wanyamapori, kumepoteza haki zao.

Anatoa mfano wa ardhi zilizomegwa kuwa sni katika mbuga za Tarangire, Serengeti, Manyara, Ngorongoro na Mkomazi, jambo analosema limewaathiri wafugaji kubaki bila ya ardhi, katika baadhi ya maeneo walioshawekeza kwa maendeleo.

WADAU
Mkurugenzi wa TNRF, Joseph Lila, anasema kupitia miradi tofauti, taasisi hiyo inahakikisha kwamba serikali kuu, wadau, wawekezaji wanafahamu na kuitekeleza, miongozo ya kitaifa.

“Lengo letu ni kuweka uwazi na uwajibikaji katika masuala ya ardhi, ili wafugaji, wakulima na wawekezaji wasisababishe migogoro kila mmoja afahamu eneo lake na wajibu wake katika jamii,” alisema Lila
Anasema iwapo miongozo ikowekwa wazi, suala la uwekezaji katika ardhi litaifanya jamii kufahamu umuhimu wa uwekezaji katika maeneo yao, kiuchumi na kijamii.

“Jamii ishirikishwe katika masuala ya ardhi, kuwepo na uwazi ili itapunguza migogoro, jamii ifahamu manufaa ya uwekezaji, ili ijiandae kama ni kutolewa kwa eneo la ardhi wakijua kwamba watanufaika kwa upande wa maendeleo ya elimu, afya na uchumi,” anasema Lila.

MATUKIO
Kuna matukio mengi ya migogoro ya ardhi yanayoelezwa kusababisha wakulima na wafugaji kutoelewa na wengine kufikia hatua ya mapigano, huku kukiwapo athari ya mifugo kuuawa.

Mnamo Februari mwaka huu, mifugo, ikiwamo mbuzi, kondoo na ng’ombe ipatayo 75 ilikufa na mingine zaidi ya 200 ikijeruhiwa, baada ya kukatwa na mapanga kijijini Kambala, wilayani Mvomero.

Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba, alilazimika kufika eneo hilo, baada ya kutoke mapigano baina ya wakulima na wafugaji.

KINACHOFANYIKA
WizarayaArdhiNyumbanaMaendeleoyaMakazi, katikakupunguzanakuondoamigogorohiyo.

Mpimaji Mkuu wa Ardhi nchini kutoka wizara hiyo, Nassoro Duduma anasema wizara kupitia kitengo cha kuhakiki, kusimamia na kushughulikia migogoro ya ardhi kitaanza kazi rasmi.

Kitengo hicho kilicho chini ya Kamishna wa ardhi, kilichoanzishwa Aprili mwaka huu kilemelenga kuhakiki, kufanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na wadau wa ardhi, ikiwamo kushughulikia masuala ya ardhi.

Anasema wawekezaji wanaohodhi maeneo makubwa bila kuyaendeleza watanyang’anywa na kuyaga wa kwa wananchi walio na mahitaji ya ardhi pamoja na kwa wawekezaji ili kuyaendeleza maeneo hayo.

“Sasa tunakuja na huu mkakatiili ‘open space’ (eneo la wazi), eneo lililohifadhiwa tutaanza na Dar es Salaam, kisha mikoani Kanda ya Mashariki, mkoa wa Morogoro na Pwani baadaye nchi nzima, watu wajiandae kuondoka kabla ya dhahama haijawakuta, taasisi.

Mtu mmoja anayehodhi ardhi, tuna jina lake tutajua tu wasiyoyaendeleza maeneo hayo na kuyarudhisha katika benki yetu ua ardhi,” anasema Duduma.

Anasema migogoro mingi inachangiwa na watu kujitwalia maeneo kinyume na sheria na kwamba mkakati huu utapunguza hali hiyo iliyopo maeneo mengi nchini.

Habari Kubwa