Namna safari ya saikolojia, falsafa inavyoangukia kwenye afya binafsi

23Jun 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Namna safari ya saikolojia, falsafa inavyoangukia kwenye afya binafsi

KITAALAMU, ikiwamo kutoka maandiko rasmi ya kitaaluma, msamiati ‘maadili’ una mzozo mkuu wa mafundisho yanayotolewa katika nafasi mbalimbali, hasa katika malezi, kumuelekeza binadamu atende namna inayomjenga kimazingira na kiafya, yeye na jamii nzima.

Ndivyo ilivyo saikolojia na fasalafa ya maisha ya kikoloni, ilivyoagukia hatima ya afya. PICHA: MTANDAO.

Maadili yanayohitajiwa na watu wote, kimsingi yanafanana, lakini saikolojia na mazingira yake yanaweza kuwa tofauti kiasi. Ila huwa saikolojia yake inayowakana katika tabia na ufuasi, hubaki kuwa zao chanya na kubwa linalomfaa mtu kwa mengi, iwe kiafya mazingira na hata kiuchumi.

Watu tangu zamani wamekuwa na maadili kwa namna maalum, kulingana na imani kama za dini, utamaduni na falsafa za vikundi vya binafsi.

Kumekuwepo aina nyingi za maadili katika jamii na kwa ujumla inakubaliwa na wanadamu wengi, mtu binafsi na mazingira ya karibu zaidi, hata kiasili.

Aina zote za maadili zinaelezwa huwa zinasaidia kuwapo ushirikiano kati ya watu, kuwezesha maisha katika jamii na kuongoza maisha yao. Mfano hai wa maadili hayo ni katika ngazi za kiakili, kitaaluma na kifamilia.

Kabla ya ujio wa wakoloni wa Kizungu barani Afrika, historia inaonyesha amani ilitawala na maadili ya Afrika yakafuatwa na Waafrika wenyewe.

Lakini, saikolojia hiyo ilichukua sura tofauti zaidi panapo ujio wa wageni, kwa sura za wafanyabiashara, wamisionari na wapelelezi kuchukua nafasi.

Walio katika biashara walitambulisha bidhaa zao, pia dini pamoja na lugha kwa jamii za Kiafrika na kwa sababu pesa hazikuwepo wakati huo, walibadilishana bidhaa na wenyeji, kama vile miwani kwa shaba au almasi kwa kioo, mavazi kwa dhahabu.

Ni mpaka sasa, saikolojia hiyo inashuhudiwa katika jamii ikiwamo ya jamii za Kiafrika, kuenda kuvaa mavazi yenye utamaduni wa ugaibuni na hasa nchi za Magharibi, kama vile Bara Ulaya na Marekani.

Falsafa na saikoliojia hiyo ndio ikashika kasi hata katika imani za kidini, kinachoabudiwa na wageni kikachukua nafasi kuengua maadili na imani walozizikuta.

Hivyo basi, wamisionari walihakikisha wanapandikiza imani zao kwa Waafrika ili kulainisha mioyo yao kiimani na kuingiza maadili yao, jambo ambalo matokeo yake yakaingia kwa ndani katika maisha ya Mwafrika.

Ni aina ya mabadikliko yaliyomletea hata mageuzi ya kiafya muumini, kwa namna moja au nyingine, kutokana na mabadiliko ya matendo na nyendo zake. Mathalan, ama mtu kuanza kutumia au kuacha sigara na pombe, daima inagusa hadi mwelekeo wa afya yake kwa namna nyingi.

Wageni hao katika ujio wao walipeleleza mifumo yote ya uongozi wa Afrika kuunda mazingira ya mataifa yao, wakaingiza tawala zao na kuangusha tawala za Afrika.

Kurejea historia, hadi kufika karne ya 15, wapelelezi wa kigeni walifanikiwa kusaidia mataifa yao walikotoka, wakaingiza maadili ya uongozi wao kwa kusainisha mikataba tofauti, ikiwamo ya ulaghai kwa viongozi wa Afrika wasiojua kusoma na kuandika.

Ikisimama tafsiri hata katika hatua, hiyo kunazalisha sura ya imani, saikolojia na afya mpya ya mwenyeji anayebadilika.

Hapo ndio zama kunasikika majina kama ya Mjerumani Karl Peters aliyeingia mkataba dhidi ya mzawa Sultan Magungo wa Msovero, Tanganyika hata akawekwa chini ya utawala wa Mjerumani.

Baada ya kufanyika mkutano wa Berlin, Ujerumani uliofanyika kati ya mwaka 1884 na 1885, Afrika ikagawanywa kwa mataifa ya kizungu, kila dola mtawala mmoja ikawa na himaya yake, ikiwamo Tanganyika chini ya Mjerumani.

Hivyo ndivyo mila na desturi za Afrika zilibadilishwa kwa mara moja na watawala wa Kizungu, wakitaka wenyeji kufuata kile ambacho watawala wao walitaka kitekelezwe.

Waswahili husema ‘mazoea yajenga tabia’ na ndivyo ilivyokuwa, tabia mpya ikajengwa ndani ya nafsi za Waafrika wengi waliotawaliwa na Wazungu.

Hapo ikaenda mbali kukishuhudiwa maadili mapya yakizaliwa kuanzia mavazi, elimu, mlo, usimamizi wa mwili na nyanja nyenginezo kwa kasi ya teknolojia vinaendelezwa na kuzika maadili na matendo ya asili ya Bara Afrika.

Zao kuu linaloangukia hapo mbali na hali ya kiuchumi ni saikolojia, falsafa na sura kuu ya mwisho afya ya umma inayozaliwa upya.

Makala hii inaegemea tathmini ya kitaaluma ya mwandishi ambaye ni mwanafunzi katika Shule ya Uandishi wa Habari (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Habari Kubwa