Ndege wanaohama makazi yao mapema wakihisi joto kupanda duniani

17Jan 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Ndege wanaohama makazi yao mapema wakihisi joto kupanda duniani

WANASAYANSI wamefanya tafiti kadhaa na kubaini kuwa, kuna aina ya ndege ambao wakiona ishara fulani za joto kupanda katika mazingira yao huhama mapema kwenda umbali mrefu ili kuyanusuru maisha yao.

Ndege hao wanaohama,husafiri masafa marefu hadi kuwasili katika maeneo yao ya kuzalia ya asili kwa karibu siku moja kabla kulingana na kiwango cha ongezeko la joto duniani kupanda, utafiti umegundua.

Ndege hufikia katika maeneo yao ya majira ya kuzaliana kwa wastani wa siku moja mapema zaidi kwa kiwango cha ongezeko la joto duniani, kulingana na utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Edinburgh.

Utafiti wa kubaini hali halisi ya viumbe hao, ulifanywa kwa kuwahusisha mamia ya aina mbalimbali ya ndege katika mabara matano duniani ili kujiridhisha na mwenendo wao kwa kuzingatia hali halisi ya joto.

Matokeo ya utafiti huo ni matumaini kwamba, utawasaidia wanasayansi kuweza kutabiri jinsi aina mbalimbali ya ndege wanavyoweza kukabiliana na mabadiliko ya baadaye ya mazingira.

Ndege hao, hujikuta wamefika kwa wakati mbaya katika viwanja vyao vya majira ya kuzaliana - hata kwa siku chache –mazingira yanayoweza kusababisha kukosekana kwa upatikanaji wa rasilimali muhimukwa ajili ya kuyafanya maisha yaende kikamilifu kama vile chakula na maeneo ya kutengenezea viota.

Kuchelewa kuwasili katika maeneo ya kuzaliana kwa upande wao, yaweza kuathiri majira ya kuzaliana na kutotolewa vifaranga na nafasi yao ya kuishi.

Ndege wahamiaji wanaosafiri umbali mrefu, ambao ni dhahiri huwa hawachukui maamuzi ya haraka kuhama wakati joto linapoongezeka , na wanaweza kuathiriwa sana wakati ndege wengineo wenye hisia za joto wananufaika na mabadiliko ya hali ya hewa katika maeneo yao kisha kusafiri na kuwasili katika maeneo ya kuzaliana mapema zaidi ikilinganishwa na ndege wengineo.
Maua na viota vya kuzaliana.

Takuji Usui, wa shule ya baiolojia ya sayansi katika Chuo Kikuu cha Edinburgh, alisema: " Mimea mingi na jamii ya wanyama hujirekebisha kulingana na ratiba za majira ya shughuli zinazohusiana na mwanzo wa kati ya masika na kiangazi, yanapozaliana maua na kuzaliana.

"Sasa tunauelewa mpana wa namna gani ndege wahamiaji wanavyobadilika kulingana na majira yanavyobadilika na jinsi mabadiliko hayo yanavyotofautiana miongoni mwa makundi tofauti ya ndege.”

"Ufahamu huu unaweza kutusaidia kutabiri jinsi ndege wanaohama wanavyosafiri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa katika maeneo ya viota vyao vya kuzaliana."

Utafiti huo wa wanasayansi ulichunguza jinsi aina mbalimbali ya ndege, ambao huchukua hatua katika kukabiliana na hali halisi kama vile mabadiliko yamsimu wa joto na upatikanaji wa chakula, zimebadilisha tabia zao baada ya muda kulingana na ongezeko la joto.

Watafiti walichunguza rekodi ya uhamaji wa ndege yapata miaka karibu 300 iliyopita.

Utafiti umekusanya taarifa ya rekodi kutoka kwa watafiti huru na wanasayansi, pamoja na maelezo kutoka kwa mwanasayansi wa asili wa karne ya 19 wa Marekani aitwaye Henry David Thoreau.

Aina ya ndege wanaohama kwa masafa marefu ni kama vile mbayuwayu na flycatcher - na wale walio katika kundi la wahamaji wa umbali mfupi - kama vile lapwing na pied wagtail– walijumuishwa katika utafiti huo.

Utafiti huo, ulichapishwa katika jarida la Ikolojia ya wanyama (Animal Ecology), kwa msaada wa Baraza la Utafiti wa Mazingira Asili

(Natural Environmwnt Reasearch )
Imetafsiriwa toka BBC

Habari Kubwa