Ndoa jinsia moja ilivyoanzia kujificha zama hizo hadi uzazi

27Feb 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Ndoa jinsia moja ilivyoanzia kujificha zama hizo hadi uzazi
  • Leo ni mabibi, mtoto ana miaka 45

MWAKA 1971, kutokana na kuzinduliwa vuguvugu la wanawake liitwalo Women Liberation Movement , Profesa wa Chuo Kikuu katika jimbo la California, Lillian Faderman, aliwasiliana na mkurugenzi mmoja wa kituo hicho aitwae Phyllis Irwin, kufungua programu ya utafiti wa wanawake.

Ilikuwa mwanzo wa mapenzi yaliyodumu nusu karne , lakini yakakumbwa na changamoto nyingi. Wakati walipokutana kwa mara ya kwanza, mapenzi ya jinsia moja yalikuwa haramu.

“Tulionekana kuwa wahalifu karibia katika kila jimbo,” ni kauli ya wanandoa hao na kuiendelea:''Wapenzi wengi wa jinsia moja walikuwa wakijificha.''

Ni hatua ya pingamizi, japo halikuwazuia kuanzisha familia, huku wakijificha nyuma ya sheria kwa ajili ya kutambuliwa kuwa kundi rasmi la kifamilia.

Wanawake hao wanasimulia namna walivyopata mbinu za kutumia sheria ili familia yao iweze kutambuliwa, katika zama hizo jamii ilikuwa inalipinga.

Phyllis, mwenye miaka 91 sasa, anasema walipoanza uchumba, hawakujionyesha moja kwa moja kuwapo mapenzi ya jinsia moja kati yao, kwani walilifanya hilo kwa kuendesha uhusiano kwa siri kubwa.

''Lakini wengine walidhani kwamba walijua uhusiano wetu katika chuo kikuu. Walituita Phyllis na Lills kwa sababu tulikuwa pamoja kila mara,'' anasimulia, huku akiangua kicheko.

''Nadhani wenzetu walituelewa na nilipoanza kuchapisha vitabu kuhusu historia ya wapenzi wa jinsia moja, niliona kana kwamba kila mmoja wetu alielewa kwamba tulikuwa wanandoa,” anaeleza.

Miaka mitatu ya kudumu uhusiano wao, waliamua kupata mtoto. Lilian ambaye ni mdogo kwa miaka 11, alienda kumuona mtaalamu wa masuala ya ujauzito.

Hata hivyo, kupewa ujauzito kwa njia ya kisayansi, halikuwa jambo la kawaida, hususan kama mtu hana uhusiano wa kimapenzi na mwanamume, lakini Lillian alifanikiwa kumshawishi daktari amsaidie.

Alijenga hoja pasipo kueleza ukweIi wa kilichomfanya yeye kutaka mtoto bila ya kuwa na uhusiano na mwanaume, akisimulia ilivyokuwa: ''Daktari aliniuliza kwa nini sijaolewa iwapo nataka kuwa na mtoto?, anakumbuka.

''Nilimjibu, nina umri wa miaka 34, nina shahada ya udaktari na wadhifa wa Naibu wa Rais wa Elimu katika chuo, nadhani inagharimu kupata wanaume,” anasema.

Anakumbusha namna daktari alivyomjibu kirahisi kwa kauli: “Naelewa unachosema na alinipachika mimba hiyo kupitia mbinu hiyo ya kisayansi ambayo ilifanikiwa.”

Kwa mujibu wa Lilian, wakati huo sheria haikuwaruhusu wanawake kuoana. Anaendelea: “Tungefurahia kuoana, sheria inasema haiwezekani mtoto kuwa na wazazi wa jinsia moja na tulijua kwamba ilikuwa muhimu kuwa na mshikamano wa kisheria, kwa sababu ya Avrom (mtoto wao).''

Anataja faida ya kumchukua mtoto Avrom na kuishi naye ni kwamba, alizaliwa wakati hapakuwapo watoto wengi wenye wazazi wa jinsia moja na njia rahisi ya kubadilisha hilo ni kumtambulisha mtoto Phyllis ni bibi yake, huku mtoto naye alimuona ni rafiki wa mama yake.

Wamekuwa watatu

Mzaliwa huyo wa mwaka 1975 hivi sasa ana umri wa miaka 45, mama yake Lilian alijifungua mtoto kwa jina Avrom na aliyempeleka hospitalini alikuwa ‘mumewe’ Lilian alipotaka kujifungua, huku akijawa na hofu.

Kila kitu kilifanyika ilivyopangwa na mwanamke huyo alirudi nyumbani, kuanza maisha mapya ya watu watatu.

Hata hivyo, wakaanza kugundua vikwazo vya familia yao kisheria, Lili akieleza: ''''Kile kilichotutia wasiwasi zaidi ni kwamba, Avrom alikuwa mgonjwa na Phyllis alilazimika kumpeleka kwa daktari. Hakuwa mzazi wake kamili, hivyo basi nililazimika kumpatia barua rasmi aliyobeba.''

Kilichonikwaza hasa ni kwamba, iwapo kitu kingenitokea, asingekuwa na haki kisheria kudai kuwa mwanawe, kwani ‘mume’ huyo hakujulikana kisheria.

Lilian anarejea mwongozo wa kisheria jimboni California, iwapo kuna tofauti ya miaka 10 au zaidi kati ya watu wawili wazima, mmoja anaweza kumchukua na kuishi naye, jambo lililompa fursa Phyllis, kwa kuwa pengo la kiumri lipo.

Lilian anasema, uhusiano wake na Phyllis ulikuwa na sura ya ‘kuchumbiana’ na anasimulia zaidi: “Hatukuliona suala hilo kuwa baya (tofauti ya kiumri) kwa sababu hatukujihisi kama mama na mwanawe, tulifanya hivyo kama njia ya kukwepa sheria.”

•Habari na picha ni kwa mujibu wa BBC

Habari Kubwa