Njia bora za kuepuka maradhi Trakoma, Vikope na Kichocho

14Mar 2019
Barnabas Maro
Dar es Salaam
Nipashe
Njia bora za kuepuka maradhi Trakoma, Vikope na Kichocho

TRAKOMA au vikope ni ugonjwa hatari uliosababisha upofu (ugonjwa wa kiumbe kutoona) kwa Watanzania wasiopungua milioni moja. Ni ugonjwa unaoshambulia macho na usipowahi matibabu, inaweza kusababisha upofu usiotibika.

Mgonjwa wa Trakoma.

Dalili zake ni pamoja na macho kuwasha, yanakuwa mekundu, yanatoa tongotongo kwa wingi, kutokana na kuuma au mtu anapoamka asubuhi.

Maambukizi ya Trakoma yanapoendelea baada ya miaka mingi, kope za macho hugeukia ndani na kukwaruza kioo cha jicho. Hali hiyo ndiyo inayoitwa ukope.

Wataalamu wa afya wana maoni kwamba, mtu anapogundua kuwa na mojawapo ya dalili hizo, asisite wala kufanya usiri katika kuchukua hatua ya kwenda kwenye kituo cha kutoa huduma za afya, kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Trakoma au Vikope, inaweza kuepukwa kwa kuchukua hatua kadhaa: Mosi, ni kuhakikisha mazingira ya nyumba na choo kuwa safi kila wakati, hali inayofukuza nzi wanaofuata uchafu, kwani ndio waenezaji wakuu wa Trakoma au Vikope.

Mhusika anatakiwa kunawa kwa maji kila siku, ili kuhakikisha nzi hawatui usoni na machoni mwake. Uso wa mtu unapokuwa na tongotongo au uchafu wowote, huwavutia nzi, ambao ndio waenezaji wakuu wa ugonjwa huo.

Pia, mhusika anapaswa kuhakikisha kwamba si yeye peke yake unayenawa uso katika jumuia yake, bali wanafamilia na jamii yake, kama vile watoto wadogo; huku wakinawa uso kila mara kujikinga mara moja kwa mwaka.

Tiba ya Trakoma/Vikope

Ili kupona, mtu anapaswa kumeza dawa maalum ya kama kinga tiba ya Trakoma/Vikope. Endapo kope zimeanza kukwaruza kioo cha jicho, mtu anapaswa kuwahi kituo cha huduma za afya na kusawazishwa kope husika, ili zisiharibu kioo cha jicho na kulipofua.

Huduma ya kusawazisha kope ni rahisi na huchukua muda mfupi tu.

Kichocho/ Minyoo Tumbo

Ili kudhibiti ugonjwa wa Kichocho na Minyoo ya Tumbo, inaelezwa umuhimu wa kujua jinsi ugonjwa huo unavyoenezwa.

Kichocho kuinaenezwa kupitia ama kuoga au kuogelea kwenye maji yaliyotuama, kwa maana ya kitu cha majimaji kinachoweza kumiminika kama vile maji na maziwa, madimbwi au mabwawa.

Mtu akijisaidia ovyo, nako minyoo ya tumbo inaenezwa kwa kula mboga, matunda yasiyooshwa vizuri na kula vyakula visivyoiva vizuri, hali kadhalika kutovaa viatu.

Nazo zina dawa zinazotibu na kukinga na baadhi ni za kumeza.

Zinavyoepukwa

Kichocho: Hiki kinaepukwa kwa ama kutooga au kuogelea kwenye maji yaliyotuama, madimbwi au mabwawa na kujisaidia ovyo.

Njia ya kujiweka mbali, mojawapo ni kuvaa viatu wakati wote, matumizi sahihi ya vyoo na kumeza dawa kama inavyoelekezwa na matabibu.

Minyoo: Inashauriwa mhusika kusafisha matunda na mboga kabla kuzijala, mtu anpaswa kula chakula kilichopikwa vizuri na kuiva.

Mengine ni umuhimu kwa kuvaa viatu kwa usahihi na kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka, kabla ya kula na kila mtu atokapo chooni.

Kitabibu, kuna umuhimu wa mtu kumeza dawa inayotajwa mara moja kila mwaka, kuboreshe afya yako.

* Makala hii ni kwa mujibu wa mamlaka za kiafya, chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Baruapepe: mar[email protected]
Simu: (+255) 07784 334 096.

Habari Kubwa