Nyama iliyosheheni mashabiki wengi, daktari akiwapa ‘vigezo na masha

21Jan 2021
Sabato Kasika
Dar es Salaam
Nipashe
Nyama iliyosheheni mashabiki wengi, daktari akiwapa ‘vigezo na masha
  • Unataka kula? Zingatia haya hapa

NYAMA ya nguruwe katika zama za karibuni, imeingia katika orodha ya kupendwa sana katika sura ya kitaifa.

Kihistoria nchini ilijulikana baadhi ya mikoa kama Mbeya kulikofugwa na kuliwa kwa wingi, lakini kadri muda ulivyoenda, hasa kuanzia mwishoni mwa miaka 1980, ulaji uliongezeka, Dar es Salaam, ikiibuka mwenyeji.

Leo imefikia hadhi kuwa miongoni mwa mlo unaopendwa sana mijini, ambako si haba imejaa kwenye bucha na mishikaki yake imejaa kwenye ‘vituo vya msaada’ vingi, vinavyojumuisha baa, baadhi ya wateja wakiunganisha na mseto ‘moja moto moja baridi.’

Umaarufu wa nyama hiyo, umesababisha ipatiwe majina mengi bandia, ikiwamo 'Noah' na 'Kitimoto', ambayo sasa ina hadhi ya msamiati pori, ikiwa rasmi kila kona.

SHIDA ILIYOPO

Ulaji nyama hiyo inayowakonga walaji, pia ina upungufu wa kuzaa matatizo ya kuwa na magonjwa inajumuisha 'African Swine Fever' ambao ni minyoo ya tegu.

Ni aina ya maradhi yanayotajwa na wataalamu wa magonjwa ya mifugo kuwa mlaji nyama ya nguruwe anaweza kudhurika, iwapo itapikwa na kuliwa bila kuiva vizuri.

Utaratibu wa kitabibu wa kiserikali ni kwamba, kila penye mlipuko wa ugonjwa tegi unapowakumba nguruwe, serikali hupiga marufuku ulaji, uuzaji nyama yake hadi hali inapokuwa shwari, ndipo unaendelea.

Mtaalamu na mstaafu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Sero Hassan Luwongo, anaueleza kuwa ni ugonjwa usiokuwa na chanjo wala tiba, bali nguruwe kuwekwa ndani ya karantini hadi uishe.

Katika mazungumzo yake na Nipashe, Dk. Luwongo anasema, ulaji wa nyama ya nguruwe isiyoiva vizuri, inamsababishia mlaji kukumbwa na ugonjwa wa kifafa.

Anafafanua kuwa nyama ya nguruwe inapokuwa na minyoo na haijaiva vizuri, inasababishia mlaji kupata uvimbe kwenye ubongo na ndipo inafuata uwezekano wa kupata kifafa.

Dk. Luwongo anasema uvimbe wa ubongo upo wa aina nyingi, akiufafanua: "Nguruwe ana magonjwa kama walivyo wanyama wengine ambayo yanatibika, yakiwamo ya kwato, lakini minyoo ya tegu inayoitwa African Swine Fever, haitibiki na ndiyo yenye madhara."

Anasema, nyama ya nguruwe ina minyoo ambayo ni wagumu kufa, hali inayotoa uwezekano wakaingia mwilini na kujenga uwezekano wa kufika kwenye ubongo, jambo linalojenga uwezekano wa madhara hayo.

"Virusi hivyo havina tiba wala chanjo. Njia pekee ni kupika nyama na kuhakikisha imeiva vizuri, pia ugonjwa unapolipuka, ni kupiga marufuku usafirishaji, ulaji wa nyama ili kuzuia ugonjwa usisambae,|” anasema.

MLIPUKO NCHINI

Ni ugonjwa unaotajwa kuibuka kila mara nchini na mwaka 2017 ulitua katika wilaya za Kalambo mkoani Rukwa na Dodoma na kusababisha viongozi kupiga marufuku ulaji nyama ya nguruwe.

Pia hatua ya karibuni ni kwamba umetua wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, unadaiwa kuua nguruwe zaidi ya 500 na serikali kupitia ofisi ya wilaya, alipiga marufuku uuzaji, usafirishaji na ulaji wa nyama ya nguruwe kwa muda usiojulikana hadi hali itulie.

Mkuu wa Wilaya, Anamringi Macha, anasema ni hatua ya kudhibiti kuenea maambukizo ya ugonjwa huo unaodaiwa kuua nguruwe kwa kasi wilayani kwake na wataalamu wetu wanaendelea kufanya utafiti kuhakikisha wanaudhibiti, ili kuzuia madhara zaidi yasijitokeze.

Aidha, Macha anawataka walaji nyama ya nguruwe wilayani mwake kuachana nayo hadi watakapotangaziwa na serikali, hivyo watumie mbadala wa nyama ya mifugo kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku kwa kuwa hawajaathiriwa na ugonjwa huo.

KULIVYO DUNIANI

Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na The International Agency for Research on Cancer unamtaja nguruwe ni mnyama, nyama yake inaliwa kwa wastani na asilimia 38 ya wakazi wote duniani.

Hata hivyo, anatoa kasoro kuwa nyama hiyo ina madhara makubwa, akitaja ni sumu ya anayoiita ‘carcin-ogen’ inayosababisha ugonjwa wa saratani.

Kwa mujibu wa watafiti hao wa WHO, wanaainisha pale kila siku mtui alapo gramu 50 ya nyama ya nguruwe, ana uwezekano wa kupata saratani kwa watani wa asilimia 18.

Utafiti uliofanyika 1998 wa WHO, ulionyesha nyama ya nguruwe iliyopikwa kwa nyuzi joto 104C, bado zaidi ya nusu (asilimia 52.37) ya minyoo iitwayo ‘trichinella worm’ hawafi.

Hiyo ni minyoo ambayo inapoingia mwilini mwa binadamu, husababisha ugonjwa uitwao ‘trichinosis’ ambao dalili zake kwa mgonjwa zanajuimuisha homa kali; kichwa kuuma; kukosa nguvu; maumivu ya nyama za mwili; macho kuwa rangi ya pinki; kuvimba uso na kope; na kudhuriwa na mwanga.

WHO inatahadharisha namna kuwapo minyoo aina tofauti waitwao kitaaalamu ‘ Taenia solium’ mlaji nyama anaweza kuipata isipopikwa vizuri na inasababisha matatizo ya mfumo wa fahamu na ndio chanzo cha maradhi ya kifafa.

Pia inaelezwa ni aina ya nyama yenye virusi vinayosababisha homa ya ini aina ‘E’ na kuna kuna wadudu wanaobaki ambao nao wana madhara tofauti mwilini kwa binadamu mlaji.

FAIDA & HASARA

Hadi sasa inaelezwa asilimia 30 ya wagonjwa wote duniani wenye kifafa huwa ni wanaoshambuliwa na minyoo hiyo ipatikanayo kwenye nyama ya nguruwe isiyoiva vizuri.

Inaelezwa kuwa watu milioni 50 duniani kote wenye kifafa ni walaji wa nyama ya nguruwe kwa namna tofauti kama vile soseji, au nyama iliyopikwa.

Pia kuna faida ikitajwa vitamini muhimu katika mwili wa binadamu; ambazo ni B1, B6 na B12 na walaji wanapata madini chuma, yanayowasaidia kuimarisha mifupa, huku magnesium inayosaidia mwilini mwa binadamu.

Mengine ya manufaaa ni viini lishe vya protini ya kutosha, ambayo inachangia kujenga mwili, pia mafuta yanayoufanya mwili kupata nguvu.

Nyama ya nguruwe inaingia katika orodha ya kuimarisha ngozi ya mlaji kuifanya iwe laini.

Habari Kubwa