Pata vigezo vya utata biashara kuporomoka

17Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Pata vigezo vya utata biashara kuporomoka
  • Utafiti: Nusu miradi inakufa

UTAFITI wa usimamizi wa biashara, unaonyesha kuwapo tabia nusu ya biashara zinazoanzishwa, zinakufa kabla ya miaka mitano, theluthi ndio zinafanikiwa kufikisha miaka 10. Kwa kifupi, ni nusu pekee za biashara ndio zinavuka safari hiyo.

Biashara zilizoshamiri Kariakoo jijini Dar es Salaam. PICHA: MTANDAO

Jarida la Forbes kwa msaada wa utafiti uliofanywa na channel za kibiashara inaonyesha biashara nane kati ya 10 (asilimia 80) hufa ndani ya mwaka mmoja na nusu.

Nini chanzo chake? Kuna sababu kadhaa zinazoorodheshwa

TATIZO USIMAMIZI

Uongozi dhaifu unaweza kudhihirisha kuwa mizozo ya kila mara baina ya viongozi wa timu yao ya kazi, kukinzana maoni ni tatizo.

Inaelezwa hatari ya kufanya uamuzi unaochelewa, au tatizo kutoshughulikiwa kwa wakati sahihi, ndivyo mwanzo wa biashara kulega.

Hatua stahiki hapo, ni kukubali kujifunza, kusoma mbinu za uongozi kadri iwezekanavyo hata kuhudhuria madarasa husika. Tafuta mwalimu binafsi wa biashara (mentor), fanya utafiti binafsi na kila aina ya mbinu kunyanyua uwezo wako wa kuongoza, kisha zichanganue mbinu zote za uongozi na chagua iliyo bora kwa biashara yako.

THAMANI PEKEE

Wakati mtu anaweza kuwa na bidhaa au huduma bora inayohitajika sana sokoni, bado anafanya vibaya sokoni. Huenda kunakoseka kuonyeshwa thamani ya bidhaa sokoni au ina washindani wengi, kuifanya bidhaa yako kuwa juu sokoni.

Swali la msingi hapo ni kujiuliza, kitu gani kinakutofautisha na wapinzani wako, unatumia mbinu gani kuwa tofauti na wenzako, washindani wako wanafanya nini hata kuikushinda?

Baada ya kuyajua hayo, boresha biashara na tengeneza mfumo na kifurushi cha huduma ambayo hakuna mwingine anaitoa katika soko, kiasi itachukua umakini wa wateja na kuwafanya waipende huduma au bidhaa yako.

Hivyo ndivyo vitatengeneza chapa yako na ndio inatoa taswira ya huduma yako kwa mteja kuitumia chapa hiyo. Itumie chapa hiyo, kwani ndio utambulisho wako; rangi au, kaulimbiu na vitu vingine vinavyoonekana, ikiwamo sera.

Kimsingi, sera ni lazima iwakilishe thamani ya bidhaa au huduma inayotolewa.

Ili kuifanya chapa yako ifahamike, lazima utumie mbinu nyingi za masoko na usiogope kusimama kwenye matukio ya kijasiriamali kuongea au kuweka vipeperushi vyako.

MAWASILIANO DUNI

Kupuuza wanachosema wateja au kutokuwa karibu nao, ni dhahiri biashara italega. Inashauriwa kuwa karibu na wateja na kuyaelewa mahitaji na mrejesho wanaokupatia.

Wateja wanaweza kuipenda bidhaa au huduma itolewayo, wangeipenda zaidi kama kitu fulani kingeboreshwa. Cha kufanyika hapo ni aliyefanikiwa, huweka mkazo katika bidhaa iliyoko sokoni kujua wateja muhimu na wanavutiwa vipi na bidhaa au huduma hiyo na utengeneze njia bora ya kusimamia uhusiano na wateja.

MFUMO USIOFAIDISHA

Moja ya viashiria vikubwa vya kuanguka biashara, ni kuwapo mfumo thabiti wa kuendesha biashara ni mpango kazi na ‘kukomaa’ na safari ya tija, kwani wazo la biashara linaweza kuwa zuri, lakini kukosekana mikakati ya uongozi kunachangia kuanguka biashara hiyo.

Muhimu hapo ni kutafuta utafiti na rejea, kisha kutengeneza mfumo kamili wa mpango wa biashara ambao unahusisha makadirio ya mapato yanayotegemewa, mikakati ya masoko na ufumbuzi wa changamoto za usimamizi katika kuvivuka vikwazo muhimu vya masoko na wapinzani.

Andaa jedwali linaloonyesha kazi husika na malengo yaliyoambatanishwa na ukomo wa muda. Ili kuweza kuyapima mafanikio, kutatua changamoto zinapojitokeza na kubaki katika njia sahihi. Mpango kazi thabiti unahusisha mbinu sahihi na unasaidia biashara yako kutoanguka.

KUSIMAMIA FEDHA

Ili kufanikisha biashara, fedha inayopatikana na kutumika isimamiwe. Ni vyema kuandaa fungu la dharura kuokoa majanga ya fedha au biashara yanapojitokeza.

Mara nyingi watu huanzisha biashara wakiwa na ndoto za kutengeneza fedha, lakini hawana ujuzi wa usimamizi wa mzunguko wa fedha, kodi na gharama.

Utatuzi bora ni kuhifadhi kumbukumbu za fedha na miamala yote, ikiwamo kujumuisha matumizi na mapato yote, kisha kutumia taarifa kutengeneza jedwali la faida na hasara, zitakazosaidia kuonyesha mwenendo wa biashara.

UKUAJI GHAFLA

Kuna wakati biashara mpya inakuwa kuliko inavyoweza kustahimili. Unaingiza bidhaa sokoni na ghafla unapokea maombi mengi kuliko unavyoweza kuhudumia.

Pia mambo yanakuwa tofauti, unashawishika kuwa bidhaa zako zitauza sana na unaweka bidhaa nyingi ghalani, mwishowe soko linakuwa tofauti na mtu anabaki kutapatapa, bila namna ya kujinasua.

Kukua na kupanuka biashara kunahitaji umakini wa mipango na mikakati unaohusisha usimamizi wa uzalishaji wa siku baada ya siku, ikihusisha
utafiti katika kupima mgawanyo wa watu katika eneo husika na kiwango cha mapato.

Aina ya bidhaa na mipango endelevu ya eneo husika.
Tafiti hizi pia lazima zijiridhishe kuwa wakati ni sahihi na fedha kwa mpango huo zipo.

Mmiliki anatakiwa ahakikishe biashara iliyopo ni imara kabla ya kuanza kujitanua, pia asiongeze bidhaa ambazo hana uhakika kuziuza.

Kuanzisha biashara ni jambo la kusisimua sana na linahitaji bidhaa au huduma iliyojikamilisha, kwa kuwepo huduma au bidhaaa hiyo sokoni.

Kama una mpango wa kuanzisha biashara au tayari una biashara yafaa ujue kuwa mafanikio yako yanategemea umakini wa mipango na mikakati yako na umakini wa usimamizi wa fedha tangu mwanzo mpka mwisho wa biashara.

* Ni kwa mujibu wa taarifa za biashara mtadaoni

Habari Kubwa