Profesa Kezilahabi: Mkongwe wa Kiswahili aliyeiaga dunia

14Jan 2020
Michael Eneza
Dar es Salaam
Nipashe
Profesa Kezilahabi: Mkongwe wa Kiswahili aliyeiaga dunia
  • Mtunzi Rosa Mistika, Dunia Uwanja Fujo…

BINGWA wa Kiswahili aliyegeuka kiongozi wa kisiasa, Profesa Euphrase Kezilahabi hayupo nasi tena, akiaga dunia miezi mitatu kabla ya kufikisha umri wa miaka 77 hapo Aprili 13.

Marehemu Profesa Euphrase Kezilahabi. PICHA: MAKTABA

Kwa wanaojua, wana tarehe inayofanana na ya kuzaliwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, tofauti yao ni miaka ya vifo.

Akiwa anatofautiana na wenzake wengi katika klabu ya waandishi wa riwaya au hadithi, Hayati Kezilahabi alikuwa msomi aliyefundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kwingineko.

Kote alikokuwa kati ya wale wenye mvuto wa kipekee zaidi kati ya waandishi wa riwaya. Alichangia sana katika kutoa tafsiri na tathmini za fasihi barani Afrika na akeanda mbali katika uchangiaji ujenzi wa fasihi kwa riwaya, kazi zake zikisomwa hapa nchini na kwingineko.

Kuingia kwake katika siasa hapakuwapo kishindo sana kuhimili cha taaluma. Zaidi, atakumbukwa kuwa mmoja wa wabunge wa upinzani walioiona kazi nzuri anayoifanya Rais Dk. John Magufuli na kuunga mkono angalau kwa hisia ya maendeleo kutokuwa na vyama.

Anakiri hivyo, akimkaribisha au kutoa salamu, wakati Rais Dk. Magufuli alipotembelea jimbo lake katika mojawapo ya ziara zake mikoani mwaka jana.

Ni kwa njia hiyo, pia alifahamika hasa katika kipindi cha ujana wake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati huo ikiwa inafukuta kwa mikondo tofauti ya kiharakati na kiitikadi, lakini alifahamika kwa utunzi, siyo harakati.

SAFARI YAKE

Maisha ya Prof. Kezilahabi, yanaelezwa alizaliwa Aprili 13, mwaka 1944, huko wilayani na katika taaluma alipasishwa kuwa Profesa Mshiriki katika Chuo Kikuu cha Botswana, Idara ya Lugha za Kiafrika.

Historia yake inagusa kwamba aliandika kazi zake kitalauma kwa Kiswahili na ameshatoa machapisho ya kitaaluma katika fani ya fasihi, iwe ni kwa kazi za Kiswahili au nyinginezo barani Afrika.

Mojawapo, inatajwa kuwa ni ‘Mkanganyiko wa Maudhui katika Kiswahili cha Kisasa’ (Aesthetic Ambivalence in Modern Swahili) na “Dhana ya Shujaa katika Riwaya za Kiafrika” (The Concept of Hero in African Literature).

Ni kazi aliyoungana na mhakiki fasihi mwingine ambaye si mwandishi sana wa riwaya za Kiswahili, Profesa Fikeni Senkoro katika uchambuzi wa ‘Kahaba katika Fasihi ya Kiafrika.’

Kazi moja iliyofahamika sana ni ‘Dunia Uwanja wa Fujo’ iliyochapishwa mwaka 1985 na mshangao wa baadhi ya wakongwe, kazi ya ujana wake iitwayo ‘Rosa Mistika’ ambayo katika chapisho la awali ilipigwa marufuku.

Baadhi yetu awali katika miaka ya 1970 mwanzoni, tulikuta imepigwa marufuku, baadhi yetu tunakumbuka wakati tunaingia shule za sekondari tulikuta tangazo ubaoni ikisomwa: “Rosa Mistika ni marufuku shuleni.”

Ina maana kazi hiyo ilipata ahueni wakati wa chapisho, hata ikaanza kusomwa tena kwa mapana, zama utandawazi ulipoingia, awamu ya pili. Hiyo ilikuwa mwishoni mwa 1988.

Ina maana kuwa mwandishi huyo mkongwe alikuwa na utundu katika sanaa ya uandishi. Kimsingi, jamii zinapokuwa katika mawasiliano na uchumi, zinakuwa huru zaidi na kutupilia mbali mazingira ya kiimla yenye lengo la kuhakikisha utamaduni na maadili, vinalindwa.

Kuna wadadisi wa fasihi ya Afrika nchi za nje waliokusanya kazi zake na kuchagua baadhi ya mashairi yake kutoa kitabu wakilishi wa mtiririko wa hisia zake kama mshairi.

UMAHIRI KAZINI

Mwaka 2015 kuna andiko lililoitwa ‘Stray Truths’ yaani kweli zilizoko nje ya mstari, ambazo kuzitaja inahitaji utundu au uthubutu kwa kiwango fulani.

Ziko tungo kadhaa za Hayati Kezilahabi zilichapishwa katika miaka ya 1980 na ile ya 1990, kwa mfano ‘Karibu Ndani’ (1988); ‘Nagona’ (1990); na ‘Mzingile’ (1991).

Chapisho la baadhi ya mashairi yake kuwa kitabu wakilishi cha kazi zake lilitolewa na taasisi ya kutafsiri mashairi ya tamaduni tofauti, yenye wachangiaji kutoka nchi kadhaa za Ulaya kama Uingereza na Ufaransa.

Kuna maeneo ambako kazi za Hayati Kezilahabi zilihusishwa katika chapisho la kitabu mtandaoni. Hakuna uhakika kama mjadala ni wa hapa nchini au Bara Afrika, ambako inawezekana wanaofundisha fasihi na hasa lugha za Kiafrika, wanapata tabu kuziainisha.

Kazi moja ya fasihi na zile za lugha au fasihi kongwe kama Kiingereza, Kifaransa na Kiarabu, licha ya kuwa Kiarabu kimegawanyika vipande kadhaa.

Hata hivyo, unaweza kupata picha sahihi zaidi ya mjadala huo ukitoka katika fasihi ya Kiswahili ambayo ina mapana ya kutosha kuwa fasihi, kulinganisha na lugha nyingine za Kiafrika, mfano Kisomali, Kiganda, Kizulu, Kikikuyu ambacho anakiandikia mkongwe Profesa Ngugi wa Thiong’o.

Habari Kubwa