Rekodi yagunduliwa mti wa miaka 1,000

16Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Rekodi yagunduliwa mti wa miaka 1,000
  • Inafuata wa miaka 4,800
  • China, Marekani watafiti

MTI unaodumu hadi wastani wa miaka 1,000 na kushangaza watu, sasa wanasayansi wamegundua na kuibuka na majibu yake kulikoni.

Moja ya jamii ya mti mkongwe, ambao sasa una miaka 600. Inauwezo wa kuishi miaka 1,000. PICHA: MTANDAO

Ni utafiti ulioubua siri kuwapo aina ya miti yenye kemikali zinazodhibiti magonjwa na hata athari za ukame unakausha mimea, ikiwa ni tofuati na aina ya miti ambayo vinasaba vyake ni tatizo kuhimili hayo.

Siri ya uwezo wake kusimamia afya yake ni kwamba, ina kama mfumo wa vinasaba ambao havisumbuliwi na ukomo wa umri wa mmea.

Mtafiti Richard Dixon, kutoka Chuo Kikuu cha North Texas, Marekani anasema katika utafiti wao walijaribu kuusambaratisha kwa majaribio na wakagundua kuna namna ya kujihami kuendeleza uhai wake, jambo ambalo ni nadra kwa mimea mingine.

Mimea hiyo inaelezwa kuwa na baadhi ya tabia kama vile; inakua taratibu kuelekea ukubwa wake, ukiwa na rangi za njano na unapatikana zaidi katika ardhi ya China, ambako sasa unatunzwa kwa upekee kwa maana ya mimea adimu.

Watafiti walioshirikiana kutoka China na Marekani, waligundua baadhi ya miti hiyo walioitafiti ina umri kati ya miaka 15 na 667 katika uchambuzi wa kisayansi kuanzia mbegu zao, chembe hai na majani. Walikusanya kwa jumla miti ‘mizee’ na ‘vijana’ wakaona yote inatema kemikali za kujihami na kuwezesha kujipa uhai zaidi dhidi ya misukosuko ya kiafya na ukame.

Utafiti wa vinasaba inaonyesha kuna uhusiano kati ya kutofikia ukomo wa mabadiliko ya makuzi katika umri fulani, kama ilivyo kwa mimea mingine, wanyama, hata binadamu.

Dk. Dixon anasema wanachokigundua kwa sasa, kinafanana kwa karibu na miti mingine yenye umri mrefu, kwamba kinachowasimamia ni mazingira ya kiafya katika mtazamo wa namna hiyo.

"Ni matumaini yetu kwamba utafiti huu utawahamasisha wengine kuzama zaidi kuhusu picha muhimu kwa umri huo wa mti," anasema.

Bingwa mwingine mtaaluma, Mark Gush, akichangia kuhusu kazi hiyo ya kisayansi, anasema mti ulioishi mikaa mingi zaidi duniani unaitwa Bristlecone pine (Pinus longaeva) –ulikadiriwa kuwa na umri miaka 4,800.

"Uliondoa kupata chakula wakati wote, mwanga na maji bado uwezo wa kufikia umri kama huo unadhaniwa kuhusishwa na kasi (ndogo) ya ukuaji, inavyojilinda na mambo kadhaa yanayofuatia kama magonjwa, hali ya hewa na hatari nyiginezo,” anasema.

Uingereza, ni moja ya nchi ambayo katika sera zake, inaamini katika upandaji miti mchanganyiko kwa manufaa ya mazingira, hali ya hewa na mahitaji mengineyo inaitumia kuifuatilia kiyasansi.

Suala la msitu nchini Tanzania nako inapewa umuhimu mkubwa, kama kuwa na asasi, idara na taasisi kama Tafori, sheria na mahitaji mengi yanayoipa umuhimu mimea.

Pia kuna baadhi ya maeneo ambayo kuna hifadhi ya misitu, ikiwamo mimea na aina ya miti maaluma iliyotengwa na hata baadhi iko hatarini kutoweka, mfano hai ni katika Msitu wa Kisarawe, Mkoa wa Pwani.

•KWA MUJIBU WA JARIDA LA KISAYANSI

Habari Kubwa