Sababu Ronaldo kuifunga Atletico

18Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Sababu Ronaldo kuifunga Atletico

KILA wakati uliopita unaonekana kuwa mzuri zaidi kwa Cristiano Ronaldo. Anaweza kuwashtua wengi kwa kusahihisha makosa yaliyopita na kufanya maajabu.

Cristiano Ronaldo.

 

Ana umri wa miaka 34, lakini bado anaonyesha kuwa unaweza kumtegemea katika jambo muhimu.

Vichwa vyake viwili na bao la penalti vilimwezesha kufunga ‘hat-trick’ yake ya kwanza akiwa na klabu ya Juventus. Lakini jambo zuri zaidi ilitokea wakati Bianconeri hao walipokuwa wakihitaji mno msaada wake.

Walipoteza kwa Atletico 2-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa pale Madrid nchini Hispania. Lakini wakaweza kupindua matokeo dhidi ya timu hiyo ya kocha Diego Simeone.

Na mabao yake ndiyo yaliyoiwezesha Juventus kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ronaldo amefunga mabao 24 katika mechi 33 dhidi ya Atlético Madrid na ilikuwa ‘hat-trick’ yake ya nane kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Yeye ndiye mchezaji pekee aliyeifunga Atletico ‘hat-trick’ nne.

Hapa tunaangalia sababu tatu zinazomfanya Ronaldo awapatie zaidi Atletico Madrid...

 

1. Anajua kujipanga

Cristiano Ronaldo anaendelea kuwa mmojawapo wa wafungaji bora zaidi katika kizazi cha sasa cha wanasoka. Inashangaza sana kumwona anaweza kufanya kazi hiyo sasa wakati akiwa na umri wa miaka 34, wakati ambao miguu yake haina kasi na yenye nguvu kama ilivyokuwa mwanzo. Lakini Mreno huyo anabakia kuwa mmoja wa waviziaji bora duniani, lakini kwa sababu nzuri.

Mshindi huyo mara tano wa Ballon d'Or anajua kujipanga na ana akili ya kujua wapi sehemu sahihi ya kuvizia mpira, na ndicho alichowafanyia Atletico Madrid, kwa kuwa walishinda kumlinda. Kutoka kwenye nafasi ya mpira kumruhusu awe mahali pazuri, kwa wakati mzuri, kuweka mpira ndani ya wavu.

 

2. Nafasi nyingi

Kiukweli hii ni sababu rahisi zaidi. Unapomlisha mipira mchezaji bora duniani kama Cristiano Ronaldo, nafasi nyingi ataweza kufunga. Makosa ya Atletico Madrid ilikuwa ni kukaa nyuma na kulinda lango, kitu ambacho kiliwawia vigumu zaidi kwao.

Kwa mfano, Cristiano hakuwa kwenye kiwango chake katika mchezo wa kwanza, kwa sababu Juventus waliingia kwa nia ya kujilinda zaidi. Bianconeri hao hawakuwa wakitumia mipira yao ili kupata mipira ndani ya eneo la hatari la Atletico Madrid walikuwa na haraka ya kufunga. Hilo lilimfanya Ronaldo kuwa peke yake mbele na kukosa mtu wa kumlisha mipira.

Mambo yalikuwa tofauti katika mchezo wa pili, kwa kuwa Juventus walikuwa wanahitaji ushindi ili waweze kusonga mbele. Kwa hiyo, Ronaldo alifunga katika krosi mbili alizozipata na kuisaidia timu yake kupindua matokeo.

 

3. Hamasa

Ni dhahiri, Atletico Madrid ni waathirika wa zamani wa  Ronaldo. Baada ya bao la kwanza walionekana kurudi nyuma na hakukuwa na mpango wowote wa kusukumiza mashambulizi mbele.

Na jinsi mchezo ulivyokuwa unakwenda, wakajikuta wanashindwa kuhimili presha ya Juventus na kujikuta wakifungwa kirahisi.

Wakati huo huo, Cristiano amezoea shinikizo. Amefunga ‘hat-trick’ nyingi huku nyuma na kuweza kupindua matokeo. Aliwahi kufanya hivyo dhidi ya Wolfsburg wakati akiwa Juventus. Alikuwa na njaa na aliamua kufanya kile kilichowezekana kuisaidia timu yake.

Ingawa Juventus ilipoteza mabao licha ya kufunga mabao matatu Santiago Bernabeu, ni dhahiri kwamba kuwasili kwa Cristiano kuliongeza nafasi yao, na kuwafanya kuwa na uhakika zaidi wa kupata ushindi na kurudi tena mchezoni kama ilivyotokea kwenye mchezo huo na wakafuzu robo fainali.

Habari Kubwa