Sanduku la nyukilia

23Jan 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Sanduku la nyukilia
  • *Trump akataa kumkabidhi Joe Biden
  • *Changamoto iliyoibua hofu Marekani

MOJA ya tukio la kuvutia, lakini halifanyiki hadharani ni lile la makabidhiano ya masanduku ya nyuklia kati ya Rais wa Marekani anayeondoka na Rais anayeingia madarakani.

Katika miongo sita wakati wa kuapishwa kwa rais mpya kila Januari 20 baada ya uchaguzi, hafla inayofichwa na shamrashamra zinazoendelea, wanajeshi wawili waliovalia sare zao za kijeshi wamekuwa wamesimama pembeni wakati wa uapishwaji.

Askari mmoja ambaye ni mpambe wa rais anayeondoka madarakani, hubeba sanduku zito ambalo humkabidhi askari mwingine ambaye atakuwa akiandamana na rais mpya.

Sanduku hilo ndilo inaloitwa ‘Black Box’ au 'Sanduku la nyuklia', ambalo limetengenezwa kwa chuma na kila mahali anapokwenda Rais wa Marekani, uandamana nalo ili kumpatia nafasi kuamuru kurusha bomu la kinyuklia akiwa nje ya ikulu ya White House.

Tangu sanduku hilo lilipoanza kutumika wakati wa utawala wa John F Kennedy, ubebaji wa sanduku hilo umekuwa kitu muhimu, licha ya kutokuwa miongoni mwa vitu vya kipekee katika sherehe hiyo ya kuapishwa Rais.

Hata hivyo, mwaka huu kwa mara ya kwanza njia ya kukabidhi sanduku hilo kutoka mkono mmoja hadi mwingine, haikufanyika tangu kubuniwa kwake zaidi ya karne moja.

Makabidhiano hayo hayakufanyika kutokana na kiongozi anayeondoka Donald Trump, kukataa kuhudhuria hafla ya kumwapisha Rais mpya Joe Biden.

Kulingana na itifaki, Trump alipaswa kuwa na sanduku hilo la nyuklia hadi saa sita.

Lakini ilipofikia muda huo, Trump tayari alikuwa umbali wa kilomita 1,500, kusini mwa Florida na kumuacha Rais Biden peke yake.

Hata hivyo, kuna masunduku mengine kama hayo ambayo yamewekwa tayari kutumika katika makabidhiano endapo kiongozi anayepaswa kukabidhi hayupo.

Swali muhimu ni kwamba makabidhiana ya sanduku hilo la kinyuklia ilifanyika vipi iwapo marais hao walikuwa maeneo tofauti?

Suluhu isiyo ya kawaida

Wasiwasi wa jinsi gani sanduku hilo la nyuklia lingekabidhiwa kwa utawala wa Biden, ulijibiwa na Idara ya Ulinzi nchini Marekani, iliyopo Pentagon kuwa ilikuwa na mpango huo siku ya kuapishwa kwa rais mpya, lakini ikakataa kutoa maelezo.

Hata hivyo, wataalamu kadhaa na wasomi wameeleza njia kadhaa ambazo zinaweza kutumika iwapo hali hiyo isiyo ya kawaida itaikumba Marekani.

Stephen Schwartz, amesema tofauti na fikra za wengi, kuna masunduku matatu ya aina hiyo.

Moja ni lile linaloandamana na rais, lakini kuna masanduku mengine mawili ambayo ya dharura yanakuwa kwa makamu wa rais au mtu aliyepewa mamlaka ili kuzuia tukio lolote kama viongozi hao wa juu wamefariki.

Schwartz amesema Pentagon inaweza kutumia mojawapo ya masunduku yake, au kuandaa jipya ili kumkabidhi Biden baada ya kuapishwa. GES

Wakati huo sanduku hilo jipya linakabidhiwa kwa Biden, lile ambalo alikabidhiwa Trump ambalo hakukabidhi linakuwa limeisha kazi yake.

Kutokana na hatua hiyo, kadi zake zinazotoa nambari za siri za sanduku hilo la nyuklia huzimwa.

"Iwapo ofisa anayebeba sanduku hilo aliaandamana na Trump, katika ndege ya Airforce One kuelekea Florida, msaidizi huyo aliondoka mahali alipo Trump, ilipofikia muda wa sita kamili na kurudi Washington na sanduku hilo, ameeleza Schwartz wakati akiiambia CNN.

SANDUKU LA SIRI

Suala la sanduku hilo limezua maswali mengi na jinsi matumizi yake yamewavutia mamilioni ya watu kwa miaka mingi.

Kile ambacho watu hawakijui ni kwamba namba za siri na funguo zake ambazo zinamruhusu kiongozi wa Taifa hilo kuwa na uwezo wa kutoa maagizo ya kutekeleza shambulio hazipo ndani ya sanduku hilo.

Funguo hizo ambazo zina uwezo wa kutekeleza shambulio la kinyuklia, huwa ni kadi ndogo ya plastiki ambayo rais aliye madarakani hubeba mfukoni.

Kadi hiyo hujulikana kama ''Code of Gold au Cookie''.

Rais hutakiwa kuikata mara mbili ili kuthibitisha utambulisho wake pale anapowasiliana na kitengo cha vita katika Pentagon, ili kuruhusu shambulio.

Mapema siku ya kuapishwa kwa rais mpya na makamu wake, hupokea maagizo ya jinsi ya kutumia sanduku hilo na rais anayechukua mamlaka hupatiwa kadi hiyo.

Kulingana na jarida la sayansi ya atomiki, Pentagon huzima kadi ya rais anayeondoka madarakani saa sita mchana baada ya kuapishwa kwa rais mpya, huku kadi ya kiongozi ikiwashwa.

Hivyo basi, saa 6:01 ya Januari 20, iwapo Trump angetaka kutekeleza shambulio la kinyuklia, asingeweza kufanya hivyo, licha ya kumiliki sanduku hilo na Biden naye asingeweza kufanya hivyo saa 5: 59 asubuhi.

Hofu iliibuka kuwa Trump angetekeleza shambulio la nyuklia kabla ya kuondoka kufuatia ghasia za uvamizi wa jengo la bunge la Capitol Hill mapema mwezi huu.

Wakati huo, kiongozi wa bunge hilo, Nancy Pelosi, aliwasiliana na idara ya ulinzi na kuwataka kutofuata maagizo ya Trump iwapo angetaka kutekeleza shambulio hilo kabla ya kuondoka katika Ikulu ya White House.

SANDUKU LILIVYO

Bruce Blair, ambaye alikuwa askari mstaafu wa kutekeleza shambulio la nyuklia nchini Marekani, alielezea BBC, kwamba tofauti na jinsi watu wanavyoamini, sanduku hilo la nyuklia halina kitufe au namba za siri zinazomwezesha rais kutekeleza shambulio la nyuklia moja kwa moja.

Amesema badala yake itifaki za shambulio hilo ni sharti awasiliane na washauri wa ngazi za juu.

"Katika sanduku hilo pia kuna mchoro wa mpango wa vita, malengo yake pamoja na idadi ya watakaofariki bila kusahau silaha zilizopo. ''Hivyo ni rahisi kuelewa hali ilivyo katika sekunde chache,'' amesema Blair.

Ndani ya sanduku hilo sio namba za siri pekee zinahifadhiwa, pia kuna vitabu viwili ambavyo ni muhimu.

Kimoja kina maelezo ya kina kuhusu aina ya shambulio hilo la nyuklia ambalo linaweza kutekelezwa, orodha nyingine ya maeneo salama kwa rais.

Muda wote sanduku hilo huonekana na antena iliojitokeza ambayo hutumika kuimarisha mawasiliano ya moja kwa moja na idara ya ulinzi ya Pentagon.

KWA MSAADA WA MTANDAO

Habari Kubwa