Siasa za barakoa, kukubalika ziko hivi…

29Jul 2021
Michael Eneza
Dar es Salaam
Nipashe
Siasa za barakoa, kukubalika ziko hivi…

SUALA la kuvaa barakoa bado halijaanza kutambuliwa katika tafsiri ya lazima kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na kwingineko nchini.

Mhamasishaji Waziri Dk. Dorothy Gwajima, akiwa katika vazi rasmi. PICHA: MTANDAO.

Wakati kuna tafsiri hiyo, jana hatua ya mapambano ilifika mbali kwa kutolewa chanjo rasmi, ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika maeneo hayo, baadhi ya wakazi wanaanza tena kuchukua umakini tangu linaloitwa wimbi la tatu kuanza kwa kasi.

Kunatajwa muundo tofauti na vilivyotangulia, ingawa haieleweki sana. Kwa jumla, kumekuwapo mawimbi mawili, ikianzia mwezi Machi, halafu mwanzoni mwa mwaka huu.

Nchi za nje kuna wimbi la nne. La kwanza likiwa la mwishoni mwa mwaka 2019 huko Wuhan, China halafu likasambaa Ulaya, kasha Marekani Kakazini na Kusini, hadi Bara Asia, kulikowaka moto.

Katika ujumla, kumekuwapo mawimbi tofauti na historia za kuenea corona kati ya nchi moja na nyingine. Ndio namna imesikika nchini jana Rais Samia Suluhu katika uzinduzi, akitaja mikoa kadhaa kama Dar es Salaam, Kagera na Kilimanjaro, ilivyofikiwa.

Wimbi la kwanza limeitwa Covid-19 na ugonjwa ukifahamika kutokana na virusi vya corona, vikimaanisha, “kirusi mviringo chenye sura ya kupatwa jua, ambako seli za ncha ya kirusi hicho ni ‘mkuki’ unaolenga kokote mwilini mwa binadamu.|

Dawa na chanjo zilizotengenezwa zimeulenga muundo wa kirusi hicho; ‘u-protini’ wake na jinsi ya kuulemaza. Ni ‘mkuki’ wa kudhibiti ncha yake kuwa butu.

Rais Samia alipoingia madarakani, tayari wimbi la tatu duniani lilishaanza. Mawimbi hayo yana kawaida yanapogundulika eneo fulani, haichukua muda kufikia kwingine, hata unazuka ubishi kirusi hicho kilianzia wapi.

Septemba mwaka jana, Uingereza ilipambana nayo ikiita ni ‘kirusi cha Afrika Kusini’ huku wanaotajwa wakikanusha vikali.

Kirusi cha pili kilianza na mazingira tatanishi zaidi, kati ya Marekani na Uingereza, lakini kama ilivyokuwa cha Afrika Kusini au na Uingereza, haikuwa na nguvu sana, licha ya kutofautiana katika maeneo kadhaa na cha awali kutoka Wuhan, China.

Serikali ya China imekanusha uvumi na tafsiri, ila inabaki na kigugumizi kueleza amna kirusi cha mnyama kama popo, kilivyobadilika kuwa cha binadamu ikikiwa na kasi kubwa ya kuambukiza.

Hadi mwanzo wa mwezi huu, inakadiriwa takriban watu 400,000 wameshakufa nchini humo. Pia licha ya kuwa virusi vya awali na vya sasa kuleta maafa makubwa duniani, Afrika bado maafa yapo kiwango cha chini zaidi.

Maeneo mengi duniani, mtu kutoka nje ni kujiweka karibu na madhara ya corona na mara nyingine virusi vinapenya mianya kuzunguka barakoa, mathalani juu ya pua.

Ndiyo sababu za msingi za ‘lockdown’ (kufungia watu ndani wasitoke nje ila kwa dharura maalum) ambazo sasa kuna maeneo wanabishia au kuzikataa, barakoa, pia chanjo katika mazingira tofauti.

Wakati Rais Samia, jana alitoa vigezo kadhaa kukubali kuchanja dhidi ya madhara virusi corona, naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, alifafanua nafasi na umuhimu wa dawa hizo, akitumia utaalamu wake kwa kina.

Yako majadiliano yaliyofika katika magazeti na mitandao ya kijamii kuhusu njama za kutengeneza barakoa na hata chanjo, na baadhi walitoa hoja za kutengenezwa virusi vya Covid-19, kwamba ni
mkakati wa kupunguza watu duniani.

Hata hivyo, ni kama darasa limeanza kuwa bayana, nchini Marekani, sehemu kubwa ya maambukizi mapya ni kwa waliokwepa chanjo, kwa visingizio kadhaa.

Tofauti kuu iliyopo sasa, ni chanjo zilizoandaliwa kirusi cha awali cha Covid-19, zimepungua uwezo kuzuia badilika cha tatu, ambacho kiligunduliwa nchini India kwa jina Delta (herufi D).

Israel inasema, chanjo yenye nguvu zaidi ya ‘Pfizer/BioNTech’ ya kampuni za Marekani na Ujerumani, ina uwezo wa asilimia 40 kuzuia maambukizi ya ‘Delta.’

USHUHUDA WA DK. MSHANA

Kuna ushuhuda wa Dk. Rogate Mshana, Mkurugenzi Mstaafu wa Fedha katika makao makuu ya Fungamano la Makanisa ya Kilutheri, Geneva amepona hospitalini KCMC, akikiri kutovaa barakoa kulimponza.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Jude Ruwaichi, mnamo mwezi Aprili, alitoa angalizo la kuwapo tatizo la kutovaa, licha ya kutolewa wito.