Tanzania ya JPM ilivyofanikiwa kuiona hatua Uchumi wa Kati

03Jul 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Tanzania ya JPM ilivyofanikiwa kuiona hatua Uchumi wa Kati

JUZI Tanzania ilitangazwa rasmi kuwa katika Uchumi wa Kati. Ni miezi mitano kabla ya kumaliza awamu yake ya kwanza ya uongozi, Rais Dk. John Magufuli na siku moja baada ya kurejesha fomu ya chama chake kuomba apitishwe kuwania tena, azma aliyotangaza kuinuia, imetimia.

Hiyo ni kupigania Tanzania kuingia katika orodha ya uchumi wa kati, mwenyewe akitabasamu kupokea hadhi hiyo kutoka ya Benki ya Dunia, kwamba ni ushindi wa Watanzania wote.

Utaratibu wa Benki ya Dunia, hutangaza mabadiliko ya hadhi hiyo kila Julai Mosi wa Mwaka na tovuti yake inataja nchi zingine zilizopanda ya hadhi kutoka kundi la nchi masikini na kuingia uchumi wa kati ni Nepal na Benin.

Kimsingi, Benki ya Dunia hutambua hadhi ya nchi kiuchumi kwa kuzigawa katika makundi: Ngazi ya juu; ngazi ya kati iliyoko katika kundi la chini na juu; na nchi zenye uchumi wa chini, maarufu kama nchi masikini.

Namna inavyopatikana kiwango cha uchumi wa nchi, ni kupitia hisabati ya kugawanya pato la taifa kwa idadi ya wananchi wa waliopo na kupata wastani wa pato la mtu mmoja mmoja kitaifa.

Wastani uliotengwa kwa mataifa ya uchumi wa kati kwa kiwango cha chini ambako Tanzania imo, ni yenye wastani wa pato la taifa kwa mtu mmoja mmoja, kati ya Dola za Marekani 1006 (Sh. 2,330,902) na 3,955 (Sh.9,163,735).

Pia, pato la taifa la kati katika ngazi ya juu, ni kwa kwenye wastani za Dola za Marekani 3,956(Sh.9, 166,052) na 12,235(Sh. 28,248,495); na nchi zenye chini ya Dola za Marekani 1006, inaangukia katika kundi la nchi za uchumi wa chini.

Benki ya Dunia imeitaja Tanzania kufika hatua hiyo ya mafanikio, baada ya kuwa na pato la taifa la wastani wa mtu mmoja Dola za Marekani 1080, sawa na Sh. 2,502,543.60.

VIGEZO VINGINE

Katika maelezo yake, Benki ya Dunia, imeorodhesha vigezo vingine vinavyotiwa maanani kama vile mfumuko wa bei, kiwango cha mabadilishano ya fedha za kigeni, pato la taifa na kasi ya ukuaji uchumi, kukiwepo mapitio ya kina kuhusu nyendo za nchi.

“Mapitio ya ki-nchi yamesaidia sana katika kufanya mapitio kwa mataifa ya Benin, Nauru na Tanzania,” inaeleza taarifa hiyo.

JEDWALI LA BENKI YA DUNIA

Uchunmi Kundi jipya Kundi la zamani Pato kwa mtu (Dola za Marekani) Julai 1, 2020 Pato kwa mtu (Dola za Marekani) Julai Julai 1, 2019.

Benin Uchumi Kati (chini) Uchumi chini 1,250 870

Indonesia Uchumi Kati (juu) Uchumi Kati (chini) 4,050 3,840

Mauritius Uchumi wa Juu Uchumi Kati (juu) 12,740 12,050

Nauru Uchumi wa Juu Uchumi Kati (juu) 14,230 11,240

Nepal Uchumi Kati (chini) Uchumi chini 1,090 960

Romania Uchumi wa Juu Uchumi Kati (juu) 12,630 11,290

Tanzania Uchumi Kati (chini) Uchumi chini 1,080 1,020

MCHAMBUZI

Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi, Deus Kibamba aliyehojiwa na shirika la habari la BBC, anafafanua benki hiyo hutathmini pato la taifa, mathalan jumla ya utajiri wa rasilimali na ule wa kifedha na kugawanya na idadi ya watu wa nchi.

Kibamba anasema hiyo ina tafsiri kwamba, taifa husika linaelekea kuimarika kiuchumi na ishara kwamba siasa za nchi zinaenda sambamba na ukuaji kasi ya ukuaji uchumi, sifa inayosaidia kuvutia uwekezaji mitajio ya kigeni nchini, hali inayochangia kuimarika uchumi.

Hata hivyo, Kibamba anakumbusha mafanikio hayo yana maana kwa Watanzania kwamba, ili wanufaike na hatua hiyo wanahitaji kuingeza juhudi za kuifanya kazi kwa mtu mmoja mmoja, ili kuboresha uchumi zaidi.

Benki ya Dunia inafafanua kuwa mataifa yenye kipato cha kati ndio yenye asilimia 75 ya idadi ya watu duniani, hali kadhalika asilimia 62.

Habari Kubwa