TECNO yazindua boda la spark 3

11Jun 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
TECNO yazindua boda la spark 3

Kampuni ya simu ya TECNO mobile imezindua promosheni ya boda la spark 3 ambapo ukinunua simu mpya ya TECNO SPARK 3 unapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwamo pikipiki.

Promosheni hiyo imeanza Mkoa wa Dar es salaam na kuenea mikoa mingine hapo baadae, ambapo mteja atakaenunua simu hiyo kwenye maduka maalumu ya TECNO yenye promosheni hiyo atapewa nafasi ya kuondoka na zawadi za papo kwa papo kama power bank yenye mAh 5000 na pamoja data cable.

TECNO Spark 3 ni simu ya kijanja yenye uwezo mkubwa wa kupiga picha pamoja na kufanya vitu mbali mbali mitandaoni imezinduliwa takribani mwezi mmoja ikiwa ndio simu inayofanya vizuri zaidi kwa upande wa simu janja za kipato cha kati.

TECNO SPARK 3 ina ubora wa kamera yenye megapixel 13, huku mtumiaji anapata nafasi ya kuifadhi vitu vyake kwenye GB 16 za memory ya ndani na muonekano wake ni wakijanja na ndio maana inafanya vizuri sokoni.

Mshindi wa pikipiki atapatikana mwisho wa mwezi wa sita kwa njia ya bahati nasibu itakayo chezeshwa moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii ya TECNO mobile hasa Instagram.

Habari Kubwa