Teknolojia kuhakikisha kahawa haitoweki siku zijazo?

27Jun 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Teknolojia kuhakikisha kahawa haitoweki siku zijazo?

Ongezeko la nyuzi joto 4C linatokana na hali ambayo utoaji wa gesi unaochangia ongezeko la joto duniani hadi mwaka 2100.

Utabiri huo ni moja ya utabiri unaohusiana na utoaji wa gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani uliofanywa na Jopo la Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC).

Dk. Tim Schilling, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Duniani, shirika linalofadhiliwa na wadau katika sekta ya kahawa duniani, anasema:
''Uzalishaji wa kahawa bora duniani bila shaka unakabiliwa na changamoto tele; kutoka kwa mabadiliko ya tabia nchi, magonjwa na wadudu, mahitaji mengine ya mashamba, upungufu wa wafanyakazi bila kusahau kuimarika kwa idadi ya wanywaji wa kahawa duniani kila mwaka''.

Katika baadhi ya maeneo ya uzalishaji wa kahawa, viwango vya joto vimeongezeka kiasi kwamba, tayari viwango vya ubora wa kahawa vimeanza kuathirika, anaongeza Dk. Schilling.

Mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea kuwaathiri wakulima wa kahawa nchini Ethiopia na Brazil huku wanasayansi wanatabiri kupungua kwa maeneo ambayo kahawa yenye ubora wa hali ya juu yaweza kukuzwa.

Mataifa kadhaa yanayozalisha kahawa yanaanza kushuhudia viwango vya juu sana vya kahawa. Dk. Baker, anaamini hili linatokana na kuharibiwa misitu kwa ajili ya kilimo.

Mataifa karibu yote ambayo uzalishaji wa kahawa unaongezeka kwa kasi sasa, inatokana na kuharibiwa kwa misitu kutoa nafasi kwa maeneo ya ukuzaji kahawa. Hiyo ni licha ya Brazil ambako kilimo cha kahawa kimeimarishwa kwa njia ya teknolojia,'' anasema mtafiti huyo.

Taasisi ya kahawa duniani imeanzisha harakati ya kuboresha uwezo wa kahawa aina ya Arabica kustahimili ongezeko la joto duniani na kuimarisha uwezo wake wa kuzalishwa kwa urahisi.

Hata hivyo, hili sio suala litakalowezekana kwa urahisi. Linaweza kuchukua kipindi kirefu.

Wanywaji wa kahawa huenda wakapata kahawa isiyo na ladha nzuri na bei yake kuwa juu, kwa sababu ongezeko la joto duniani linasababisha ardhi inayoweza kutumiwa kukuza kahawa kupungua, wanasema watafiti kutoka Kew Gardens, London.

Uzalishaji wa kahawa nchini Ethiopia, kitovu cha kahawa ya hali ya juu ya Arabica, pia taifa linaloongoza kwa uuzaji wa kahawa nje ya Afrika, huenda ukawa hatarini sana katika karne ijayo, hatua muhimu zisipochukuliwa, kwa mujibu wa ripoti, iliyochapishwa hivi karibuni

"Nchini Ethiopia na kwa kweli duniani kote, hatua zisipochukuliwa kahawa itapungua, na kuna uwezekano mkubwa ladha yake kuwa mbaya na kugharimu zaidi," Dk. Aaron Davis, mtafiti wa kahawa katika Kew na mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo, aliiambia BBC.
Kahawa itakwisha?

Unywaji wa kahawa unatarajiwa kuzidi uzalishaji kwa mwaka wa tatu, kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirikisho la Kimataifa la Kahawa (ICO). Kwa sasa, shehena ya kahawa iliyohifadhiwa kutoka miaka ya nyuma ya uzalishaji kwa wingi imechangia kudhibiti uhaba wa kahawa au kupanda kwa bei.

Hata hivyo, wauzaji nje wa kahawa wanavyoendelea kulazimika kutoa kahawa kwenye shehena waliyohifadhi miaka ya nyuma, hazina yao inaendelea kupungua, ICO wanasema. Bila kujali wasiwasi kutokana na mabadiliko ya tabia nchi siku za baadaye, kulikuwapo na wasiwasi awali kutokana na mabadiliko ya tabia nchi mwaka huu nchini Brazil na Vietnam, nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa kahawa duniani.

Hata hivyo, hofu hiyo imepungua na bado kuna wasiwasi wa kutokea kwa mabadiliko ya hali ya hewa yasiyotarajiwa miezi kadhaa ijayo kuweza kusababisha kupungua kwa muda buni za kahawa.

Ni hali ya kipindi kirefu cha baadaye inayowatia wasiwasi zaidi wakulima na wanywaji wa kahawa kwa pamoja.

Katika baadhi ya maeneo ya uzalishaji wa kahawa, viwango vya joto vimeongezeka kiasi kwamba, tayari viwango vya ubora wa kahawa vimeanza kuathirika, anaongeza Dk. Schilling.

“Kutokana na hayo yote, bei ya kahawa itapanda,'' aliongezea.

Maeneo yanayokuzwa kahawa nchini Ethiopia huenda yakapungua hadi asilimia 60 kutokana na ongezeko la joto la nyuzi joto 4C linalotarajiwa kufikia mwisho wa karne hii, utafiti wa Kew Gardens na washirika wake Ethiopia unatabiri.

"Mtazamo wa kutojali na kutochukua hatua, unaweza kuwa na madhara makubwa sana kwa sekta ya kahawa Ethiopia kwa muda mrefu," anasema Justin Moat kutoka Kew, mwandishi mwingine wa ripoti hiyo.

Watafiti wa Kew wanasisitiza kwamba, endapo hatua zitachukuliwa, hali hii inaweza kuepukika. Kuhamishwa kwa maeneo ya ukuzaji wa kahawa, pamoja na kuhifadhiwa kwa misitu na kupandwa kwa miti, vinaweza kuchangia ongezeko tena la maeneo ambayo yanaweza kufaa kukuza kahawa nchini Ethiopia.

Kuna uwezekano wa kukabiliana na vitu vinavyoathiri upandaji wa kahawa duniani, na hata tukaimarisha maradufu uzalishaji kahawa kwa zaidi ya mara nne na nusu badala ya kuendelea na hali ilivyo sasa,'' anasema Dk. Davis.

Kahawa ni kitega uchumi kwa takribani watu milioni 15 nchini Ethiopia. Hii ni asilimia 16 ya raia wote.

Wakulima wa maeneo ya mashariki ya nchi hiyo, ambayo mabadiliko ya tabia nchi tayari yanaathiri uzalishaji, wametatizika miaka ya karibuni, na wengi kwa sasa wanasema mavuno yameshuka kutokana na ukame wa muda mrefu.

Jamal Kassim, Mkulima wa kahawa Ethiopia, ameshuhudia upungufu mkubwa wa mazao yake tangu aipande miaka kumi iliyopita.

“Miti yangu ilizaa matunda mengi sana katika miaka ya kwanza, lakini sasa haizai tena. Nashindwa kukidhi mahitaji ya jamii yangu,'' anasema.

Ethiopia haiko pekee yake katika hali hii ya kupungua kwa mazao yake ya kahawa. Utafiti wa hivi punde zaidi wa vuguvugu la mashirika yasiyo ya kiserikali ya tabia nchi yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa (IPCC) unathibitisha kuwa Brazil inakumbwa na hali hiyo hiyo.

Kwa takribani miaka mitatu sasa, tumepokea kiwango cha chini cha mvua kuliko ilivyotarajiwa mazao yetu yameathirika sana.

Kupanda kwa kiwango cha joto kwa nyuzi joto 3C kumesababisha kuongezeka kwa kiwango cha mvua kwa asilimia 15 haswa katika maeneo yanayokuzwa kahawa kwa kiwango cha juu mno ya Minas Gerais na Sao Paolo. Hali hii inaweza kusababisha kupungua kwa eneo zima linalokuzwa kahawa kutoka asilimia 70-75 hadi 20-25

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, maeneo yanayotambuliwa kwa ukuzaji wa kahawa nchini Brazil, imeshuhudia ukame mbaya zaidi kuwahi kuikumba katika kipindi cha zaidi ya karne moja iliyopita. Ukuzaji wa kahawa katika jimbo la Minas Gerais ambayo ni kitovu cha kilimo hicho mapato yamedidimia kwa asilimia 20 kinyume na mwaka wa 2013.

Uzalishaji wa kahawa ya hali ya juu ya Arabica ulishuka kipindi cha mwaka mmoja kati ya Juni 2014 na Juni 2015. Kiangazi pamoja na joto kali katika jimbo la Espirito Santo katika kipindi cha miaka miwili tangu wakati huo, pia vimechangia kushuka kwa mavuno ya kahawa isiyo ya ladha tamu zaidi ya Robusta.

Na hata sasa, kote katika eneo hilo, mabwawa ya maji yanayotumiwa na wakulima kupata maji ya kunyunyizia mashamba yao hayana maji.

Serikali ilidhibiti unyunyiziaji mashamba maji katika miji kadha wakati wa ukame mbaya. Ujenzi wa mabwawa mengine ya kuhakikisha maji ya kutosha yanahifadhiwa wakati wa mvua unaendelea.

“Kwa miaka minne sasa, hatujapata mvua ya kutosha na mazao yetu yameathirika sana," anasema Inacio Brioschi mkulima wa kahawa kutoka eneo la Espirito Santo Brioschi ilipoteza nusu ya uzalishaji wake wa kahawa mwaka 2016 na inatarajia uzalishaji kuwa asilimia 60 chini ya kiwango cha kadiri mwaka huu.

Ukame wa mara moja hauwezi kushirikishwa na tabia nchi anasisitiza, Dk. Peter Baker, wa shirika la kahawa na mazingira linaloshirikiana na sekta ya kahawa. Hata hivyo tofauti kubwa ya viwango vya joto na mvua vinaathiri mimea na vilevile sekta hiyo ya kahawa.

Kwa hakika sio tu kuwa kiwango cha joto kinapanda ghafla bali ni mkusanyiko wa mabadiliko haya ya mara kwa mara ndio yanayodhuru soko la kahawa,'' anasema Daktari Baker.

Utafiti wa hali ya anga unahakiki mtazamo huo kuwa kuimarika kwa joto na mabadiliko ya tabianchi kwa mujibu wa Richard betts mkuu wa utafiti wa hali ya anga Uingereza.

Ukame pamoja na kuongezeka kwa viwango vya joto vina maana kwamba kwa jumla hali ya anga ina athari zaidi, anasema.

Huku kiwango cha joto kikiendelea kuongezeka duniani ni haki kusema kuwa, ukame unapotokea madhara yake huwa makali zaidi hivyo mashamba yanakauka sana,'' anasema Bett.

Uzalishaji wa kahawa Ethiopia, kitovu cha kahawa ya hali ya juu ya Arabica, pia taifa linaloongoza kwa uuzaji nje wa kahawa Afrika, huenda ukawa hatarini sana katika karne ijayo, hatua zisipochukuliwa, kwa mujibu wa ripoti, iliyochapishwa hivi klaribuni.

Habari Kubwa