Tembo afanyiwa upasuaji kwenye pembe Colombia

14Nov 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Tembo afanyiwa upasuaji kwenye pembe Colombia

HIFADHI moja wa wanyama nchini Colombia, imemfanyia upasuaji tembo mmoja kwa pembe yake iliyokuwa imepasuka.

Tembo huyo mwenye uzito wa tani tano alipatikana katika shamba moja linalomilikiwa na walanguzi wa dawa za kulevya.

Watu 30 walishiriki kwa njia moja au nyingine wakati mnyama huyo ajulikanaye kwa jina la Tantor alipokuwa akidungwa dawa ya kumpa usingizi.

Zaidi ya watu 100 walichanga pesa kwa ajili ya upasuaji huo uliogharimu zaidi ya dola za Marekani 8,500.

Upasuaji huo ulipaswa kufanyika miaka miwili iliyopita wakati Tantor alipojeruhi pembe yake, lakini shughuli hiyo ilichelewa baada ya kukosekana kwa vifaa vinavyostahili vya kumfanyia upasuaji.

Ilibidi vifaa maalumu vitengenezwe kwa ajili ya upasuaji huo.

Tantor alipelekwa katika hifadhi ya Barranquilla Aprili mwaka 1991 baada ya kuokolewa na shirika la kupambana na dawa za kulevya nchini Colombia, kutoka kwenye shamba moja linalokuwa likimilikiwa na walanguzi wa dawa za kulevya.

Anaaminiwa kuwa na umri wa takribani miaka 50.

BBC