TGNP yaanika magumu ya corona na familia kupitia angalizo la SADC

25Nov 2021
Yasmine Protace
Dar es Salaam
Nipashe
TGNP yaanika magumu ya corona na familia kupitia angalizo la SADC

WASTANI miaka 13 iliyopita, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ilibuni kipimo cha kufuatilia maendeleo ya kijinsia ndani ya nchi wanachama, ikiwa na viashiria 100; kipimo kiliitwa Barometa ya Kijinsia.

Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia, Hance Obote, akizungumza jambo katika mkutano wa kijinsia. PICHA: MTANDAO.

Hapo kuna maeneo saba yanayosimamia viashiria hivyo, ikijumuisha: Uhusiano wa kimapenzi na afya; afya ya vijana; utoaji mimba salama; UKIMWI; matendo hatari; na mambo ya kimapenzi

Mwaka huu, nchi 16 wanachama wa SADC zimekutana kujadili suala hilo, ikiwamo halisi ya chanjo ilivyo. Kimsingi, barometa hiyo inaonyesha ujumbe mzito kwamba sauti ya chaguo haishii katika uadilifu na mwili pekee, bali na haki za wanawake katika jamii.

Hapo kuna mjadala uliozama hata katika afya ya uzazi, ngono salama, afya ya uzazi kijinsia na haki za vijana, utoaji mimba salama, maambukizi ya VVU, ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni na janga jipya la Uviko 19.

Suala hilo la liliangaziwa kwenye barometa hiyo na takwimu zinaonyesha huenda itachukua mwaka mmoja au miwili zaidi.

Katika kipindi cha watu kuamriwa kujifungia maarufu ‘lockdown’ dhidi ya maradhi hayo katika baadhi ya nchi wanachama, kunatajwa kutawaliwa na utata wa takwimu halisi ya namna Uviko 10 umetawala, hadi kufikia mwaka huu, kwani hakuna takwimu sahihi za wagonjwa kati ya wanawake na wanaume, hali kadhalika vifo vyao.

Waziri wa Afya nchini Malawi, Dk. Patricia Kakiati, anasema hakuna suluhisho sahihi lililofikiwa katika kuweka sawa picha halisi na ya kitakwimu katika uwasilishaji yanayohusu eneo hilo kijinsia, akielekeza jicho mahsusi katika chanjo.

JICHO LA GEMSAT

Mwenyekiti wa Jinsia Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Mtandao wa Tanzania (GEMSAT), Dominica Haule, katika uzinduzi wa ripoti ya barometa iliyozinduliwa na TGNP Mtandao, anatamka Uviko 19 imeingia nchini mara ya kwanza mwaka jana.

"Kinamama ni watafutaji. Kipindi cha mwaka jana kulipotangazwa corona na watu tukatakiwa kutulia maeneo yetu. Kwa kweli, kinamama wengi wameharibikiwa biashara zao," anaeleza.

Anafafanua kwamba walifanikiwa kutembelea Dar es Salaam eneo la Slipway, pia Bagamoyo amezuru na kuzungumza na jinsia zote, kinamama na kinababa, ambako kuna kampuni zimekabiliwa ‘lockdown; hata wafanyakazi badala ya kupewa mishahara, walipewa posho wakiwa nyumbani.

Dominica anasimulia ziara nyingine katika soko la samaki Feri, Dar es Salaam, ambako amewakuta wakaanga samaki wasio na barakoa na alipowahoji kulikoni hawakuvaa barakoa, alijibiwa kwamba hawakuwa na uwezo wa kununua nyenzo hizo kwa saa nne, hivyo wakaamua kutovaa.

Kuhusu chanjo, ana ushauri watu wajitokeze kupata huduma hiyo na sio kuishia kusikiliza maneno ya watu, ikiendana na elimu kwa umma katika nanma ya kukabiliana na maradhi corona

WANAHARAKATI JINSIA

Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia, Hance Obote, kutoka Kituo Cha Taarifa na Maarifa Saranga, anasema mwaka Jana matukio ya ukatili yalifanywa kwa watoto wa kike  waliokaa ‘lock down’ kutoka na maradhi Uviko -19 wakarudi shule na ujauzito, pia baadhi ya familia ziliitumia hayo mazingira kutesa watoto wao.

Anasema, ukatili wa kiuchumi ulijitokeza kutokana na biashara nyingi kufungwa na wenye mali, huku wafanyakazi wakiangukia ugumu wa maisha ya kila siku, hata kukajitokeza athari kwa watoto.

Kuna baadhi ya mashirika yamepunguza wafanyakazi, huku wanafamilia wakiwamo watoto, waliokosa mahitaji ya msingi kutoka kwa wazazi walioathirika kibiashara.

Obote anasema, hali ya watoto kutoenda shule  zilipofungwa, ziliwanyima ulinzi dhidi ya ukatoli hasa wa kingono.

Joyce Mkina kutoka Idara ya Nguvu ya Pamoja (TAPO) ya TGNP Mtandao, anfafanua lengo la mkutano wa mwaka 2008 ulijumuisha nchi 26 za SADC kuisaini  makubaliano ya  itifaki ya kijinsia na kinachofanyika sasa ni tathmini  ya 13, ambayo ni ya mwisho kuhusu uzazi kwa wanawake .

Habari Kubwa