UN: Asilimia 9 ya watu Israeli ni wavuta bangi

16Mar 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
UN: Asilimia 9 ya watu Israeli ni wavuta bangi

ISRAELI ni kati ya nchi zilizo juu katika kufanya utafiti unaohusiana na matumizi ya bangi, huku wachambuzi wakisema kwamba hakuna hatua kubwa iliyochukuliwa katika kukabiliana na matumizi yake.

Ingawaje kujihususha na bangi kwa namna yoyote ile unakuwa mtihani mkubwa wa kisheria kwa maana ya kitendo batili, lakini sheria huwa msumeno zaidi kwa wanaorudia kosa.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) inayoshugulika na dawa za kulevya na uhalifu, takriban asilimia tisa ya raia wa Israeli ni watumiaji wa dawa za kulevya aina ya bangi.

Hata hivyo, wataalamu hao wanabashiri kwamba, huenda kiwango hicho kikawa juu zaidi, kwani kuna watu ambao hawakufikiwa. Huo ni kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2012.

Hivi sasa kuna kamati maalumu iliyoundwa kufuatilia tatizo hilo na hasa katika bara Marekani na Ulaya.

"Kwa upande mmoja, tunajifungulia wenyewe kwa maisha ya baadaye na kwa upande wa pili tunaelewa kwamba hata iliyopo na tunajaribu kusawazisha mambo," anasema Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu

Katika hilo, Waziri wa Sheria, Ayelet Shaked, anatamka: "Israel haiwezi ikafumba macho katika mabadiliko yanayofanyika duniani kuhusiana na matumizi ya bangi na athari zake.”

Aidha, Waziri wa Usalama Gilad Erdan, anaongeza kuwa, nyendo hiyo ilikuwa muhimu katika kutekeleza sera mpya,ya kuboresha elimu na kupambana na uhalifu.

Sheria za Israeli zinamlenga mtu anayekamatwa kwa mara ya kwanza na akikiri kutumia bangi, atataozwa faini ya Dola za Marekani 270 ambayo ni sawa na Sh. 594,000.

Mtu huyo akinaswa kwa mara ya pili, faini hiyo inakuwa mara mbili ya kiwango cha kwanza, ambayo sasa inakuwa Sh. milioni 1.19.
Pia, inapokuwa kwa mara ya tatu, faini ya mara ya pili inakuwa mara mbili ya hatua ya pili, ambayo inaongeza hadi kuwa Sh. milioni 2.376 na inapotokea mtu anapokutwa anavuta bangi kwa mara ya nne, sasa anakabiliwa na kesi ya jinai katika vyombo vya sheria.

Kuna wakati huko nyuma, kilinaswa kiwanda cha siri cha kuandaa bangi kwa mfano wa sigara, ambacho kilikuwa kinaandaliwa na kuna wataalamu wa siri wanaofanya kazi hiyo, kama ilivyo katika kiwanda cha sigara.

Ni kiwanda kilchokuwepo mafichoni katika milima iliyoko Kaskazini mwa nchi hiyo, kilikutwa kiwanda cha siri cha kuandaa bangi na akakutwa mtaaluma mwanamke.

L Makala hii imeandaliwa kwa mujibu wa taarifa za mtandao.

Habari Kubwa