UN yawajadili vijana na uchumi wa tabianchi

07Dec 2018
Na Mwandishi Wetu
Poland
Nipashe
UN yawajadili vijana na uchumi wa tabianchi
  • Wajinoa kwa makuu 3 mwakani

ARI, mabadiliko ya kiuchumi na Imeelezwa wiki hii kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea mjini Katowice , Poland, kutafuta mwongozo wa kimataifa kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, akihutubia mkutano unaoendelea mjini Katowice, Poland.
Pembeni, Luis Alfonso de Alba na mwakilishi wake maalumu wa mkutano wa mwakani.
Wa Kwanza, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu, Robert Orr.
PICHA: UMOJA WA MATAIFA.

Akizungumza na waandishi wa habari na wadau kwenye mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amewasilisha maoni yake kuhusu mkutano huo wa mwakani.

Anasema; “Mkutano huo utajikita katika kuhakikisha mambo muhimu matatu: Kuamsha ari ya kweli, kuchukua hatua halisi za mabadiliko katika uchumi na ushirikishwaji wa raia na uhamasishaji wa vijana.”

Ni mkutano uliopangwa kufanyika Septemba 23, mwaka ujao kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, kuchagiza msaada na uungwaji mkono wa hatua za mabadiliko ya tabianchi katika ngazi ya kisiasa amesema Guterres na kuongeza kuwa

“Tutafanya mkutano huo wakati wa wiki ya vikao vya ngazi ya juu vya Baraza Kuu, ili kuhakikisha tuna wakuu wengi wa nchi na viongozi wa serikali watakaohudhuria kadri iwezekanavyo,” anasema.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa kawaida linahudhuriwa na takribani viongozi na wakuu wa nchi 130 wanaojadili na kuweka ajenda za kimataifa kwa mwaka huo. Guterres anawaeleza washiriki kwamba: “Matokeo ya mkutano huo yatakuwa matokeo yenu. “
Amezialika serikali zote , sekta za biashara, taasisi za fedha, sekta za umma na binafsi, pia asasi za kiraia kushiriki katika mchakato wa maandalizi.

Alipoulizwa endapo Umoja wa Mataifa una mpango wa kufanya mazungumzo na nchi wazalishaji wa nishati ikiwamo mafuta, gesi na makaa ya mawe, anasema mazungumzo tayari yameshaanza.

Katibu Mkuu anadokeza kuwa kuna changamoto katika sekta hiyo na ni vigumu, lakini sekta hizo zimeendelea kutambua haja ya kuhamia kwenye suluhu ya nishati mbadala.

Mkutano huo pia utaangazia masuala sita anayotaja kuwa: Mabadiliko kuelekea nishati mbadala; ufadhili wa hatua za mabadiliko ya tabia nchi; gharama za hewa ya ukaa; kupunguza uchafuzi utokanao na gesi ya viwandani.

Mengi yanayotajwa ni kutumia maliasili kama suluhu, kuwa na miji endelevu, hatua kuanzia ya mashina na mwnendo dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mwezi uliopita, Katibu Mkuu alimteua, Luis Alfonso de Alba, kuwa mwakilishi wake maalumu wa mkutano huo.

Akihudhuria mkutano huo, mwakilishi huyo anasema kwamba moja ya vipaumbele vyake katika miezi ijayo, ni kushirikiana kwa karibu na kila mdau wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi, ili kuwahamasisha.

“lengo sio kujadiliana matokeo bali ni uhamasishaji wa ushiriki wa ngazi ya juu , kuchagua nini kitakachokwenda kwenye mkutano kwa mantiki ya hamasa na ubunifu na kisha kuwa na mukhtasari wa majadiliano wakati wa mkutano wenyewe,” anafafanua.

Katika kufungua pazia la mkutano huo, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, litakuwa na mkutano maalum mwezi Machi mwakani.

Makala hii ni kwa mujibu wa taarifa za Umoja wa Mataifa.

Habari Kubwa