URUSI Vs UKRAINE

25Jan 2023
Na Waandishi Wetu
URUSI
Nipashe
URUSI Vs UKRAINE
  • Putin amebakia kuwatumbua makamanda, vita ikimwelemea

UNAPOKARIBIA mwaka mmoja wa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, mapambano yanaendelea tena yakiongeza hali ngumu kiuchumi duniani, kuanzia chakula, nishati na bidhaa za viwandani.

Kwa kifupi ni kama mambo ya mvamizi Urusi ni mabaya na safari hii Rais Vladimir Putin, anabadilisha tena viongozi wa vita akimteua Ofisa Mkuu wa Kijeshi, Valery Gerasimov kuwa msimamizi wa uvamizi wa nchi hiyo dhidi ya majirani zake Ukraine.Ni katika kutumbua kulikofanyika karibuni tangu kuanza kwa vita. Amiri jeshi mkuu anamteua Gerasimov Mnadhimu Mkuu wa Jeshi kuimarisha vita vinavyodaiwa na nchi za Magharibi kuwa Urusi imeshindwa.

Miezi mitatu tu baada ya kufanya mabadiliko ya mara ya mwisho, Putin amemteua kamanda mwingine wa kuongoza kampeni ya Urusi nchini Ukraine, akionyesha kutoridhishwa kwa Kremlin na mwenendo wa kile kinachoitwa "operesheni maalum ya kijeshi" iliyozinduliwa Februari 24 mwaka jana
Ofisa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, au mkuu wa wafanyakazi jeshini, amefanyakazi hiyo  kwa muongo mmoja uliopita, katika mabadiliko yaliyomshusha cheo mtangulizi na bosi wake Sergei Surovikin, aliyetumbuliwa baada ya siku 95 za kufanyakazi ya kuongoza majeshi ya Urusi kuipiga Ukraine.

Mabadiliko hayo yanamaanisha kuwa sasa ni juu ya "mtu wa tatu muhimu zaidi katika uongozi wa kijeshi wa Urusi - baada ya Putin na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu, kurekebisha hali ya Ukraine," anasema Jeff Hawn, mtaalamu wa jeshi la Urusi na mshauri wa Marekani katika kituo cha utafiti wa kijiografia na kisiasa cha New Lines.

Wanaomfuatilia nyendo zake wanasema ni mtu wa wastani kuliko 'Jenerali Armageddon'

Valery Gerasimov (67), sio tu ofisa wa cheo cha juu zaidi katika jeshi; yeye pia ni aina tofauti sana ya kamanda kutoka kwa Sergei Surovikin, ambaye aliitwa “Jenerali Har–Magedoni” kwa sababu ya ukatili na ubakaji.

Akiwa mkuu wa muda mrefu zaidi wa wafanyakazi au Mnadhimu Mkuu tangu nyakati za Soviet, Gerasimov, anaweza kujivunia mafanikio yakiwamo ya zamani huko Chechnya na Crimea. "Pia anaonekana kama ana ushawishi wa kudhibiti mambo kuhusu vita na ni mtu ambaye Washington inaweza kufanya kazi naye," anasema Hawn.

 

“Yeye si ‘Jenerali Har–Magedoni’ kama Surovikin aliyetumbuliwa, kwa hakika, lakini haijulikani wazi ni kiasi gani cha matokeo anayoweza kuleta kwenye vita na hasa wakati huu wa mapigano,” aonya Stephen Hall, mtaalamu wa Urusi katika Chuo Kikuu cha Bath.

Anaongeza kwa hakika, "hata kama angetaka kurekebisha mfumo wa uendeshaji wa jeshi la Urusi, hatakuwa na vifaa, wala njia, wala wafanyakazi wa kufanya hivyo wala mbinu mpya," anaongeza Hawn.

Kwa mtazamo wa kijeshi, mabadiliko au kutumbua huko ni "uthibitisho kuwa ulihitajika na kwamba kutakuwa na mambo mabaya siku zijazo na kwamba hata Putin anatambua kuwa uratibu mbaya wa shughuli za kivita umekuwa tatizo na ndilo suala lililochangia kuboronga," mchambuzi wa usalama wa Urusi Mark Galeotti, anaandika kwenye mtandao wa twita.

Kwa hivyo mambo haya yanamaanisha nini? Mosi ni uthibitisho, ikiwa tuliuhitaji muongozo mwingine au kwamba kutakuwa na mambo makubwa mabaya yanayokuja na kwamba hata Putin anatambua kwamba uratibu mbaya wa mambo umekuwa chanzo cha kuchemka huko Ukraine.

Ingawa hata Gerasimov anapoingia sasa anaweza kuamrisha vikosi vya jeshi na kundi la mamluki kuwaamrisha mamluki Wagner na jeshi la Kadyrovtsy, kweli? Ndiyo ujumbe wa twita.

 

Katika taarifa iliyotangaza kuteuliwa kwa Gerasimov, ikitolewa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi inasema lengo ni "kuandaa uratibu na kufanyakazi kwa karibu kati ya matawi ya jeshi". Majukumu yake hayo pacha kama Mnadhimu wa Jeshi na Kamanda Mkuu nchini Ukraine yanamaanisha kuwa ana zana zote mkononi za kutekeleza jukumu hilo na anatarajiwa kuwa ataweza kuwasilisha mbinu mpya angalau kwa kuandika kwenye karatasi.
Kumtoa Gerasimov kafara au kudhoofisha maluki ya Wagner? Ni swali ambalo wachambuzi wanahoji? Umuhimu wa kutumbua hata hivyo, unaweza kuwa wa kisiasa, ukifika wakati wa mabadiliko katika vita vya kiushawishi kati ya jeshi la Urusi na kikundi cha mamluki cha Wagner kinachoongozwa na mfanyabiashara bilionea Yevgeny Prigozhin.

Hali ya Jeshi la Urusi imeonekana kuwa taabani, na uthabiti na uwezo wake umeporomoka vibaya baada ya msururu wa vikwazo nchini Ukraine lakini shambulio baya la mwaka mpya la makombora mazito kwenye kambi ya Warusi huko Makiivka, ambalo lilibainisha uzembe na kukosekana weledi wa viongozi wakuu wa kijeshi.

Cha kushangaza wakati kambi ikilipuliwa bilionea Prigozhin na mamluki wake wa Wagner wamekuwa wakitunishiana misuli kuzungumzia vita vikali huko Soledar, vikipiganwa mapema mwaka huu wakidai waliwashinda walishinda na kuuteka mji wa Donbas wa Ukraine pekee. Wakiwa wamekasirishwa na maneno ya Wagner, Jeshi la Urusi liliwahi kuelezea kwamba mapigano bado yalikuwa yanaendelea na kwamba askari wake wa miavuli walihusika sana katika vita hivyo vya Donbas.

Wakati matokeo ya umwagaji damu huko Soledar bado hayajulikani, Kundi la Wagner tayari limeshinda vita vya kujigamba na kujiimarisha maoni huko Moscow kwamba wanamgambo wa hao mamluki wa Prigozhin wako mstari wa mbele katika vita vya Urusi katika miezi kadhaa. Hivyo kupewa ‘sapoti’ zaidi na wakosoaji wa kitaifa wa kijeshi na kumruhusu bilionea Prigozhin anayewasimamia mamluki hao  kupata sifa zaidi ya mpinzani wake huko Kremlin, Waziri wa Ulinzi Shoigu.

Kwa kuzingatia mabadiliko hayo uteuzi wa Gerasimov ni "kuona kama onyo lililotolewa na Putin kwa Prigozhin wa kundi la Wagner, kwa hivyo hafikirii kuwa anaweza kufanya chochote anachopenda", anasema Hall.

Akiwa mmoja wa washirika wa karibu wa Waziri wa Ulinzi Shoigu, kamanda mkuu  mpya inamaanisha uwezekano wa kulinyima uhuru kundi la Wagner au kulipa uhuru kidogo zaidi kuliko mtangulizi wake Surovikin, ambaye anachukuliwa kuwa karibu kiitikadi na bilionea Prigozhin hivyo kuwabeba mamluki.

Hata hivyo kuanzia sasa na kuendelea, Kamanda Mkuu  Valery Gerasimov, yuko kwenye mstari wa kutumbuliwa na hawezi tena kuwalaumu wengine iwapo hali itazidi kuzorota nchini Ukraine inaonekana kama amewekwa katika hali ya kukwama, ambayo itampa Putin kisingizio cha kumwondoa jeshini kwa ulaini iwapo hali itaendelea kuzorota zaidi kwenye vita vya Ukraine.

CHANZO FRANCE 24

 

Habari Kubwa