Utamaduni na kanuni mbovu za ulaji, mvuto wa magonjwa yasiyoambukizwa

14Jan 2021
Michael Eneza
Dar es Salaam
Nipashe
Utamaduni na kanuni mbovu za ulaji, mvuto wa magonjwa yasiyoambukizwa
  • Zaingia taratibu, zina ubishi kutoka
  • Nyama iko maarufu mezani, lakini…

JITIHADA zimekuwa zikifanyika miaka mingi kuielimisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora ili kuzuia magonjwa yasiyoambukizwa.

Kuna siku kadhaa za kimataifa zimewekwa ili kuwezesha uwapo wa mitandao ya kuandaa mijadala na harakati za aina tofauti kuhusu umuhimu wa lishe bora, lakini kiwango cha ufaulu kimebaki suala la mjadala.

Taasisi za afya za kiserikali na vikundi huriam bado vinaendelea kuhimiza lishe inayofaa, ingawa havina mamlaka kamili ya kisheria, katika ukiukwaji wake ambao, huzaa matokeo magonjwa yasiyoambukizwa yanakuwa na gharama kubwa.

MTIHANI WA UDHIBITI

Watalaamu wamekuwa wakitafuta chanzo cha kushindwa kufuata maelekezo ya lishe bora kwa ajilii ya afya ya muda mrefu, kwani magonjwa yasiyoambukizwa hujijenga taratibu mwilini, yakichukua muda mrefu.

Athari yake, inachukua sura pale yakishajikita mwilini katika mfumo wa mzunguko wa damu, inakuwa ngumu kuondolewa, kwani sababu yanakuwa sehemu ya kilichoko mwili.

Tabu iliyoko katika mfumo wa maisha ni kwamba. kinachofanyika katika mwili wa binadamu kinaanza na mazoea, kana kwamba ndicho kinachotakiwa, wakati ukweli ulioko kwamba ni uharibifu tu.

Sehemu ya tatizo kubwa zaidi kwa mwanadamu, ni namna ya kupanga viwango vya sukari na mafuta, kulinganisha na mahitaji halisi mwilini.

Kutumia lishe ya aina fulani kwa wingi au kila wakati kunauzoesha mwili kuikubali aina hiyo ya lishe na kuondoa vipingamizi vinavyohusu ama sukari au mafuta kwa viwango vinavyotakiwa mwilini.

Ni kuanza ratiba au mpangilio mpya wa kuchukua chembe za lishe hizo kutokana na upatikanaji wake, hali inayofanya sukari au mafuta kutawala mwilini, kuzuia mtiririko wa kawaida wa sukari au mafuta kuingia, kutumika na kutolewa mwilini.

Kisha inaelezwa, kiwango kingine kinaingia na kufuata mkondo huo huo na inapofikia mahali mwili unakosa uwezo wa kudhibitio sukari au mafuta, zenyewe ndizo zinautawala mwili. Ndio hatua ya magonjwa kuanza kuchukuia nafasi yake.

WIGO WA UTAFITI

Katika nchi zinazoendelea kama barani Afrika, hakuna tafiti nyingi zinazofanyika kuhusu lishe, mazoezi na afya, kulinganiasha na kulikopiga hatua zaidi ya maendeleo kama bara Ulaya na ufuatiliaji wa kina unafanyika kutoka taasisi tofauti za tiba za serikali na binafsi.

Matokeo yake hutumika kama kama vigezo vya kupitisha au kupinga hitaji la mabadiliko ya sheria kuhusu bidhaa za vyakula na vinywaji, ambako kuna makundi tofauti, mathalan penye mlo, bidhaa za nafaka na nyama upnde mmoja, pia vinywaji baridi na vilevi upande mwingine.

Nguvu ya sheria ipio katika maendeo kama kila badiliko la kodi, huwezesha aina moja ya bidhaa na kuvuruga matazamio ya bidhaa ya aina nyingine. Hivyo, kuna vita ya kibiashara inayojificha katika tafiti za lishe.

Kwa mfano kuna tafitii zinazotajwa na hata kaulimbiu ya taasisi tofauti za afya kuwa ‘sukari ni sumu’ ikidaiwa iwekewe sheria inayohusu ununuzi na matumizi yake, lakini kuna sura ya pili majibu, kwamba siyo rahisi mwanasiasa au mwanaharakati anayetaka mabadiliko kuashiria kudhihirisha ukweli ulioko.

Inajenga tafakari ya hoja kati ya sukari na mbadala wa asali na siagi mwilini na matokeo yake. Katika nchi nyingi zilizoendelea kama UIaya, nyama hasa nyekundu ni chakula halisi na msingi wa lishe ya kila siku, mfano mmojawapo ni mlo mkuu ama mchana au usiku huwa ni nyama, ikiandamana na mboga za kuusindikiza.

Watumiaji lishe ya nafaka kama ugali au wali kuwa msingi na inachosindikiza ni nyama, samaki ua maharagwe walio nayo ni wahamiaji.

Kutokana na kupenda kutumia nyama kama chakula kikuu takriban kila siku, kinatajwa kuchochea magonjwa ya moyo, watu wengi wanajaribu kutumia lishe za ziada kupunguza athari hizo.

WANAKOKWAMA WALAJI

Pia, vitamini zinaoandaliwa maabara, badala ya kupatikana kutokana na lishe halisi na baadhi ya wataalamu wanatia shaka uwezo wake kumsaidia mhusika.

Msisitizo wa kitaalamu ni kwamba mabadiliko ya lishe na mazoezi ni muhimu, ila bado kuna tatizo la watu kufahamu hasa ni nini kinachozuia watu kuchukua mwekeleo wa ‘lishe bora’ na siyo ‘bora lishe

Kwanini watu wanazama katika nyama? Kuna sababu muhimu mbili zinazoshindana. Moja ni utamaduni kwa maana ya mapokeo lishe na mazoea katika maisha ya mtu binafsi, hali ambayo pia inajichanganya na hisia za kitabaka, kula ni kielelezo cha umaskini na aliyeko vizuri kiuchumi anakula nyama.

Hisia hizo zinapotawala mtu kukubali cha upande wa pili kisayansi, chakula kuleta shida katika msukumo wa damu, kisukari.

Lakini kuna wanaorekebisha fikra na kujielimisja kwenda katika ukweli kufahamu kwamba tahadhari ya lishe ni muhimu zaidi, ingawa kuchukua hatua kudhjibiti bado ni shida. Mathalan, mtu mzima anaona aibu kufanyua mazoezi kukimbia hadharani, wengine wanabaki kuugua kimyakimya

Katika nchi zilizoendelea, kuna uwezekano mkubwa zaidi wa elimu kuleta mabadiliko katika mazoea lishe. Miongoni mwa makundi makubwa ya watu na tafiti zinaonyesha kuwa waliosoma zaidi, wako makini kwa mausala hayo kuliko wenye elimu ya kawaida, iwe sekondari au ufundi).

Hata hivyo, kuna tatizo sugu la lishe kwa sababu wengi wanajiwekea mipaka kwa kuhofia magonjwa na siyo kwa kupenda lishe mbadala, hivyo wanakuwa kama mtu anayetaka kuacha sigara halafu aporomoke tena, aendelee, aache tena.

Ni hapo anachukua hatua ya vigezo vingine kama vile vya kitabaka au kijinsia kuhoji mfano wa wanaoshiriki urembo au hata warembo kwa jumla, wana uwezo kiasi gani wa kujizuia lishe kwa mazoea hata wakapunguza unene na uzito?.

Habari Kubwa