Vimbunga pasua kichwa usalama mazingira dunia

14Nov 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Vimbunga pasua kichwa usalama mazingira dunia
  • Marekani kila siku, hasara shilingi trilioni nyingi

VIMBUNGA ni tatizo. Huo kimsingi, ni mfumo wa upepo unaosafiri kwa kasi kubwa majini na hasa kwenye bahari na mara nyingi unapatikana katika ukanda wa kitropiki, ambao hali ya hewa yake inatawaliwa na joto.

Hali halisi ya madhara ya kimbunga kilichotokea katika pwani ya Beira, nchini Msumbiji. PICHa mtandao

Nadhani katika nchi jirani ukanda wa baharini, kama vile taifa la Msumbiji kwamba ‘zimeonja’

Ni aina ya upepo unaokimbia kwa kasi ya maili 74 kwa sasa, ambayo ni sawa na kilomita 119 kwa sasa. Wataalamu wameipa jina ’tropical cyclone.’

Watafiti wa kisayansi wana hoja kwamba mabadiliko katika kiwango kilichofika sasa ni kwamba, vimbunga vinakimbia katika kiwango mara tatu, ikilinganishwa na ilivyokuwa miaka 100 iliyopita.

Kuna juhudi kadhaa zimekuwa zikifanyika kukabili vimbunga hivyo, ingawa bado hakujapatikana mafanikio yenye uhakika.

Hadi sasa, vimbunga hivyo vinaingia katika hesabu ya kuwa vyanzo vya asili vyenye uharibifu mkubwa katika jamii’ zikitawaliwa na Kimbunga Katrina, kilichotokea mwaka 2005, ambacho zaidi ni nchini Marekani.

Huko kunatajwa kutia hasara Dola za Marekani bilioni 125 (shilingi trilioni 287.5) ambayo ni kiasi cha wastani wa asilimia moja ya Pato la Taifa la nchi hiyo.

Swali kubwa la kitaalamu linalotawala hivi sasa, ni namna gani mtu anapigana dhidi ya vimbunga baina ya eneo moja na lingine, pia usalama wa mali zao.

Katika kukagua athari hizo za vimbunga vya kila siku, watafiti wanasonga mbali kukagua madhara kiuchumi, kwamba haishii katika mali tu, bali hata ardhi inavyoharibiwa.

Kwa kufuatilia uhalisia kupitia vigezo mbalimbali, watafiti wamebaini athari za vimbunga imeogezeka kwa wastani wa asilimia 330, kwa kila muongo mmoja unaopita na chanzo kikuu ni ongezeko la joto.

Pia, mtazamo wa watafiti kufafanua uhalisia ulipo ni kwamba mbinu na mitazamo yao katika kupata majibu ya uhalisia huo, bado ni sahihi zaidi katika kupata ukweli ulivyo.

Watafiti Wamarekani waliifuatilia kimbunga mwaka juzi na kuathiri wastani wa watu milioni 1.1 katika makazi ya watu yenye ukubwa wa kilomita za mraba10, 000.

Kimbunga Dorian kilichotokea hivo karibuni huko jimboni Florida, mwezi Septemba ilitia hasara ya kasi kikubwa sana cha pesa.

•Kwa mujibu wa taarifa za mtandao.

Habari Kubwa