Wa5 wakuvaa viatu vya Ronaldo Madrid

26Jun 2017
Na Mwandishi Wetu
MADRID, Hispania
Nipashe
Wa5 wakuvaa viatu vya Ronaldo Madrid

RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez yupo katika kibarua kigumu cha kumshawishi Cristiano Ronaldo kuendelea kubaki katika klabu hiyo.

Hali hiyo inatokana na straika huyo kutangaza nia yake ya kuondoka Hispania kufuatia kukerwa na tuhuma za kukwepa kodi kutokana fungu aliloingiza katika haki zake za matangazo.

Manchester United, PSG ni miongoni mwa klabu zinazopewa nafasi ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ureno endapo kweli atakomalia uamuzi wake huo, lakini je, kama akifikia hatua hiyo ni nyota gani wanaoweza kuvaa kiatu chake Real Madrid…

1. Eden Hazard
Eden Hazard, sio siri kuwa Real Madrid wamekuwa wakimfuatilia mshambuliaji huyu wa Chelsea tokea mwanzo wa dirisha la usajili kufunguliwa na wanasababu nzuri ya kufanya hivyo. Hazard anaweza kutumika kama mbadala wa Ronaldo amefunga mara 16 msimu ulioisha amekuwa na mchango mkubwa kwa mabigwa wa Premier League.

Mchezaji huyu amenukuliwa akisema anatamani kushinda vikombe vitatu na Blues na kufanya kuongeza nafasi yake Stamford Brigde.
Lakini Madrid walikuwa karibu kushinda vikombe vitatu mwaka huu na kama Ronaldo ataondoka watakuwa na kiasi kingi cha pesa kwa ajili ya kumsajili.

2. Kylian Mbappe
Kylian Mbappe akiwa anatizama hatima yake katika kipindi hichi. Kipaji hiki bora toka Monaco kimekuwa kikihusishwa na baadhi ya klabu katika wiki za karibuni; Arsenal, Manchester City na Real Madrid ni miongoni mwa hizo, amefunga mara 15 katika kipindi cha msimu wa 2016/2017 na kushinda ubingwa wa Ligue 1 akiwa na Monaco.

Mbappe anaweza kuwa vizuri kucheza pamoja na Benzema na Gareth Bale, lakini Real Madrid wanaweza kumchukua kabla ya PSG au Arsenal?

3. Paulo Dybala
Mshambuliaji huyu wa Argentina, amekuwa akitambuliwa kama mrithi wa Lionel Messi, lakini hakuna aliyewahi kusema hawezi kuwa Ronaldo. Akifunga mara nne katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutoa pasi za mwisho mara nane kwa Juventus, Dybala anaweza kuwa mchezaji sahihi kwa Zidane.

Muargentina huyu amekuwa Juventus kwa miaka miwili na haikumchukua muda mrefu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza; tangu kuwasili kwake, kikosi cha Turin kimeshinda mataji mawili ya Seria A na taji la Kombe la Italia mara mbili.

Klabu yake ya sasa ilishindwa mbele ya Real Madrid mwaka huu katika mechi ya fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo inaweza kuwa sababu nzuri ya kubadilisha mawazo.

4. Antonie Griezmann
Antonie Griezmann ametuma ujumbe kwa mashabiki wa Atletico Madrid. Jose Mourihno ameonyesha kumhitaji na Manchester United, lakini amekataa na kuchagua kubakia Atletico.

Lakini uaminifu wa Griezmann kwa Atletico haitoshi kama Real watampa nafasi ya kucheza kama mshambuliaji wa mbele katika klabu hii bora barani Ulaya.

Griezmann ameifungia Atletico mara 16 mwaka uliopita na alionyesha katika mashindano ya Euro 2016, na ni mmoja wa wachezaji waliochaguliwa kugombea tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya (Ballon d’Or) kwa mwaka 2016.

Mara mbili katika mwaka uliopita Ronaldo amemfanya kushindwa kushinda taji; katika fainali ya Euro 2016 na nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Mfaransa huyu anaweza kuwa hajashawishika kuhamia kwa Mourihno, lakini kuwa mbadala wa Ronaldo hatohitaji hata kubadilisha anuani yake!

5. Neymar
Neymar anaweza kuwa mbadala sahihi wa Ronaldo, wana ujuzi na tabia za kufanana, wote wemecheza kama washambuliaji wakitokea pembeni na wanapua za kunusa mabao. hata hivyo, itakuwa ngumu kuamini Mbrazili huyu kuvaa jezi ya Real Madrid, haikataliki huyu ndiye mbadala sahihi.

Uhusiano wake na Messi na Suarez unaonyesha hayupo tayari kuhama Nou Camp kwa sasa, japokuwa hatima yake haijaeleweka kwa Barcelona waliofanya mabadiliko ya kocha mwishoni mwa msimu huo haukuwa katika matarajio yao.
Kuama kwa sasa inaweza kuwa njia nzuri ya kuanza upya.

Habari Kubwa