Wachina wanavyochinja mbwa mil.10 kila mwaka

26May 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wachina wanavyochinja mbwa mil.10 kila mwaka

ULAJI nyama ya mbwa katika jamii nyingi ni haramu.

Hiyo inaenda mbali zaidi, hata kugusa baadhi ya imani kwamba ulaji nyama hiyo ni haramu kubwa.

Pia katika kauli inayohusiswa na utani, ulaji nyama ya mbwa unaelezwa kwa baadhi ya makabila nchini kwamba ni jambo la kawaida, ikitumika kama kitoweo.

Huko nyuma jijini Dar es Salaam katika eneo la Upanga Magharibi, kulitokea tatizo la kutoweka mbwa wa wakazi mtaani.

Baada ya kufuatilia chanzo cha hali hiyo, ilibainika raia wa nchi mmoja ya bara Asia, aliyekuwa mkazi wa eneo hilo, alikuwa na tabia ya kuua mbwa hao wa majirani zake na kisha kula nyama zao.

Wataalam wa afya wanaichambua nyama ya mbwa kuwa nzuri kwa sababu ina viini lishe kama vile mafuta, rehemu, vitamin A, B1, B2, B3 nk.

Miongoni mwa maeneo ya bara Afrika ambako nyama ya mbwa inalika kwa wingi ni nchi kama vile Cameroon, Ghana, Nigeria, Morocco, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)na Liberia.

Ulaji nyama ya mbwa una sura mbili. Inaliwa kama sehemu ya utamaduni wa jamii, pia wakati wa shida ikiwamo kwenye vita na pana[oskosekana chakula mbadala.

Katika baadhi ya sehemu, nyama ya mbwa inaliwa katika staili inayoendana na kuhitimisha utamaduni wa jamii husika.

Nchi za ugahibuni kama vile
China, Vietnam, Thailand, Uswisi, Canada, Mexico, Hong Kong, Taiwan, India, Indonesia, Japan, Korea Kusini,Ufilipino na New Zealand.

Kwingineko ni Uingereza, Ireland, Ubelgiji, Ufaransa, Uholanzi na Poland, Thailand, Visiwa vya Timor, Visiwa vya na Vietnam.

Takwimu za kimataifa mwaka za juzi,
zinabainisha kwamba watu walikula jumla ya mbwa milioni 25 duniani kote

Nchini Marekani kuna madai nyama za mbwa zilitengezewa soseji hadi miaka ya 1845 ndipo ilipoachwa

Lakini haina maana nyama hiyo hailiwi rasmi nchini Marekani hivi sasa. La hasha! Inaliwa na wengi katika taifa hilo linalojumuishwa na wakazi wenye asili tofauti, pia wanaotoka mataifa mbalimbali.

Inapatikana rasmi katika maduka ya nyama kwa kuuuzwa, baada ya kupitia michakato yote ya ukaguzi kiafya, kama inavyofanywa kwa mifugo mingine.

Huko DRC, kuibuka maradhi ya ebola ambayo tiba yake ni tatizo na imeua watu wengi, ilisababisha mabadiliko katika ulaji nyama ya mbwa.

Kwa kiasi kikubwa ilipungua sana, kutokana na madai kwamba jumla ya mbwa 156 nchini humo waliambikizwa ebola.

Nchini Morocco, licha ya serikali kutunga sheria inayokataza ulaji wa nyama hiyo, bado kuna sehemu kubwa ya jamii inayotumia nyama hiyo.

Wananchi wa Nigeria, katika baadhi ya maeneo wanakula nyama ya mbwa katika baadhi ya maeneo wakiwa na imani kwamba ni dawa.

Hata hivyo, kuibuka ebola kumechangia kupunguza ulaji nyama ya mbwa nchini Nigeria, kama ilivyo nchini DRC na kwingineko kulikokumbwa na maradhi hayo na kunaliwa nyama ya mbwa.

WACHINA NA NYAMA YA MBWA

Nchini China ndiko kwenye ulaji wa nyama ya mbwa wa haIi ya juu duninani, ambako kunakadiriwa mbwa milioni 10 wanachinjwa kila mwaka, hususan jimboni Guangdong.

Kiasi hicho ni wastani wa asilimia 40 ya mbwa wote wanaoliwa duniani kwa mwaka.

Unapofika msimu wa baridi, Wachina wanadaiwa kula nyama ya mbwa kwa wingi, wakiamini inawaletea joto mwilini.

Wachina pia ni vinara wa kula nyoka, ikiwa, nyama inayouzwa kwa bei kubwa kutokana na kuwa adimu.

Mtanzania aliyewahi kuishi nchini China (jina linahifadhiwa) alieleza uzoefu wake wa kula nyama ya nyoka, anaifanananisha na ladha ya samaki nahuliwa na watu wenye uchumi mzuri, kutokana na bei yake kubwa.

Ni kawaida mtu akiwa nchini China, akiingia katika mgahawa na kukuta miongoni mwa nyama zinazouzwa ni pamoja na mbwa, ambao wanafugwa shambani kama ilivyo mifugo mingine.

Pia, nyama ya paka inauzwa kwenye migahawa kwa staili hiyo ya mbwa na ina wateja.

SHEREHE YA KULA MBWA

Katika kinachoonyeha nyama ya mbwa ina thamani kubwa kwa umma, kuna utamaduni wa kuandaa maadhimisho maalumu ya mwaka ya kula nyama ya mbwa kwa siku kadhaaa mfululizo.

Hata hivyo, katika sura ya pili kuna wanaopinga maadhimisho hayo, wakidai si sehemu ya utamaduni wa Wachina, bali ni tukio la kibiashara zaidi, kuipatia soko ya nyama hiyo.

Katika miaka ya karibuni, utamaduni huo umefungua mlango zaidi kuhamia hadi kwenye ulaji nyama ya paka.

Mwaka 2011, sherehe za namna hiyo zilifanyika na kudumu kwa siku 10 na jumla ya mbwa 15,000 walichinjwa na kuliwa.

Namna nyama ilivyoandaliwa, inajumuisha kuchoma na nyingine ya kuchemsha kupata supu na kongoro.

Uuaji wa mbwa hufanyika kama ilivyo kwa nguruwe. Anapigwa kichwani kupoteza fahamu na ndipo anachinjwa na nyama inayopatikana ina soko kubwa.

Watu hupanga foleni ndefu kununua nyama hiyo inayouzwa kwa bei ya wastani wa Pauni nne (Sh. 12,700) kwa kilo.

Jijini hapo kuna majengo ambayo ni sehemy za kuchinjia mbwa zisizopugua 100 ambazo huchinja wastani kati ya mbwa 30 na 100 kwa siku kwa kila sehemu.

Hivi sasa kuna kampeni kutoka kwa wanaharakati kuzuia uchinjaji huo wa mbwa na hivi karibuni jumla ya watu 3,000,000 walitia saini azimio la pingamizi kutaka serikali ifunge nyumba hizo za kuchinja mbwa.

Azimio hilo lliwasilishwa kwa Waziri wa Kilimo, Chen Wu na inasomeka:" Fanya kitendo cha kibinadamu kwa kukataa maadhimisho haya na kukokoa maisha ya mamia ya mbwa wanaotolewa kafara kutokana ma tukio hili.

“Ni tukio linalohuisiana na kuwachinja, kuwachuna wakiwa hai, kuwapiga hadi kufa mamia ya mbwa wasio na makosa.”

Aidha, waraka huo unasemeka:"Kabla ya maadhimisho ya mwaka 2014, madaktari na wauguzi walipigwa marufuku kula mbwa mahali hapo (kwenye sherehe).

“Kwenye migahawa inayouza nyama ya mbwa, iliagizwa kuweka tangazo linalosomeka ‘mbwa’ katika mbao zake za matangazo.”

Harakati hizo za kupinga ulaji wa nyama za mbwa ziliongezeka maradufu, na kuwepo vikundi vingi vya kupinga nchini China, chini ya kivuli cha umoja wao unaojulikana kama Mtandao wa Wachina wa Kuwalinda Wanyama(CCAPN)

MARUFUKU YA NYAMA

Wakati wa michezo ya Olimpiki iliyofanyika mjini Beijing mwaka 2008, serikali ilipiga marufuku kwa muda, uuzaji nyama za mbwa katika migahawa 112 iliyoteuliwa kuhudumia wageni.

Baadaye mwaka 2010, serikali ilileta muswada unaopiga marufuku ulaji nyama ya mbwa, lakini umekuwa ukikwama kupitishwa.

Sababu kuu, China ni nchi ya biashara ya kimataifa na hivyo inatembelewa na wageni wengi, baadhi ni walaji nyama ya mbwa.

Katika mapendekezo hayo ya sheria ni kwamba, mtu atakayetiwa hatiani akila nyama ya mbwa, atatiwa kifungoni hadi siku 15.

MAUZO YASHUKA HOTELINI

Misukosuko ya karibuni imeyumbisha biashara za nyama za mbwa na paka katika migahawa mingi nchini China.

Tangu mwaka 2013, mauzo yanadaiwa kushuka kwa kasi kubwa, wastani wa theluthi moja ya mauzo ya nyama hizo imeshuka.

Pia inaelezwa hali hiyo imebana kibiashara, hata mgahawa mmoja maarufu wa jijini Guangzhou kwa kuuza nyama za mbwa na paka, ulilifungwa mwaka jana, baada ya kudumu tangu mwaka 1963.

Sababu kuu iliyoleta ugumu huo kutokana na kuweka sheria ngumu kwa migahawa inayofanya biashara ya kuuza nyama hizo.

Pia katika miji ya Yuancun and Panyu, kuna migahawa maarufu kwa kuuza nyama za paka na mbwa, nazo zilifungwa mwaka jana.

Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa taarifa za mtandao.

Habari Kubwa