Wagundua ngazi mpya tano za kisukari

08Mar 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wagundua ngazi mpya tano za kisukari

Wanasayansi wamebaini kwamba, licha ya kuwepo maradhi ya kisukari yanayotambulika katika sura kuu mbili, kuna mengine matano yaliyojificha.

Mgonjwa wa kisukari akihudumiwa. PICHA: MTANDAO.

Wakati aina ya kwanza inatokana na mwili kwa asili yake unashindwa kudhibiti sukari, aina ya pili inatokana na mlo mbaya unaochangia kuharibu usimamizi wa sukari mwilini.

Wasomi wa Sweden na Finland, wanasema kisukari duniani kipo katika wastani kila kundi la watu 11, mmoja anaugua na ina sura tano mpya, walizozichapisha katika jarida la kisomi;Lancet Diabetes and Endocrinology.

Mosi, inayowahusu watu wenye umri mdogo, afya njema, lakini miili yao haizalishi kinga kudhibiti sukari.

Pili, vijana wenye afya njema, wanaoshindwa kuzalisha kinga ya sukari wakati chembe (insulin) za kinga hizo hazijaathirika; Kundi la tatu ni wenye vitambi ambao wana tatizo kama kundi la pili.

Nne, wenye uzito mkubwa na miili haipokei kazi za insulin; na mwisho ni wanaopata kisukari katika umri mkubwa.