Wanaoishi barabara kubwa kumbukumbu zao zinakufa

12Jan 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wanaoishi barabara kubwa kumbukumbu zao zinakufa

UTAFITI wa wasomi katika sekta ya afya kupitia taasisi ijulikanayo kama Lancet, umegundua watu wanaoishi jirani na barabara kubwa, wanaathirika na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu.

Katika utafiti uliofanyika nchini hapa kwa miaka 11, kati ya mwaka 2001 na 2012, unaeleza asilimia 10 ya wanaoishi walau umbali wa mita 50 kutoka barabara kubwa, wanapata maradhi yanayohusiana na kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kufikiri.

Ni utafiti uliofanyika ndani ya miaka 11 na kuhusisha jumla ya watu milioni mbili, umetoa sababu kuwa kuathirika huko kunatokana na athari za kelele na hewa chafu kutoka barabara kuu.

Hata hivyo, watafiti wenza kutoka Uingereza wanasema licha ya mafanikio hayo ya kitafiti, kazi zaidi inatakiwa kufanyika ili kupata ukweli wa kina kuhusu jambo hilo.

Wakati nchini Canada kuna takwimu hizo za watu milioni mbili, duniani kote kunadaiwa kuwapo waathirika wa namna hiyo wanaokadiriwa kufika milioni 50.

Hata hivyo, hatua hiyo ya mafanikio katika utafiti haijabainisha namna ugonjwa unavyoweza kumfikia mwathirika wa maradhi hayo.

Ni utafiti uliofanyika kati ya mwaka 2001 na 2012 na imefahamika kuwa wanaoishi mbali na barabara wastani wa mita 300, hawakuwa na athari hizo zinazoelezwa kuwepo.

Ripoti ya utafiti ilikuwa na ufafanuzi kwamba, wanaoishi ndani ya umbali wa mita 50 kutoka barabara kuu, waliathirika kwa wastani wa asilimia saba ya idadi ya watu wote waliochunguzwa.

Pia, kwa wanaoishi umbali wa kati ya mita 50 na 100, asilimia nne ndio waathirika; huku kundi lingine linaloishi katika umbali kati ya mita 101 na 200 kutoka barabarani, waathirika walikuwa asilimia mbili ya wakazi hao.

Mtaalamu kutoka Taasisi ya Taifa ya Afya ya Otario, Dk. Hong Chen, anasema katika ripoti yake: “Kuongezeka kwa wakazi na mji kumewaweka wengi karibu na barabara kuu na namna wanavyokuwa karibu na magari mengi, ndiyo kunaongezeka kazi ya Dementia (maradhi ya kupoteza kumbukumbu).”

“Hata athari ndogo kutoka barabara kubwa, inaweza kusababisha athari kubwa kwa umma. Utafiti zaidi unahitajika kuelewa uhusiano baina ya mambo mbalimbali ya magari barabarani, kama vile uchafuzi wa hewa na kelele.”

Inapendekeza kufanyika utafiti kuhusu athari za vipande vidogo vya mawe au vumbi na hewa, kwani wanadai utafiti umehusu maeneo wanakoishi waathirika na hewa yenyewe, wakisisitiza kwamba kilichotafitiwa ni makazi ya waathirika na si namna walivyoathirika.

Mtaalamu bingwa katika maradhi yanayohusiana na kubukumbu nchini, Uingereza, Profesa Martin Rossor, kutoka Taasisi ya Utafiti wa Afya, anasema: “Athari ni ndogo, lakini kuvuga umma mkubwa, athari kama hiyo inakuwa na maana kubwa katika tafsiri ya afya ya umma.”

Aidha, Mkurugenzi wa Kituo cha Maradhi ya Kumbukumbu, katika Chuo Kikuu cha Nottingham, Profesa Tom Dening, naye anakiri kuvutiwa sana na matokeo ya utafiti huo.

“Inaaminika uchafuzi wa hewa kutoka kwenye magari inaweza kuchangia katika asili ya ubongo na baada ya muda inaweza kuongeza hatari ya kupoteza uwezo wa kumbukumbu.”

Kwa mujibu wa Profesa Dening, huo ni ushahidi unaochangia kuwaondoa watu katika maeneo ya barabara kubwa.

"Iko bayana kwamba kuishi katika mazingira ambayo kuna uchafuzi mkubwa wa hewa, ni mbaya na vigumu kumwambia yeyote kuwa pazuri," anafafanua msomi huyo.

Hivyo, wasomi hao wanashauri umma kuepukana na mazingira ya namna hiyo yanayowaweka karibu na maradhi kama hayo
BBC

Habari Kubwa