Wanasayansi weusi ‘injini’ ya uchunguzi wa safari za anga za juu

17Jan 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wanasayansi weusi ‘injini’ ya uchunguzi wa safari za anga za juu

1.Robert Shurney (1921-2007)
Dk Robert Shurney alikuwa mwanafizikia kutoka Chuo Kikuu cha Tennessee State. Alifanya kazi kama mhandisi wa safari za anga za juu- , aliyefanya kazi katika kituo cha uchunguzi wa anga za juu nchini Marekani (NASA).

Kama Marshall Space Flight Center , yeye ameyafanyia kazi majukumu kadhaa makubwa na muhimu kwa ajili ya NASA.

Miongoni mwa majukumu hayo ni pamoja na kubuni matairi kwa ajili ya chombo cha kusafiri anga za juu ikiwemo Apollo 15 ambayo iliyofanya safari yake anga za juu mwaka 1972.

Ubunifu wake ulihusisha kuunganisha nyaya maalum zenye matundu kwenye magurudumu katika nafasi ya mpira ili kupunguza uzito, lakini bado ikatoa ufanisi unaohitajika .

2.Christine Darden (1942-)

Christine Darden ameshinda tuzo-naakun katika hesabu na uhandisi wa mitambo mhandisi, ambaye amefanya kazi na NASA tangu mwaka1966 na akatambuliwa kuwa kiongozi katika kupunguza mshtuko wa mawimbi kutoka katika mbawa za chombo kinachosafiri katika anga za juu pamoja na pua ya chombo hicho.

Baada ya kuanza kazi kama mchambuzi wa data wa NASA, Darden alipandishwa cheo na kuwa mhandisi wa anga vyombo vya anga za juu mwaka 1973 kisha akahamia katika nafasi mbalimbali za uongozi. Mwaka 1989, aliteuliwa kuwa kiongozi wa kiufundi wa kundi la NASA - NASA’s Sonic Boom Group of the Vehicle Integration Branch of the High Speed Research Program - ambapo alikuwa akiwajibika kuendeleza mpango wa utafiti wa ndani katika NASA.

Mnamo Oktoba 1994, Darden akapandishwa kuwa naibu meneja mipango wa program ya majaribio ijulikanayo TU-144 ya utafiti wa kasi kubwa katika NASA; na mwaka 1999, aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa Mpango wa Usimamizi Ofisi ya Aerospace Performing Center katika Langley Kituo cha Utafiti ambako aliwajibika katika Kituo cha Utafiti cha Langley akiwa na dhamana ya kusimamia menejiment ya trafiki na masuala mengine ya anga za juu katika vituo vingine vya NASA .

Darden pia aliwahi kuwa mshauri wa kiufundi katika masuala kadhaa ya serikali na miradi binafsi miradi mbalimbali, pia ni mwandishi wa machapisho zaidi ya hamsini katika eneo la ubunifu wa mabawa ya chombo kinachoruka anga za juu katika mtiririko wa kasi kubwa na maeneo mengine muhimu ya kisayansi na kihandisi.

3. Emmett Chappelle (1925-)

Emmett W. Chappelle ni mwanasayansi aliyetoa mchango muhimu katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na dawa, uhisani, sayansi ya chakula na masuala ya kikemia ya anga za juu ( astrochemistry).

Mwaka 1958, Chappelle alijiunga Taasisi ya Utafiti wa Mafunzo ya Juu ambapo aligundua chembechembe za mimea inaweza kubadilishwa kutoka hewa ukaa kuwa oksijeni.

Ugunduzi huo ulisaidia kutengeneza ugavi wa oksijeni salama kwa wanaanga. Mwaka 1966, alijiunga na NASA ambapo utafiti wake ulilenga bioluminescence, ambayo ni mwanga bila joto.

Aligundua mbinu ambazo zinaendelea kuchunguza bakteria katika maji na kutumika kwa ajili ya kugundua bakteria katika mkojo, damu, maji maji ya uti wa mgongo, maji ya kunywa na vyakula.

Chappelle amekuwa akiheshimiwa kuwa miongoni mwa watu 100 wanaotambulika kuwa wanasayansi wenye hadhi ya juu sana wenye asili ya Afrika(African-American ) katika karne ya 20.

Alijumuishwa katika orodha ya wavumbuzi -the National Inventors Hall of Fame mwaka 2007, kutokana na ugunduzi wake wa mchanganyiko mnamo Januari 21, 1969, ambaye alipata moja ya hakimiliki zake 14.

4.Patricia Cowings (1948-)

Dk Patricia Cowings ni mwanasaikolojia ambaye amekuwa akifanya utafiti ndege zinazoruka katika anga za juu kwa NASA.Alikuwa mwanamke wa kwanza katika Amerika kupewa mafunzo kama mwanasayansi wa anga za juu. Ingawa hakuwahi kwenda kwenye anga za juu , ametumia miaka 34 ya kazi zake katika NASA na kuchangia kufanya mazingira bora kwa waliofanya hapo.

Cowings aliwasaidia vyema wanaanga bora kukabiliana na masomo ya anga na madhara ya mvuto wa fiziolojia ya binadamu na utendaji.

Alikuwa mtu muhimu katika kuendeleza na hati miliki,mrejesho wa mafunzo, matibabu kwa ugonjwa unaotokana na mwendo kasi angani na maumivu ya kichwa.

5.Shelby Jacobs (1935-)

Shelby Jacobs alikuwa mhandisi wa mitambo, ambaye alifanya kazi katika program ya kuhamisha chombo cha Apollo katika anga za juu .

Miradi hiyo ni pamoja na Apollo-Soyuz orbiter space shuttle ambaye alikuwa meneja wa mradi, bado anachukuliwa kuwa moja ya mafanikio ya uhandisi wa ajabu zaidi katika historia ya binadamu .

Jacobs baadaye aliendelea na kubuni mifumo mbalimbali , ambayo ni pamoja na mfumo wa uhamisho wa kamera mwaka 1965.

Anafahamika vyema kwa jukumu lake katika kubuni, ufungaji na upimaji wa mfumo wa kamera, ambayo ilifungwa kikamilifu katika Apollo 6 Aprili 1968.

Mfumo wa video inayojitenga kati ya hatua ya kwanza na ya pili ya kuhamisha ni moja ya picha zaidi ambazo zimekuwa zikijirudia mara kwa mara katika historia ya anga za juu.

6.Dk. Vance Marchbanks (1905-1973)

Dk. Vance Marchbanks alikuwa daktari wa upasuaji wa moyo na mtaalamu wa matibabu kwa NASA. Katika muda wake pale, Vance alisaidia kuendeleza njia za kufuatilia ishara muhimu kwa wanaanga wakati ndani ya ndege angani . Alikuwa ni Vance aliyekuwa akiwajibika kwa afya ya John Glenn wakati wa ziara ya kwanza ya chombo ya Amerika kwenda anga hizo .

7.George Carruthers (1939-)

Dk. George Carruthers alikuwa mhandisi wa vyombo vya anga za juu, aliyejenga mifumo wa kamera kwa NASA kwamba zinazalishwa baadhi ya picha za kudumu zaidi kutoka angani. Carruthers aliwajibika kuendeleza kamera za masafa marefu ultraviolet camera / spectrograph kwa mwaka 1972 katika Apollo 16 , iliyotumika kujengwa kwanza na uchunguzi wa mwezini

Mwaka 1970, kwa kutumia roketi ya sauti , Carruthers alifanya ugunduzi wa kwanza wa molekula ya hidrojeni katika anga. Pia aliendeleza mfumo wa zana za roketi na vifaa vyenye kamera mbili vikiwa na uwezo mkubwa sana wa kunasa picha iliyotumika katika chombo cha the STS-39 space shuttle mission mwaka 1991.

*Imetafsiriwa na Jackson Kalindimya toka mtandao wa atlantablackstar.com

Habari Kubwa