Wasiofurahia matiti yao wazito kubaini kansa

11Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wasiofurahia matiti yao wazito kubaini kansa

KANSA ya ziwa ni tatizo kubwa kwa kinamama. Lakini je, inakabiliwaje? Hapo ndipo kwenye tatizo katika namna ya kupigana vita hivyo.

Sasa watafiti wamekuja na mapya walioyagundua, kwamba kinamama wasioridhiki na kiwango cha urembo wa matiti yao, ni mara chache sana wanachukua muda kuchunguza kiwango chake au uwepo wa walakini wowote.

Katika ripoti iliyochapishwa katika Jarida la Afya linalohusika na afya ya kinamama, ambayo inatokana na kinamama Waingereza 384, waligundulika kuwa wavivu na wenye uwezo mdogo kugundua kasoro kwenye matiti yao.

Inaelezwa na watafiti kuwa inapotokea hoja ya kuchunguza matiti kwa kinamama hao, vikwazo vya ‘hapa na pale’ vinajitokeza kama vile aibu au kujisikia kukerekana tendo hilo.

Katika ripoti hiyo ya utafiti, asilimia 31 ya kinamama ambao hawakufurahia tendo hilo walionyesha haja ya kuwa na matiti madogo, wakati wana makubwa.

Pia, kuna wengine asilimia 44 wenye matiti madogo walionyesha hisia ya kupenda kuwa na matiti makubwa.

Inaelezwa nchini Uingereza, kila mwaka wanagunduliwa wagonjwa wapya 55,000 wa kansa ya matiti, ingawaje katika sura ya pili wanaelezwa kuwa ni mmoja kati ya 10, ndiye anayochukua hatua ya kwenda kumuona daktari mara moja kwa ajili ya matibabu.

Umma unahimizwa kwamba, kukagua matiti mapema ni njia mojawapo bora ya kudhibiti kansa.

Mtaaluma Profesa Viren Swami, kutoka Chuo Kikuu cha Anglia Ruskin, ambaye alishiriki utafiti huo, anasema kinamama ambao hawajaridhika na ukubwa wa matiti yao, kujidhibiti kisaikolojia.

Uangalizi wa karibu zaidi wa matiti binafsi ya kinamama, inaelezwa inawasaidia kubaini mara moja kugundua kasoro za kiafya.

Mtaalamu Dany Bell kutoka asasi ya Kansa ya Macmillan:"Kutokufurahia jambo kuhusu mwili wao, kusiwazuie watu kujikagua.

"Uvimbe ni ishara iliyozoeleka sana ya kansa ya zuwa, hivyo kukagua kila mara maana yake ni kuigundua mapema," anasema Bell na kuongeza ni muhimu kwa wanaume na kimama kwa pamoja kujenga kawaida ya kujikagua.

Mtafiti Sophia Lowes, kutoka Asasi ya Utafiti wa Kansa Uingereza, anasema katika utafiti wao hawakujumuisha vigezo kama vile mambo mengine ya kijamii yanayoleta mabadiliko katika ziwa la mwanamke.

Mwanamke huyo mtafiti anawasisitiza kinamama wenzake kuwa makini kufuatilia matiti yao kwa karibu, hata kuwa wepesi kugundu mabadiliko yoyote yanayowatokea.

"Kama unagundua kisicho cha kawaida, mfahamishe daktari wako," anasema Bell na kuongeza:” Mara nyingi si kansa, lakini kama yenyewe, kuigundua mapema kuna tofauti kubwa.”

 

 

Habari Kubwa