Wataalamu viwango, chakula dawa wajibu swali gumu ulaji ‘aspartame’

24Nov 2020
Gaudensia Mngumi
Dar es Salaam
Nipashe
Wataalamu viwango, chakula dawa wajibu swali gumu ulaji ‘aspartame’

DUNIA ya sasa imejaa bidhaa zenye sukari au utamu bandia ambao huitwa aspartame. Hii ni bidhaa yenye utamu mara 200 ikilinganishwa na sukari hasa ya miwa.

Sukari yenye utamu bandia ‘aspartame’ inayotumiwa kutengeneza vyakula na vinywaji vya aina mbalimbali inaelezwa kuwa si salama kiafya. PICHA:MTANDAO

Aspartame hutumiwa kuongeza utamu kwenye vyakula mfano viwandani inatumika kuzalisha vyakula hasa pipi, keki, chokleti na vinywaji kuanzia soda na juisi.

Ina majina mengine, wapo wazalishaji wanaoiita NutraSweet, Equal na Canderel. Sukari hiyo inaelezwa kuwa ina athari nyingi kiafya ikihusishwa na kansa, magonjwa ya moyo, ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu na kusahau ( alzheimer), mishtuko ya moyo, kiharusi na matatizo ya akili na kuumwa sana kichwa.

Aspartame ambayo ni bidhaa ya utamu bandia inayotumika duniani kote inapatikana katika bidhaa zaidi ya 6,000 ikiwa ni pamoja na soda zinaelezwa kuwa hazina sukari (diet) vinywaji vya kuongeza nguvu au ‘eneji ‘.

Inazalisha pipi ngumu na laini zisizo na sukari (ya miwa); lakini imo kwenye tomato sosi ‘ketchup’, kwenye dawa za watoto, za vitamini na za matone.

Dunia imeshuhudia miongo kadhaa kuhusu wasiwasi wa aspartame ambayo imekuwapo na hadi leo wasomi wanaendelea kuizungumzia na ikumbukwe kuwa aspartame iliidhinishwa kwa mara ya kwanza mnamo 1974.

Hata hivyo licha ya kutumia miaka 50 sasa wanasayansi wa Marekani na wengine huru wameibua wasiwasi juu ya athari za kiafya na upungufu katika sukari hiyo.

Kuanzia mwaka 1987 taarifa za uchunguzi zilichapishwa zikiripoti kuhusu wasiwasi huo na changamoto za aspartame kiafya na uduni wa utafiti uliosababisha kuipa idhini ya kuitumia kama chakula cha binadamu.

Kunaripotiwa kuwa katika tathmini ya Mamlaka ya Usalama wa Chakula Ulaya, ilipendekezwa mtengenezaji maarufu wa sukari hiyo bandia duniani apigwe marufuku.

Wataalamu wa usalama wa chakula wanataka sukari hiyo yenye utamu wa bandia inayotumiwa sana duniani au aspartame kupigwa marufuku nchini Uingereza na kuhojiwa kwanini ilionekana kuwa inakubalika hapo awali.

Taarifa za Jarida la Chakula za Novemba 2020, zinasema uuzaji wa aspartame unapaswa kusimamishwa kwani ni kemikali inayotuhumiwa kutokana na utamu na imependelewa bila kufanyiwa tathmini ya usalama.

Athari za kiafya na mambo muhimu kwenye aspartame zinasema kuwa ingawa utafiti mwingine kati nyingine hazijaripoti matatizo yaliyoko kwenye aspartame utafiti uliofanywa na watafiti wa kujitegemea uliofanywa kwa miongo kadhaa umeunganisha aspartame na orodha ndefu ya bidhaa zenye changamoto za kiafya zikiitaja saratani.

Katika utafiti kamili wa saratani hadi sasa kwenye jina la aspartame, utafiti uliofanywa na Kituo cha Utafiti wa Saratani ya Cesare Maltoni cha Taasisi ya Ramazzini, ulitoa ushahidi madhubuti kuwa ilisababisha saratani katika panya.

Utafiti unasema aspartame ni chanzo cha magonjwa hasa saratani kwa viumbe hai hata kama italiwa kwa kipimo cha kila siku cha kiwango kidogo kuliko ulaji unaokubalika kwa siku
Ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa panya mwaka 2006, kwa mujibu wa jarida la utafiti ulioangalia afya na mazingira. Utafiti mwingine wa ufuatiliaji uliofanyika mwaka 2007 uligundua kuongezeka kwa kiwango cha juu cha tumors mbaya (vivimbe vyenye saratani) katika panya wengine.

"Matokeo yanathibitisha na kuimarisha uchunguzi wa kwanza wa majaribio ya [kansa ya aspartame] na uwezekano wa kusababisha saratani katika kiwango cha kipimo karibu na ulaji unaokubalika wa kila siku kwa wanadamu.

Habari Kubwa