Wavumbuzi vijana waibuka na teknolojia ya kufyeka majani

20Dec 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wavumbuzi vijana waibuka na teknolojia ya kufyeka majani

Emma Masibo na Lucy Bwire wana mambo mengi yanayofanana.Wote ni wanafunzi wa uhandisi wa mitambo wakiwa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Ufundi ya Sang'alo ,kaunti ya Bungoma , Magharibi ya Kenya.

Kama hiyo haitoshi, vijana hao wote wana umri wa miaka 23 na 24, kwa mtiririko huo.

Zaidi ya hayo, wote hao wawili wana ndoto zinazofanana zinazotafsiri maono yao katika hali ya urafiki wa ujasiriamali . Kwa pamoja sasa, wavumbua kifaa nafuu kiuendeshaji kinachotumika kufyekea majani kinachotumia nishati ya jua.

Kwa mujibu wa Masibo, wanafunzi`hao kabla hawajabuni kifaa hicho , walikuwa wanawaangalia wafanyakazi wa karakana ya chuoni kwao walivyokuwa wanaifanyia matengenezo mashine ndogo ya kukatia nyasi katika maeneo ya wazi karibu na shule.

Mashine hiyo ilikuwa inatumia inatumia injini -powered lawn mowers –ambayo inapotumika ilikuwa inapiga kelele hata kuwa kero wakati wakiwa darasani wanajifunza.

Ilikuwa inakera, kuvuruga mwenendo wao wa kujifunza pia kuongeza gharama za mafuta kwa ajili ya uendeshaji wake ambayo shule ilipaswa kugharamia kwa mwaka mzima.

Mazinghira hayo ndiyo yakawafanya waamue kwamba, kuna kitu fulani kinatakiwa kufanyika ili kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda sawa.

Ndipo wakaamua kuketi na kufikiri kwa pamoja, kubuni na kujenga mfumo mpya (Prototype) ambao sasa baada ya majaribio kadhaa unatumika shuleni .Gharama walizotumia ni sh 324,000 ( dola 180). Hii ni robo ya gharama ikilinganishwa na kifaa cha awali (mowers).

Mtambo huo, unaweza kuchajiwa kwa kutumia umeme na kuhifadhi nishati hata kuwezesha ufyekaji wa manyasi kufanyika hata majira ya usiku kama hakuna mwanga wa jua.

Ili kuweza kufanikisha mtambo huo mdogo kufanya kazi majira ya usiku , zimefungwa taa maalum zinazotumia mwanga wa jua (solar) .

Mtambo huo hufanya kazi usiku au katika mwanga hafifu wa hali ya kitropiki kama ilivyo katika sehemu nyingi za Kenya.

"Kutokana na mtazamo wa kijinsia, mitambo ya jadi iliyokuwa ikitumika - ama kwa kubuni au namna nyingine - zimeonekana kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya wanaume.

Ni vigumu kuiwasha kwa sababu inapiga kelele na kutoa harufu ya mafuta hata kuwakera wanawake. Lakini hii iliyotengenezwa sasa inayotumia nishati ya jua ni rafiki kwa wanawake. Ni rahisi kuiwasha, ni kiasi cha kutumia swichi moja tu kisha unatumbukiza gia ili kuuwasha mtambo huo , " anasema Masibo.

Kwa mujibu wa Bwire, ilikuwa rahisi kwao kutengeneza mashine hiyo ndogo kwa kutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira yao.

Taasisi iliwafadhili kwa kuwanunulia vifaa kama solar panel, detector kwa ajili ya matumizi ya ufanisi wa mashine hiyo pamoja na betri maalum.

Peter Wamalwa, ambaye ni mhadhiri na mshauri wao wa kiufundi, aliusifu sana ubunifu wa vijana hao wanawake. " Walitafuta ufumbuzi wa tatizo kwamba ajili ya jamii yetu imekuwa na mtazamo chanya sio kwa ajili ya jinsia ya kiume tu.

Kwa hiyo, katika mazingira kama haya wanapofanikisha suala kama hili, hiyo inaonyesha kwamba, uwezo wao wa ubunifu ni imara, " alisema.

Alisema mashine hiyo ina viwango, hivyo wateja wanaweza kutumia kulingana na vitengo vya mahitaji yao. Aliongeza kwamba, mashine hiyo haihitaji ujuzi mkubwa ili kuitumia na kuifanya kuwa endelevu.

Yaweza kutumika hata kusafisha sakafu, hivyo kugeuzwa kwa ajili ya kusafisha uchafu katika mazingira ambayo kaya nyingi nchini Kenya zinaweza kumudu.

"Katika nchi hii peke yake, hebu fikiria namna mashine hizo zinazotumia mafuta zinavyotumika na athari za uzalishaji wao wa hewa chafu kwa mazingira.

Kuja kufikiria nini kitatokea kama kaya nyingi na taasisi kama hospitali na shule zinazotumia mashine inayotumia nishati ya jua (mowers lawn) katika suala la faida kwa mazingira na kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingetumika kitakachookolewa , " Wamalwa anasema.

Kwa mujibu wa Wamalwa, taasisi sasa inatarajia kuwasaidia wanafunzi kibiashara ili kufanikisha uvumbuzi wao. " Katika miaka miwili ijayo tunataka kuzihakikisha taasisi zote kujifunza kupata mashine (mower) ya nishati ya jua," alisema.

Masibo anasema, wao tayari wameboresha mpango wa kuendeleza mashine (mower) kwamba ni katika mfumo wa kiti cha gurudumu, na kukifanya kuwa bora kwa watu wenye ulemavu.

Maoni ya Wamalwa yanaungwa mkono na Fred Matiang'i, wa Kenya ambaye ni katibu wa sekta ya elimu , sayansi na teknolojia , aliyekuwa akiongozwa na kile alichokiita kiwango cha juu cha ubunifu wa wanawake wawili vijana.

Katibu wa baraza la mawaziri, aliyefungua maonyesho hayo ya siku tano ya Taifa ya Sayansi mjini Nairobi hivi karibuni alisema, wakati alipotembelea Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Sang’alo ambao walikuwa wakionyesha vifaa vya ubunifu kuwa, wizara yake itakuwa kiungo kwa wabunifu, sambamba na sekta na wavumbuzi vijana ili kuhakikisha unakuwapo uzalishaji mkubwa katika vitengo.mbalimbali

"Hii ni teknolojia kwa vitendo kwamba inatatua changamoto moja au zaidi inayoikabili nchi hii ," alisema Matiang'i, na kuongeza "Natumaini itapatiwa hakimiliki ili kuepuka ukiukwaji wa hakimiliki."

Wiki hiyo ya sayansi iliwavutia waonyeshaji zaidi ya 100. Washiriki ni pamoja na watunga sera, wasomi, wanataaluma, wanasayansi, wanafunzi, wajasiriamali na wengineo kutoka taasisi za kitaifa na kikanda kama vile vyuo vikuu, taasisi za utafiti, ufundi stadi, ufundi na taasisi za mafunzo ya ujasiriamali, mashirika ya kimataifa na wadau wa maendeleo.

Lakini Masibo na Bwire sio vijana pekee waliolenga kutumia nishati ya jua kudhihirisha uvumbuzi wao.Wanafunzi wengineo wa chuo kikuu cha Kenya Josephat Ngetich ,21 na Cosmas Mibei ,20 ambao wanajifunza ngazi za astashada katika masomo ya sayansi , Chuo cha marafiki cha Kaimosi ,Kaunti ya Vihiga, magharibi ya Kenya ambao wametengeneza mtambo mwingine wa jiko utumiao nguvu za jua “multi solar cooker.”

NB:Makala kwa hisani ya IPS

Habari Kubwa