Wenye mji wao Mpanda walivyoteketeza vichaka ‘makao makuu’

24Nov 2022
Neema Hussein
MPANDA
Nipashe
Wenye mji wao Mpanda walivyoteketeza vichaka ‘makao makuu’
  • magenge uhalifu Makaburini, stesheni kazi kupita ‘usiku, mchana’

 

Hapo kuna simulizi kutoka kwa Juvenary Deus, Mwenyekiti wa Mtaa wa Msasani, mjini Mpanda, anayetoa ushuhuda kwa Nipashe, mtaa wake ulikuwa moja ya maeneo yalikofanyika maasi ‘mchana kweupe’, hadi katika maeneo yenye mapori makubwa.

Makaburi ya Mwangaza, katika Mtaa wa Mpadeko, mjini Mpanda katika hali mpya baada ya kusafishwa. Awali palikuwa na majani kimo zaidi ya mita mbili, wahalifu wakitumia kukaba watu na kuhifadhi nyenzo zao.

 

Hapo kuna simulizi kutoka kwa Juvenary Deus, Mwenyekiti wa Mtaa wa Msasani, mjini Mpanda, anayetoa ushuhuda kwa Nipashe, mtaa wake ulikuwa moja ya maeneo yalikofanyika maasi ‘mchana kweupe’, hadi katika maeneo yenye mapori makubwa.

Ni mazingira yaliyotumika kuwa kificho cha makundi ya kihalifu na eneo mojawapo panatajwa ni makaburi ya Mwangaza, katika Mtaa wa Mpadeko. kata ya Makanyagio.

Eneo hilo kipindi cha nyuma lilikuwa tishio kwa wakazi husika, kutokana na kuzungukwa na nyasi ndefu na ikawa sababu ya kutumika kama kificho cha wahalifu na silaha zao.

Ni jambo lililochukua nafasi kubwa, hata serikali ngazi ya mkoa nayo kuingilia kati kukabili makundi hayo ya uhalifu, hali kadhalika kusafisha maficho.

Kwa mujibu wa taarifa ya kimkoa, eneo jingine lililokuwa pori jirani na stesheni ya treni, nako vijana wahalifu wakapatumia kudhuru abiria.

Baada ya serikali kugundua maeneo hayo hatari kwa maisha ya watu, ikaweka jicho hata kufikia hatua kujadili katika vikao mbalimbali na ndio mwarobaini wa uhalifu kutoka mapori ya mjini Mpanda, kufikia mwisho.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpadeko, Kata ya Makanyagio, Ivo Chambala, anaeleza kwamba wakati anaingia madarakani mwaka 2019, kulikuwapo makundi ya kihalifu, akiwa na ufafanuzi wake kuwa:

"Sasa katika vikao vyetu tulikuwa tunajua kabisa hilo eneo la makaburi ya Mwangaza ni eneo hatarishi hasa, tukiliacha likiwa chafu, kwa sababu vitendo vyote vya kihalifu vilikuwa katika hilo chaka linalowahifadhi wavuta bangi.

“Hata mali za wizi zilikuwa zikifichwa katika hayo makaburi. Kupitia vikao vya kiserikali tulivyokua tukivifanya, ikaonekana pale tufanye kila namna kwa juhudi hata kuomba msaada katika taasisi yeyote serikalini au nje ya serikali, tuweze kusaidiana kuweza kuondoa vichaka ili kuepusha masuala ya uhalifu, ikiwemo uvutaji bangi na ubakaji.

"Nakiri eneo hilo halikuwa sehemu salama, kinamama wengi wamedhalilishwa, wamebakwa pia hata watoto wadogo vilevile, hata kuporwa wameporwa sana katika eneo hilo.

“Mpaka hivi sasa tunawahimiza wananchi, pindi tutakapokuwa hatuna uwezo wa kutumia nguvu ya kusafisha eneo hilo, tutakapokuwa tumewahitaji kuwaomba msaada basi tusaidiane wote kwa pamoja.

“Sababu eneo hilo kwanza ni hatarishi, endapo tutakuwa tunaliacha bila kufanya usafi, pili ni lazima tuheshimu sababu ndio safari yetu ya mwisho, baada ya kumaliza maisha ya hapa duniani," anasema Chambala

Anakumbusha mikasa kadhaa, ikiwamo mwendesha bodaboda kutekwa na kupelekwa makaburini walikomnyang'anya vifaa vyake. Pia, kuna lingine binti naye akabakwa katika eneo hilo, hali kadhalika makaburi kufukuliwa kutafuta mali.

"Tukio jingine ambalo sio rasmi, labda kipindi ambacho tunafanya usafi tulikuja kugundua, vilevile eneo hilo lilikuwa kama maficho ya silaha za jadi mapanga,visu vilikuwa vinahifadhiwa pale usiku, baada ya watu kumaliza shughuli zao mtaani," anaeleza Chambala.

USAFI  UNAVYOFANYIKA

Chambala anasema, eneo hilo linasafishwa na wanaohusika, wakazi wote wa mitaa inayolizunguka, pia wakihusisha Manispaa ya Mpanda, kwani ni eneo la maziko ya jumla kwa jamii ya mahali hapo, hivyo wakawahusisha waumini aina zote.

"Mwitikio unakuwa bado ni mdogo, suala la machaka bado linaendelea, ila kupitia uongozi wa serikali kuna mfadhili aliyekuwa amejitolea kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza na uongozi wa Kata ya Makanyagio, kupitia diwani wetu, wenyeviti na watendaji wa kata.

“Huyo mfadhili alikubali kulipa angalau gharama kidogo, ili kuweza kuwatumia wafungwa kusafisha eneo hilo na kuondoa kero na adha iliyokuwa ikitukuta," anaeleza Chambala.

"Kwa ushirikiano wa pamoja, tulikuja kungundua pia ni sehemu ya vijana wengi ambao wapo majengo na kituo chao inakuwa Shule ya Sekondari Mwangaza.

“Ndio ilikuwa kituo wanachokutana mara kwa mara, ukiwaona ni kama wamekwenda kwenye mazoezi ya mpira, kumbe wanakuwa ukingoni mwa makaburi kwa ajili ya kupanga mipango yao ya kihalifu,” anasema.

"Katika vikao vyetu tulikuwa tunajua kabisa, hilo eneo la makaburi ya Mwangaza ni hatarishi, hasa tukiliacha likiwa chafu, sababu vitendo vyote vya kihalifu lilikuwa hilohilo chaka linawahifadhi wavuta bangi, hata mali za wizi zilikuwa zikifichwa katika hayo makaburi.

"Kupitia vikao vya kiserikali tulivyokuwa tukivifanya ikaonekana pale tufanye kila namna juhudi hata kwa kuomba msaada katika taasisi yoyote serikalini au nje ya serikali, tuweze kusaidiana kuweza kuondoa vichaka ili kuepusha maswala ya uhalifu ikiwemo uvutaji bangi na ubakaji.

"Kwa hiyo, mpaka hivi sasa tunawahimiza wananchi pindi tutakapokuwa hatuna uwezo wakuweza kutumia nguvu ya kusafisha eneo hilo tutakapokua tumewahitaji kuwaomba msaada basi tusaidiane wote kwa pamoja.

“Eneo hilo kwanza ni hatarishi, endapo tutakuwa tunalicha bila ya kufanya usafi, pili ni lazima tuheshimu sababu ndio safari yetu ya mwisho baada ya kumaliza maisha ya hapa duniani," anafafanua Chambala,

kuhusu vichaka vya makaburini.

Anasema eneo hilo wanaohusika kufanya usafi ni wakazi wa mitaa inayolizunguka, pia katika vikao vyao wanaihusisha na Manispaa ya Mpanda, kwa sababu maziko yanayofanywa hapo ni kwa karibu wakazi wote, hivyo hata viongozi wa dini wanahimizwa kuwahusisha waumini usafi wake.

Pia, anasema kuna mwitikio mdogo na hadi sasa kupitia uongozi wa serikali kuna mfadhili aliyejitolea kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza linalotumia wafungwa pamoja na uongozi wa Kata ya Makanyagio, kupitia diwani wenyeviti na watendaji wanasafisha eneo hilo na kuondoa kero ya vichaka.

Juvenary Deus ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Msasani, anaisimulia Nipashe kuwa:"Mwaka jana, hili eneo ndio lilikuwa linaongoza kwa ukabaji, unakuta labda msafiri zile siku za treni anakuwa hana hata fedha tu ya kusema alipe aingie uwani na wazo la kuomba kwa mtu hana.”

Anaendelea: “Basi anaamua kuingia kwenye kichaka ili watu wasimuone, kumbe wale mabwana ndio wanakuwa kule, basi ndio wanakabwa kwa mtindo huo.”

 

Pia, anasimulia mbinu nyingine ya wahalifu hao wanaoazima mavazi ya askari mgambo kutisha wapita njia, eneo hilo la stesheni, akifafanua: “Wanamuonyesha hicho kitambulisho na yeye anakubali, anawafuata, akifika huko anawakuta na wengine kwenye kichaka ndio wanamkaba sasa hizo ndio zilikua mbinu zao.”

 

 

 

 

 

 

 

Top of Form

Bottom of Form

Habari Kubwa