Yajue maumivu ya mguu,janga la kidonda cha kisukari

21Apr 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Yajue maumivu ya mguu,janga la kidonda cha kisukari

Ni jambo la kawaida kwamba watu wengi wanaougua kisukari, wanahaha kusaka tiba ya maradhi hayo kupitia mfumo rasmi na usio rasmi katika matibabu.

Moja ya athari za maradhi hayo, inajtokeza kupitia maumivu makali miguuni.

Kisukari kinaelezwa kuwa na sababu nyingi za chanzo chake inayoishia katika maumivu makali. Kubwa zaidi ni zinazohusishwa na mishipa ya mwili na hasa katika maeneo yanayoathiriwa na kuwepo sukari nyingi, ikiwemo mishipa midogo na inayobeba hisia za mwili.

Inaelezwa kwamba, sehemu kubwa ya wagonjwa, maumivu yao yanawaguswa katika eneo hilo.

Kuna baadhi ya watu wanaguswa hata wanapoguswa ngozi zao au hata mwili kugusa shuka la kulalia, inatosha kumsababishia maumivu makali.

Pia, mwili ukiathirika kwa namna yoyote ile, nayo inaangukia katika maumivu makali

Ili kukabiliana nayo, hatua ya kwanza ya mgonjwa anayopaswa kujiwahi dhidi ya maumivu hayo, ni kuangalia kiwango chake cha sukari kwenye damu na kuchukua hatua za matibabu. Maumivu makali yanaendana na kiwango cha sukari kilichopo mwilini.

Pia,kuna hatua nyingine ya kutibu kwa kusugua sehemu zenye maumivu na krimu maalumu au kufunga bandeji maalumu katika sehemu inayouma na kula vidonge.

Kuna wakati mwingine inapobidi, mgonjwa anavaa viatu na soksi maalumu zinazowasaidia wenye matatizo ya namna hiyo.

Mishipa inapoathiriwa na sukari, maumivu huanzia kutokana na hali misuli kulegea na baadhi ya mishipa kuwa katika mpangilio ambao si sawa.

Mara nyingi maumivu yanavyojitokeza ni kupitia mzunguko mdogo wa damu miguuni na kusababisha maumivu ya ndani. Kuna mafuta maalumu yanayotibu.

Mtu anayeathiriwa na kisukari miguuni, huvimba miguu, kutokwa jasho na kuwa ngozi kavu.

Kutokana na uwepo wa sukari nyingi mwilini, balaa la pili linaloanza kumuandama mgonjwa ni la kushambuliwa na bakteria. Hiyo inazaa maumivu ya ziada.

Nishipa mikubwa na midogo ya damu, husafsishwa na oksijeni kutoka kwenye moyo, ikisafiri na damu na kuitakatisha mishipa hiyo.

Kuwepo mafuta kunapunguza nafasi ya damu, baada ya kuwepo ongezeko la mafuta ambayo huleta shida mzunguko wa damu, mazingira yanayojengwa na ongezeko la sukari kwenye damu.

Kuwepo mafuta kwenye kingo za mishipa ya damu, husababisha ziada ya madini aina ya calciums, jambo linaloathiri mzunguko wa damu.

Ni hali inayomaanisha kupunguza kiasi cha oksijeni na lishe ambayo mishipa hiyo inapaswa kuipata. Hapo ndipo maumivu makali yanapoanza.

Mishipa huvimba na kuumia zaidi na sababu kuu ni kwamba inashindwa kuhimili kasi ya mzunguko wa damu ambazo zinatafuta njia mbadala katika mshipa midogo, bila ya mafanikio.

Wakati mwingine damu inapojaa katika mishipa midogo, inashindwa kuimudu na kuishia kupasuka.

Kuna tiba inayopendekezwa, ambayo ni mazoezi ya mwili na matibabu mengine rasmi kupunguza msukumo wa mzunguko wa damu.

Maumivu makali ya msuli na viungo vya mwili, yanasababishwa na kukakamaa mishipa.

Sababu kuu ni kutokuwepo msukumo na mzungukio sahihi wa damu katika sehemu hizo, hali inayosababishwa na kisukari.

Hiyo inamfanya muathirika kutokuwa na mfumo mzuri wa kutembea. Viungo vinakamaa kunatokana na kuwepo protini na sukari katika maungo ya mwili.

Pia, hali hiyo huwakabili watu wasio na matatizo ya kisukari.

Mtu mwenye sukari nyingi mwilini, anakabiliwa na tatizo la kuathiriwa na bakteria na dalili za mtu kuathirika ni kwamba inavimba, ya moto, yenye uchovu na kuwashwa kila mara.

Kuna wakati inafikia hatua mbaya ya kuingia kwenye mishipa au kusamba au kwenye ngozi ya mwili.

Inaelezwa kwa ujumla, mateso yatokanayo na kisukari, hatua zote matubau ni ya dharura, ila njia bora ya kukabliana na matatizo hayo ni kudhibiti sukari mwilini.

Hizo ni hatuan zinazoendana na mginjwa kusimamia afya yake kwa karibu, kupeuka athari kama vile kuathiri ngozi na mwili kwa jumla, dhidi ya kuchomwa na vitu kama vile sindano na msumari au mwili kuathiriwa na fangasi.

Pia mwili kutunzwa na matumizi ya mafuta kama vile miti ya chai na ufuta na matunda ya zabibu.

KIDONDA CHA KISUKARI

Mtaalamu wa tiba aliyebobea katika ugonjwa wa kisukari, Dk. Daniel Cohen katika kazi yake ya kitafiti, ana maoni kuhusu balaa la kisukari kwa afya ya mwanadamu.

Anasema iwapo mtu mwenye kisukari anapatwa hata na jeraha dogo, ikiwemo la vipele vya ndevu anapaswa kuwa makini katika namna ya kuisimamia

Dk. Cohen anatahadharisha kuwa mwenye kisukari anahitaji umakini, ikiwemo namna anavyofunga kamba za viatu vyake visimbane na inapotokea maumivu hata cha kidole au sehemu nyingine, awahi haraka kutafuta tiba kwa daktari.

Uelewa binafsi wa kusimamia hata jeraha dogo, ni silaha nyingine anayopaswa kuwa nayo katika kupambana na athari za kisukari dhidi ya jeraha na namna ya kuipatia matibabu sahihi.

KIDONDA CHA KISUKARI

Katika hali ya kawaida, kisukari ni ugonjwa sugu unaoendana na mazingira kwamba mwili wako hauna uwezo wa kutumia sukari inayoingia mwilini kwa mpangilio sahihi.

Athari mojawapo ya hali hiyo, ndio hiyo ya jeraha kushindwa kupona kwa wakati na kuna wakati mwili kupata ganzi ya mishipa kushindwa kutoa hisia za maumivu.

Inapofika hatua mishipa imeathirika, hali inakuwa mbaya kwa muathirika anaweza kukatwa na kitu cha ncha kali na asisikie maumivu. Hilo lina kawaida ya kuzaa athari kwa mtu pasipo kujitambua.

Kwa ujumla, ni jambo linalojenga mazoea ya mfumo wa kinga kupungua uwezo na kukaribisha athari nyinginezo.

Watu wenye mishipa midogo na imezibika kutokana na uchafu, hali inayojitokeza sana kwa wenye kisukari, wako hatarini kupata majeraha ambayo ni ngumu kupona.

Hiyo inatokana na mzunguko wa damu ambao ni muhimu sana katika tiba ya jeraha, haifiki inavyotakiwa kwenye jeraha lilipo, kutokana na uwezo mdogo wa mishipa kusafirisha damu.

TIBA YAKE

Hatua ya kwanza ya tiba kwa kidonda cha kisikari, isimamiwe kwa umakini wa hali ya juu tangu hatua ya kwanza,
kwani ni rahisi kukuzwa na bakteria watakaoishambulia.

Mara inapotokea kidonda, watalaamu wanaeleza kioshwe na maji masafi na wala isitumiker sabuni au spitiri kama vile ‘Iodine’ na ‘Hydrogen Peroxide’ huwasha kwenye kidonda.

Kidonda kinatakiwa kuwekewa ‘antibiotic’ yoyote na kasha kufungwa vizuri na bandeji itakayobadilishwa kila siku, huku akilikagua jeraha kila wakati.

Ni hatua inayoshauriwa kufanyika, huku mgonjwa akiwa na ukaribu mkubwa na daktari wake katika hatua ya kufuatilia matibabu.

Pia, mgonjwa anapaswa kuwa na ulinzi wa karibu dhidi ya maeneo hayo yaliyojeruhiwa, kuepuka kukikuza kidonda.

Habari Kubwa