Ziara ya Waziri Mkuu Zhou Enlai ilikuwa ni historia katika Maendeleo

16Oct 2020
Nipashe
Ziara ya Waziri Mkuu Zhou Enlai ilikuwa ni historia katika Maendeleo

​​​​​​​Ziara ya Waziri Mkuu wa China nchini Tanzania ilikuwa ni historia katika maendeleo ya mahusiano mema kati ya nchi zetu mbili. Miradi kadhaa iliyosaidiwa na Serikali ya China nchini Tanzania ilikuwa tayari imeanza kwa kipindi kile.

Job Lusinde, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania.

Hivyo, urafiki kati ya Tanzania na China ulianza kabla ya Waziri Mkuu Zhou Enlai kutembelea Tanzania. Mtakumbuka kwamba mwaka 1964, jeshi letu liliasi na ilikuwa lazima kulivunja na kuanza kujenga jipya. Serikali ya China ilitupatia vifaa bure vilivyohitajika kulipa nguvu jeshi letu. Zaidi, serikali ya China ilitusaidia kutoa mafunzo kwa jeshi la polisi, na Moshi, walibomoa majengo makuu kuuu ya shule na kujenga mengine zaidi yanayofaa kwa ajili ya Chuo. Ziara ya Zhou haikuwa kuona wanyama na kufurahia vivutio vya utalii. Alikuja kufanya ukaguzi wa kazi iliyokuwa imefanywa kwa msaada wa China, na kujadili masuala yenye maslahi kati ya nchi zetu mbili.

Waziri Mkuu Zhou Enlai alipokelewa na kundi la watu wakiwa na shauku ambayo lilikuwa haijawahi kuonekana Dar es Salaam. Kuna sababu kadhaa, kwanza ilikuwa kwamba, kulikuwa na propaganda nyingi dhidi ya China kutoka kwa nchi za Magharibi ambazo zilitufanya tuwe na huruma kwa China, nchi ambayo pia iliyofanyiwa udhalimu kutoka nje, na ikapigania ukombozi. Pili, watu wa Tanzania walisikia mambo mengi mazuri kuhusu Warizi Mkuu Zhou, hasa kama mmoja wa waasisi wa Sera ya kutofungamana na upande wowote, ambayo ilikuwa msingi wa Sera ya Mambo ya nje ya Tanzania. Na mwisho, ingawa wakati ule hatukuwa tumetengeneza vizuri mawazo yetu ya ujamaa, Misingi ya Chama Cha Tanganyika African National Union (TANU, na Chama tawala cha Tanzania bara wakati ule) zilikuwa na mwelekeo wa ujamaa. Watu walihitaji kumuona kiongozi wa nchi kubwa ya kijamaa ya China.

Niliteuliwa kumsindikiza Waziri Mkuu Zhou Enlai wakati wote wa ziara yake. Ilikuwa ni heshima kubwa kwangu kusafiri naye mahali pote. Nilikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Waziri Mkuu Zhou alikuwa ni mtu rafiki sana. Aliweza, ndani ya muda mfupi, kukufanya uwe na amani na kujisikia uko vizuri katika kuwa nae. Mwalimu Nyerere alikuwa pia na kipaji hicho. Alikuwa muda wote akikufanya kujisikia kuwa na amani. Waziri Mkuu Zhou alituzungumzia kirafiki kuhusu China - kuhusu matatizo na magumu waliyokumbana nayo na namna walivyopanga kukabiliana nayo. Wakati Mwalimu na Waziri Mkuu Zhou wakiwa wanazungumza, walicheka mara nyingi, ungeliweza kuona kwamba, hakika walipendana, na ilikuwa inafurahisha kuwaona.

Waziri Mkuu Zhou alikuwa akifahamika kama msomi na mtu mwenye akili sana. Alifahamu siasa za dunia vizuri sana, na alikuwa na hakika na takwimu katika masuala mengi katika vidole vyake. Alikuwa pia na kumbukumbu nzuri na aliweza kukumbuka pia hata taarifa ndogondogo kuhusu mada zote. Alikuwa pia na uelewa na msimamo wa China katika ulimwengu na aina ipi ya nchi inahitaji kuwa.

Jambo moja muhimu lililochochea uhusiano wetu na China, ilikuwa kwamba, kutoka wakati Tanganyika ilipopata uhuru, ilifuata msimamo wa Jamhuri ya Watu wa China (PRC) kuwa haikutakiwa kuwa nje ya Umoja wa Mataifa, wakati Taiwan ikidai kuiwakilisha China yote. Tanzania kamwe haikusita kuunga mkono kurejeshwa kwa PRC kwenye nafasi yake katika UN. Serikali ya China na viongozi wake walifurashwa na msimamo huu uliochukukiwa kama swala la msingi na hali.

Mijadala kuhsu ujenzi wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ilikuwa ikiendelea wakati huo. Mwalimu Nyerere alikuwa tayari ameshatembelea China na kukutana na Mwenyekiti Mao Zedong na Waziri Mkuu Zhou Enlai. Baada ya Mwalimu kutoa ombi la msaada wa ujenzi wa TAZARA, Mwenyekiti Mao alimuuliza, 'Je reli itasaidia katika ukombozi wa Africa? alijibu, 'Ndiyo, itasaidia', Mwenyekiti Mao alijibu kwa maneno mafupi manne, 'Itajengwa.' Akisema uwepo wa Waziri Mkuu Zhou ulitoa uhakika kuwa itafanyika kama ilivyoahidiwa. Hicho ni kitu kimoja tulichojifunza. Mwenyekiti Mao alichukua maamuzi ya sera na ilikuwa Zhou aliyemuamini kuyatafsiri na kuyatekeleza kikamilifu.

Ziara yake nchini kwetu, ilikuwa, hivyo basi, sababu muhimu na fursa kujadili maeneo yote ya mradi wa TAZARalA.TAZARA ilikuwa ni mradi mkubwa uliotekelezwa na serikali ya China nje ya China. Hata kama kwa juu juu, mradi ulikuwa ni ujenzi wa kawaida wa mradi, kiuhalisia, ilikuwa ni zaidi ya hilo. Ilikuwa ni Kipindi cha Vita Baridi. Kulikuwa na masuala mengi ya kisiasa, uchumi, kijeshi, na ulinzi yanayopaswa kufikiliwa. Kwa namna gani nchi za Magharibi zilizokataa kuunga mkono zingeichukua? kwa namna gani mzigo wa kifedha ungeweza kugawanywa na nchi tatu? kwa namna gani Watanzania wangeweza kutazama uwepo wa wachina maelfu katika nchi yao? Kwa namna gani wafanyakazi Wachina na Tanzania wangeweza kufanya kazi pamoja, na namna gani usalama wa wafanyakazi ungeweza kuhakikishiwa? Kama Waziri wa Mambo ya Nje, nilishirikishwa kwa kina katika majadiliano haya na mipangilio. Suala ya usalama ni sehemu muhimu zaidi. Nilisema awali, kulingana na tulivyojifunza, Mwenyekiti Mao alimuamini Waziri Miuu Zhou kusimamia miradi yote muhimu ndani na nje ya China. Akili nyingi za kiutawala za Waziri Mkuu Zhou zilikuwa za kishujaa na zilionekana wakati wote wa ujenzi wa TAZARA. Alikuwa mtu wa vitendo sana na alifuatilia kila hatua ya kazi, akitoa miongozo kwa vitendo na hasa katika kuhakikisha usalama na ushirikiano wa juu zaidi miongoni mwa wafanyakazi wa nchi tatu zilizokuwa zikijenga TAZARA.

Nina kumbukumbu nzuri ya Waziri Mkuu Zhou Enlai. Ziara yake nchini Tanzania ilikuwa ni alama ya manufaa ya wote kwa urafiki wa Tanzania na China.

(Makala ni masimulizi ya Hayati Job Lusinde kuhusu ziara ya Waziri Mkuu Zhou Enlai Juni 1965 wakati akihojiwa na Bwana Walter Bhoya, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Wachapishaji ya Mkuki na Nyota tarehe 27 Machi 2019)

Habari Kubwa