Man U wasaka beki kuumia kwa Young

24Jan 2016
Nipashe Jumapili
Man U wasaka beki kuumia kwa Young

ENGLAND. Louis van Gaal amethibitisha kuwa Manchester United wanapamba kuhakikisha wananasa beki kisiki kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa mwezi huu baada ya klabu hiyo yenye matumaini finyu ya kutwaa ubingwa kuandamwa na majeraha kufuatia kuumia kwa Ashley Young.

aSHLEY YOUNG

United walikaribisha Southampton kwenye Uwanja wa Old Trafford bila nyota wao wanne wa kikosi chya kwanza baada ya Young (atakayekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuumia nyonga) kuunga na Luke Shaw (amevunjika mguu), Marcos Rojo (ameteguka bega) na Antonio Valencia (majeraha ya enka).
“Young amepata majeraha makubwa ya nyonga na anatakiwa kufanyiwa upasuaji,” Van Gaal alisema. “Kwa hiyo, wakati tukilazimika kumsubiri kwa muda mrefu apone, tunapaswa kusaka mchezaji ambaye anaweza kucheza kama beki wa pembeni. Sasa tuna mabeki wanene wa pembeni ambao ni majeruhi. Hii inashangaza namna tulivyoweza kuwa katika hali hii msimu huu, lakini bado ni tatizo.”
Licha ya Ashley Cole kuwa huru baada ya kuondoka Roma, inafahamika kuwa United hawako tayari kumsajili beki huyo (35).
“Ni [Matteo] Darmian tu aliye 'fiti', ninahitaji mabeki wa pembeni,” Van Gaal alisema. “Ugumu wake ni kwamba tunahitaji kiwango fulani na tunaangalia uwezekano wa kupata, lakini si rahisi."

Habari Kubwa