Wahalifu wafichuliwe kila kona

22Sep 2016
Mhariri
Nipashe
Wahalifu wafichuliwe kila kona

NALIPONGEZA Jeshi la Polisi kwa juhudi kubwa linazofanya kupambana na uhalifu katika Jiji la
Dar es Salaam na kwingineko.

Ingawa siyo rahisi kabisa kukomesha tabia ya ujambazi, lakini hata wao sasa wamekuwa wakienda kwa tahadhari.

Hata hivyo, kuna jambo ambalo nataka kulisemea leo ambalo kwa kiasi kikubwa naona kama linachangia kupunguza kasi ya jeshi letu kupambana na wahalifu. Kuna watu ambao kwa sababu wanazozijua wao
wanasaidia wahalifu ama kuwaficha.

Kama si kuwepo kwa watu wanaoshirikiana na wahalifu, inawezekanaje
siri kwamba taasisi fulani leo inakwenda kuweka ama kuchukua pesa benki ifichuke?
Majambazi wanafahamu.

vipi kwamba leo ndiyo siku ya watu fulani kwenda kuchukua mishahara ama kuweka pesa za mauzo benki?
Hapa lazima kuna mtandao mkubwa tu wa watu wanaowapa tafu wahalifu. Na kama mtandao huu hautavunjwa, kasi ya
polisi kupambana na ujambazi, itakosa nguvu.

Naomba wananchi watoe ushirikiano wa hali na mali ili kundi hili la wasaliti lianikwe hadharani na kuchukulia
hatua kali.

Habari Kubwa