Mawasiliano ya simu sasa yazingatie maadili ya jamii

22Jan 2016
Christina Mwakangale
Nipashe
Mawasiliano ya simu sasa yazingatie maadili ya jamii

KWA kipindi cha cha karibu muongo mmoja sasa, teknolojia habari na mawasiliano imekua kwa kasi Tanzania hata kuchangia ongezeko la watumiaji wa simu za mkononi.

Takwimu zinabainisha kuwa Mwaka 2008 kulikuwa na watumiaji wa simu milioni tatu, idadi ambayo sasa imeongezeka maradufu.
Sasa Watanzania wengi vijijini na mijini wanamiliki simu za mkononi. Hali halisi ilivyo ni kwamba Watanzania wawili kati ya mmoja ana simu,ikiwemo katika kila kaya 10, nane zinamiliki walau simu moja ya mkononi.
Simu hizo za mkononi katika karne hii ya 21, zimekuwa zikitengenezwa kwa utaalam mkubwa, kuwezesha kupata taarifa kwa haraka zaidi na kuchangia mabadiliko makubwa.

Ulimwengu huu wa digitali, umeyafanya mawasiliano kutoka upande kutoka upande mmoja wa dnia kwewmda mwingine kuwa rahisi zaidi na kwa haraka zaidi.Dunia ya sasa ni kama kijiji kimoja kikubwa.

Baadhi yao wamekuwa wakitumia simu zao kupiga picha au kutuma picha katika mitandao ya kijamii hivyo kuharakisha upatikanaji wa habari.

Hii inatokana na ushindani uliopo kwa kila mtu kuwa na hamu ya kutaka kuwa wa kwanza kuihabarisha jamii na mengineyo.

Nia yangu si kukatisha tamaa wale wanaokuwa wa kwanza kutuhabarisha papo hapo (yaani breaking news), lakini mkazo uwe kuzingatia maadili.

Jamii ianze kujitambua kwa kubadilika na kutumia simu zao vizuri kwa kufuata maadili na muhimu kukumbushana ili kuzingatia hilo.

Mabadiliko yanaanzia kwa mtu mmoja mmoja na tuanze kujirekebisha katika hili, ila si kuacha kufikisha taarifa hata pale ni muhimu kufanya hivyo.
Kila kitu katika jamii kikiwa na uhuru uliopitiliza ni vurugu.Uhuru usio na mipaka haufai na tena ni hatari.Kila jambo linatakiwa kuwa na kiasi.
Kimsingi kinachotakiwa ni kwa jamii kuhakikisha kuwa, inatumia vyema uwepo wa teknolojia hiyo, ili kuleta mabadiliko chanya na si vinginevyo.
Isifike mahali, uwepo wa teknolojia hiyo ukaonekana kama hauna faida kubwa kwa kufunikwa na matumizi mabaya au yasiyostahili yanayofanywa na baadhi ya watu, ambao kwa sababu wenyewe wanajituma kufanya hivyo.
Jamii inatakiwa kuachana kabisa na mienendo isiyofaa ili kuifanya jamii inufaike zaidi na ukuaji wa mawasiliano, badala ya kujuta, hata baadhi kufikia hatua ya kutamani kuona kuwa afadhali tungeishi bila ya kuwa na teknolojia hiyo, kuliko kuwa nayo kisha inaleta madhara ya kuisambaratisha jamii au kuchangia mmonyoko wa maadili na mengineyo.
Kama kuna makosa yamefanyika ni kwamba, kinachotakiwa ni kubadilika na kuchukua njia sahihi.Linalowozekana leo lisingoje kesho.

Habari Kubwa