Mshindi Jackport akabidhiwa kitita

12Feb 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Mshindi Jackport akabidhiwa kitita

YASSIN Ally ambaye aliibuka mshindi wa Jackpot ya SportPesa amekabidhiwa zawadi yake ya hundi ya Sh. milioni 437.6 kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Mshindi wa Jackport SportPesa, Yassin Ridhiwani (Kushoto), akipokea mfano wa hundi ya Sh. milioni 437. 6 kutoka kwa Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas (kulia). Katikati ni mke wa mshindi huyo, Rehema Omary. PICHA: MPIGAPICHA WETU

Yassin mkazi wa Ubungo jijini amepata zawadi hiyo baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 13.

Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi mfano huo wa hundi ya zawadi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas alimpongeza kwa ushindi huo.

Tarimba alisema kuwa wao SportPesa ni kampuni isiyobahatisha katika katika michezo hiyo na ndiyo maana wamekuwa namba moja hapa nchini huku akitoa shukrani kwa Watanzania kuwafikisha hapo walipo.

"Sh. milioni 437, siyo ndogo kwa Mtanzania wa kawaida, lakini kama SportPesa tunafarijika tukiona maisha ya Watanzania yakibadilika baada ya kushinda na SportPesa hivyo niwatake Watanzania waendelee kubashiri nasi kwani kila wiki SportPpesa itakuwa ikitoa mamilionea.

Alisema SportPesa inatoa zawadi kwa kila mshindi anayeshinda bila kuangalia mazingira anayotokea ili mradi awe na umri kuanzia miaka 18.

“Tunachukua fursa hii kuwashukuru washindi wetu wa wiki hii na kuwaomba watumie vema pesa walizojishindia kwa ajili ya kuendeleza maisha yao, pia ni faida kwa serikali ambayo kwa kupitia ushindi wake kumeinufaisha kwa kukatwa Sh. milioni 87 iliyokatwa kwenye kodi.”

“Kuna washindi wengine pia waliojishindia mechi 10, 11 na 12, hivyo SportPesa tunawazawadia hata wale ambao hawakufanikiwa kubashiri mechi zote 13 kwa usahihi”

Naye Yassin alisema alianza kubashiri na SportPesa takribani miezi mitano iliyopita na alipata hamasa zaidi baada ya kuona washindi wa Jackpot wa kitita cha Sh. milioni 825.

“Nilianza kucheza na SportPesa miezi mitano iliyopita baada kuwaona Magabe na Kingslay wakikabidhiwa cheki yao, niliamini na kuanza kucheza. Nashukuru Mungu leo nimeibuka kuwa mshindi.”

Naye Mwakilishi wa Michezo ya Kubahatisha Kitengo cha Ilala, Haule Philip alisema: “Ushindi unaopatikana wa SportPesa unakuwa wa uwazi na ndiyo maana Yassin ambaye mshindi leo hii yupo hapa mbele kwenye vyombo vya habari.

“Ushindi huu wa Yassin umeongeza mapato serikali ambaye yeye anakatwa Sh. Mil 87 ambazo zote zinaingia serikalini, kikubwa ni kumtaka mshindi huo aendelee kuzitumia pesa hizo vizuri, alisema Philip.

Elibariki Sengasenga, Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, alisema SportPesa ni sehemu ya michezo ya ambayo serikali inaratibu, hivyo tuwapongeza kwa hatua waliyofikia katika michezo hii.

Habari Kubwa