Kaze aeleza siri straika wawili kuibeba Yanga

27Oct 2020
Adam Fungamwango
Dar es Salaam
Nipashe
Kaze aeleza siri straika wawili kuibeba Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amesema amegundua kuwa viwanja vya mikoani kama timu inataka kufanya vizuri ni lazima achezeshe mastraika wawili kutokana na namna vilivyo na jinsi timu nyingi zinavyolazimika kucheza mipira mirefu.

Akizungumza baada ya mechi kati ya timu hiyo dhidi ya KMC ambayo walishinda mabao 2-1 katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Kaze raia wa Burundi ambaye hiyo ni mechi yake ya pili kuiongoza Yanga huku zote akiibuka na ushindi, alisema timu nyingi wanazocheza nazo zikicheza kwenye viwanja hivyo mara nyingi hucheza mipira mirefu, hivyo inakuwa ngumu kucheza na straika mmoja, jambo ambalo aliamua kumtumia Waziri Junior kama straika wa pili, huku Michael Sarpong akiwa namba moja na matunda yake kuonekana....epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa