Ronaldo ameichoka Man United

12Jan 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Ronaldo ameichoka Man United

CRISTIANO Ronaldo amemwambia wakala wake Jorge Mendes kwamba anataka klabu mpya kutokana na kuchoka kucheza Manchester United.

Kwa mujibu wa mtandao wa michezo wa Sport nchini Hispania, uhusiano mzuri wa Mendes na Rais wa Barcelona Joan Laporta pamoja na uhitaji wa magoli wa Kocha Xavi Hernandez unafanya kuwapo kwa uwezekano wa Ronaldo kuhamia Nou Camp majira ya kiangazi.

Mendes atawasilisha jina la Ronaldo kwenye meza ya Barcelona kuhusiana na kile kitakuwa uhamisho wa kusisimua wa nyota huyo wa zamani wa Real Madrid.

Ronaldo alijiunga na Manchester United akitokea Juventus msimu huu saa chache baada ya uvumi kuenea alikuwa mbioni kujiunga na Manchester City.

Habari Kubwa