Vita Ligi Kuu Bara yahamia Zanzibar

11Jan 2021
Hawa Abdallah
Zanzibar
Nipashe
Vita Ligi Kuu Bara yahamia Zanzibar

TIMU za Simba, Yanga na Namungo, tayari zimetinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi huku Chipukizi na Jamhuri za visiwani hapa zikishuhudiwa zikiaga michuano hiyo sambamba na bingwa mtetezi, Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani Morogoro.

Kuingia nusu fainali kwa timu hizo tatu za Bara huku Azam FC nayo jana jioni ambayo ilikuwa ikivaana na Mlandege ya visiwani hapa, ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kushinda na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo iliyoshirikisha timu tisa mwaka huu.

Timu za Bara zimeongeza mvuto mkubwa kwa mashabiki wa hapa na kila zinapocheza wamekuwa wakijazana uwanjani kuzishuhudia, hivyo nusu fainali kati ya Simba na Namungo na Yanga dhidi ya mshindi wa mechi ya jana kati ya Azam na Malindi ni mechi ambazo zitavuta mashabiki wengi zaidi visiwani hapa....Soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa