Yanga hawajakata tamaa na ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu

15Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Yanga hawajakata tamaa na ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu

NAHODHA wa timu ya soka ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam, Lamine Moro, amesema bado kikosi hicho cha mabingwa wa kihistoria hawajakata tamaa ya kusaka ubingwa wa Ligi kuu kwa msimu huu.

“Wanaodhani kuwa sisi tumekata tamaa na ubingwa, wanakosea sana kwa sababu wachezaji wote hapa mawazo yapo kwenye ubingwa" amesema Moro.

“Nimekuwa nikiona huko mitandaoni watu wakizungumza vibaya kuhusu timu na wanafikiri sisi tumekata tamaa, niwaambie kwenye maisha hakuna kukata tamaa, tutapambana hadi mwisho kuwania ubingwa wa msimu,"

“Tangu nimefika Tanzania sijawahi kuona mechi rahisi hasa kwa Yanga, ushindani huo umekuwa ukitufanya nasi tuzidi kuongeza juhudi ili kufikia malengo," amesema.

Habari Kubwa