‘Wapiga mbizi’ Dar wapongezwa

12Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar
Nipashe
‘Wapiga mbizi’ Dar wapongezwa

Klabu maarufu ya kuogelea ya Dar Swim Club imewapongeza waogeleaji wake kwa kufanya vizuri katika mashindano ya taifa ya kuogelea yaliyomalizika hivi karibuni katika bwawa la Hopac.

Waogeleaji.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro alisema kuwa waogeaji wake wameboresha muda wa kuogelea na kuipa ushindi wa kwanza klabu hiyo kwa upande wa wanawake kwa kukusanya pointi 1,964.50.

Inviolata alisema kuwa kwa upande wa wanaume, walikusanya pointi 1,086.50 na kushika nafasi ya pili. Alisema kuwa wamefarijika na matokeo hayo hasa kwa kuzingatia kuwa waliwakilishwa na waogeleaji chipukizi.

“Hii ni faraja kwetu, tumeweka mikakati ya kukuza mchezo wa kuogelea kwa miaka 10, tuna waogeaji wadogo wenye vipaji,” alisema.

“Wakati tunaanza, hatukutegemea kufikia hatua hii, tulitwaa medali 94 katika mashindano ya kuogelea ya Taliss na kushika nafasi ya kwanza na kuwa klabu bora.”

Alisema kuwa mafanikio ya klabu yao yametokana na ushirikiano wao na wazazi na wadhamini mbalimbali.

Habari Kubwa