African Lyon yaingia kambini Zanzibar

14Aug 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
African Lyon yaingia kambini Zanzibar

TIMU ya African Lyon ya Dar es Salaam imeingia kambini visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kocha wa Lyon, Ramadhani Aluko.

Kocha wa Lyon, Ramadhani Aluko ameiambia Lete Raha juzi jioni kwamba na ikiwa huko, timu hiyo itapata mechi kadhaa za kujipima nguvu.

“Tunataka kutumia vizuri kipindi hiki cha wiki ya mwisho ya maandalizi kuelekea Ligi Kuu, tukiamini kabisa tutakuwa na ligi ngumu, ambayo tunahitaji kuwa tumejizatiti ili kuimudu,”alisema Aluko, kocha wa zamani wa Simba SC.

Ikumbukwe, African Lyon timu ya zamani ya mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta itafungua dimba na Azam FC Uwanja wa Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Habari Kubwa