Ajibu: Kileleni chanzo Yanga kukamiwa

11Feb 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Ajibu: Kileleni chanzo Yanga kukamiwa

NAHODHA na mshambulijia wa Yanga, Ibrahim Ajibu, amesema wamekuwa na kipindi kigumu kwenye michezo yao ya ugenini kwa kukamiwa na wapinzani wao kutokana na wao kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara.

Ibrahim Ajibu.

Yanga imejikuta ikiambulia pointi mbili kati ya tisa katika michezo mitatu waliyocheza kabla ya mchezo wa jana dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa.

Akizungumza na Nipashe jana, Ajibu alisema kama wachezaji wanapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri licha ya ugumu wa michezo yao.

Alisema kuongoza kwenye msimamo wa ligi kwa muda mrefu kunawafanya wapinzani wao kuwakamia wakiamini wanacheza na timu imara.

"Tutapambana mpaka mwisho ili kutimiza lengo letu la kutwaa ubingwa msimu huu, bado tuna michezo mingi na nafasi ya kutwaa ubingwa ipo," alisema Ajibu.

Aidha, alisema baada ya mchezo wa jana watarejea Dar es Salaam kujiandaa na mchezo unaofuata.

Yanga inakabiliwa na mchezo dhidi ya watani zao, Simba uliopangwa kuchezwa Jumamosi Februari 16, wiki hii.

 

Habari Kubwa