Ajibu: Ni heshima kupewa unahodha

10Jan 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Ajibu: Ni heshima kupewa unahodha

NAHODHA mpya wa klabu ya Yanga, Ibrahim Ajibu, amesema kwake ni heshima kubwa ambayo ameonyeshwa na kocha wake Mwinyi Zahera ya kumpa jukumu la kuwaongoza wenzake.

Zahera, alimpokonya unahodha beki wake wa kati, Kelvin Yondani na kumpa mshambuliaji huyo baada ya Yondani kuonyesha utovu wa nidhamu.

Akizungumza na gazeti hili, Ajibu, alisema kuwa anafahamu majukumu ya unahodha na anatajitahidi kufuata kile kocha wake anachokitaka kutoka kwake.

“Ni jukumu kubwa, na ni heshima kupewa nafasi hii, nitahakikisha nafanya kile kocha ambacho anakitegemea kutoka kwangu, lakini pia nitashirikiana vizuri na wachezaji wenzangu kuhakikisha kila jambo linaenda vizuri,” alisema Ajibu.

Alisema malengo yao kama wachezaji ni kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri kwenye ligina hatimaye kuchukua ubingwa.

Yanga wanaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 50 baada ya kucheza michezo 18 wakifuatiwa na Azam FC wenye pointi 45 huku Simba waliocheza michezo 14 wakiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 33.

Mchezo ujao, Yanga watacheza na Azam kukamilisha michezo yao ya mzunguko wa kwanza kabla ya kuanza ngwe ya lala salama.

Habari Kubwa