Al Ahly wamnyima usingizi Cannavaro

04Apr 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe
Al Ahly wamnyima usingizi Cannavaro

NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema atamuomba kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van de Pluijm, ampange katika kikosi cha kwanza wakati watakapoikaribisha Al Ahly kutoka Misri kwenye mechi ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika itakayofanyika Jumamosi jijini Dar es Salaam.

nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro'.

Akizungumza na gazeti hili jana, Cannavaro alisema tayari mwili wake uko 'fiti' kucheza mechi hiyo na kuisaidia timu yake kupata ushindi.

Cannavaro alisema kwa muda aliokuwa nje ya uwanja, umemsaidia kupona na kupata muda mwingi wa kupumzika.
"Ninatamani kuanza katika mechi huyo, nimepanga kumueleza kocha kama nimepona na ninaweza kucheza," alisema Cannavaro.

Beki huyo wa kati aliongeza kuwa mbali na mechi za ligi, akili za wachezaji wa timu hiyo zilihamia kuufikiria mchezo huo, huku wakiweka lengo la kuhakikisha wanashinda ili kujiweka kwenye mazingira mzuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Yanga inakutana na Al Ahly baada ya kuiondoa APR ya Rwanda wakati mabingwa hao wa kihistoria wa Afrika wakiwafunga mabao 2-0 Reacreativo do Libolo ya Angola.

Habari Kubwa