Alliance waanza kuitisha Yanga

23Mar 2019
Faustine Feliciane
Dar es Salaam
Nipashe
Alliance waanza kuitisha Yanga

WAKATI bado wakiwa katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila, amesema kuwa wapinzani wao Alliance FC si wa kuwabeza na wanapaswa kujipanga vizuri.

Mwandila alisema kuwa kurejea uwanjani kwa nyota wake Ibrahim Ajibu kutasaidia kuongeza nguvu na kuimarisha mikakati ya kufanya vema katika mechi hiyo ya hatua ya robo fainali ya Kombe la FA itakayochezwa Machi 30 kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba jijini Mwanza.

“Hautakuwa mchezo mwepesi, tumeona kwenye mchezo wetu wa ligi ambao tulifanikiwa kupata ushindi, lakini hali ya upinzani ilikuwa kubwa sana… wapinzani wetu ni wazuri sana hasa wanapocheza nyumbani,” alisema Mwandila.

Aidha, alisema wanapaswa kuwaheshimu wapinzani wao kama wanataka kupata matokeo mazuri katika mechi hiyo na hatimaye kusonga mbele katika michuano hiyo.

Habari Kubwa