Arsenal pungufu waikamata Spurs nyumbani

06Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Arsenal pungufu waikamata Spurs nyumbani

ARSENAL pungufu jana ilipambana kiume na kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Tottenham Hotspur katika mechi kali ya Ligi Kuu England ‘dabi’ iliyozikitanisha timu jirani jijini London.

Wachezaji wa Arsenal

The Gunners walilazimika kucheza sehemu kubwa ya kipindi cha pili wakiwa 10 uwanjani baada ya Francis Coquelin kuonyeshwa kadi nyekundu mwanzoni mwa kipindi hicho.

Spurs wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo, walianza mchezo wakiwa pointi tatu mbele ya Arsenal, walitumia mwanya wa kadi nyekundu ya Coquelin dakika ya 55 kufunga mabao mawili ya haraka haraka, kabla ya Alexis Sanchez kufunga bao la kusawazisha kwa Arsenal dakika ya 76.

Arsenal iliyokuwa ikicheza bila kipa wake namba moja, Petr Cech na nafasi yake kuchukuliwa na David Ospina, walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa Aaron Ramsey katika dakika ya 36.Matokeo hayo yameiacha Arsenal nyuma kwa pointi tano dhidi ya vinara wa msimamo, Leicester City.

Habari Kubwa